Self-Contained Houses: Kuna umuhimu gani wa kuwa na choo pamoja na bafu "separately"? Kwanini hivyo nyumba viwili visiwe na matumizi yanayofanana?

Self-Contained Houses: Kuna umuhimu gani wa kuwa na choo pamoja na bafu "separately"? Kwanini hivyo nyumba viwili visiwe na matumizi yanayofanana?

Shida zipo ukichanganya bafu na choo. Maji ya bafuni yana sabuni ambayo huuwa bacteria wanaobadirisha haja kubwa kuwa maji. Ndio maana kuna tank 2, ya pembe 4 na ya mduara.
Vema, lakini lile la pembe 4 na la duara pia huwa yanaungana, hapo inakuwaje?
 
Kwa kifupi mkuu ujenzi mwingi hapa bongo watu wana copy na Ku paste..
Ukiuliza kwann nyumba nyingi chini wanapaka rangi nyeusi,,au wanapaka rangi tofauti na rangi ya ukuta wa juu ,,majibu hakuna,
Nyumba nyingi ni mfumo wa sketi na blauzi..
Rangi nyeusi inayopangwa chini inazuia mchwa
 
Ndio yana kuja kukutana kwenye shimo la pili ambapo kwenye shimo la kwanza ni kinyesi tu na maji ambayo yametumika kusafirisha kinyesi na mkojo
Kwann tank za pembe 4 na duara. Na isiwe zote mbili pembe 4 au zote zikawa duara.
 
Sasa mjeshi kwa hiyo hujui kwamba kule nje kuna mashimo 2? La mstatili na lile la mviringo? Au septic tank and soak away pit??
Ninajua kwamba kule nje kuna mashimo 2 lakini sijui kazi zake ni nini mkuu. Alafu mimi ni raia sio mjeda.
 
Kwa ujenzi wa kisasa una weka chumba kimoja kwa taka za ndani ya mwili kinyesi na mkojo na za nje kuoga kupiga mswaki n.k angalizo kama hauna hela za kutosha ni bora ukajenga kwa kutenganisha kwa sababu maji ya taka ya nje mwili na manisha yenye sabuni na kemikali kama shampool zina weza kuingia kwenye sinki la choo na kupelekea kuua backteria wanao mengenya kinyesi na kupelekea choo kujaa haraka ni hayo tu
Watu wengi hawajui hii wallah
 
Umejibiwa akija mama mkwe ameenda chooni na wewe unataka ukaoge uende kazini utamgongea umwambie toka mama nataka kuoga???
Kwanini nimgongee wakati kuna chumba cha pili chenye huduma kama hicho chumba alichopo yeye.
 
Kwanini uoge CHOONI..wakati choo Ni kwakujisaidia..na Kuoga Ni kuoga

Nyumba nyingi zakupanga zinachoo na bafu hapo hapo... Unaenda kuoga asubuhi...mikojo inanuka vibaya mno na usiombe mtu awe kajisaidia hajasifisha vizuri. Unaanza kusafisha kwanza..nyumba za wapangaji wengi..choo Cha nje.


Nadhani hivi vitu vibaki separate.
 
Back
Top Bottom