Mkuu,
Nilikuwa nafikiri hivihivi lakini nikaona ngoja nikae kimya nisije kuambiwa nina bias.
Lakini, kwa sababu wewe umelianzisha hili, nataka kukuunga mkono.
Na kabla sijashambuliwa na mashabiki, this has got nothing yo do with talent.
Mimi naona kuna mambo ya management, exposure na mixing/arrangement ya muziki zaidi kuliko talent ya msanii.
Ujue wenzetu ndiyo maana wana watu wengi sana sana utaambiwa huyu producer, huyu mixer, huyu sound engineer, huyu arranger, halafu sisi tunachukulia poa mtu mmoja anaweza kufanya kazi zote hizo.
Yani unaweza kupiga ala zote sawa, ukaimba sawa, kashehe ikaja kwenye mixing and arranging chombo gani kianze, wapi chombo gani kiwe muted wapi, flow ya wimbo iendeje, bridge ikae wapi, chorus ikae wapi, harmony ikae wapi. Identity ya wimbo ijulikane kwa chombo kipi.
Hapo panahitaji utaalamu wa hali ya juu.