Selim bin Abakari, mtu mweusi wa kwanza kufika Siberia Watu wa kule wakadhani ni Mungu

Masai ameanza kutengeneza vitu vyake lini?
Matairi anayovaa...migolole hadi shanga wananunua
Umeona matairi tu !! Jaribu kwenda Ngorongoro unakone wako unique ebu tafuta mzungu au mtu wa nje muulize kuhusu kabila gani kubwa Tz .
 
Hebu wela link ya hicho kitabu cha safar za wasuaheli.
 
Jambo jema alikutana na mkoloni asiye mchoyo.
Ingekuwa mkolon wa jangwani nani angemruhusu hiyo mikato?
Kwanza angehasiwa na kuvaa kitumwa.
Acheni mzungu aitwe mzungu
Brainwashed Hadi huruma
 
Attachments

Kuna huyu Mngazija mmoja mwenye akili sana aliyeitwa Selim bin Abakari. Wakati Wajerumani ndiyo wanaanza kutawala Tanganyika huyu Selim Alikuwa akifahamu kijerumani, hivyo akaajiriwa na afisa mmoja wa serikali ya Ujerumani kama mfanyakazi wake. walisafiri naye sana.

Safari ya kwanza ilikuwa ni kupeleka meli ya mvuke ziwa Nyasa. Walisafiri kupitia mto Zambezi, mto Shire na kuingia Malawi. Huko walifunga boti yao na ikaanza safari ziwa Nyasa. Walifika Kyela, wakaenda Ukinga, Unyakyusani, Kwa Chifu Merere wa Usangu, wakaenda hadi Rukwa na Zambia kwa wawemba. Selim ameandika yote hayo. Ameelezea vizuri mambo mbalimbali waliyokutana nayo.

safari ya pili wameenda na bosi wake Berlin ujerumani kutokea Dar. Wako na meli, wakaenda Unguja, Tanga, Mombasa, Lamu, Somalia, Misri hadi Napoli Italia. hapo walipanda Treni hadi Berlin. Kaeleza vizuri na hali ya kila mji waliopita.

Kutoka Berlin wakasafiri kwenda Urusi. Walienda St Petersburg kwa treni. Wakaenda hadi Moscow. Baadaye wakapanda boti na kusafiri mto Volga, huko wakachukua magari ya farasi kuelekea Siberia. Safari yao ilikuwa kufika milima ya Altai iliyo mpakani mwa China, Urusi, Mongolia na Kazakhstan. Kaeleza vizuri sana safari yake. Anasema huko Siberia watu hawajawahi kuona mtu mweusi. Walivyomuona walimnyenyekea sana, walijua yeye ndiye bosi wa msafara, maana watu weupe wamezoea kuwaoana.

Pia kuna watu huko wanaabudu Mungu wao ambaye ni Mweusi, Walipomuona Selim wakaanza kama kumsujudia, kwamba Mungu wao amerudi. Sidhani kama kuna mswahili amewahi safiri kama huyu bwana.
silimu-en-russie1.jpg

silimu-21.jpg

fb-couvsilimu.jpg

Simulizi zake zinapatikana kwenye kitabu Safari za Wasuaheli(Waswahili) cha mwaka 1901.
Tunaomba soft copy
 
Kinapatikaneje hicho mkuu?
 
Back
Top Bottom