Sema hii ngoma Harmonize aliandika tuache masihara

Sikuwahi kuizingatia, ila harmonize kwenye uandishi na melody katulia mnooo
 
Nakuunga Mkono, ngoma nyingi sana za harminize zina mistari mikali, melody nzuri ila biti unaiona ipo ipo tu si kali si mbaya.

Niliacha kusikiliza muziki rasmi 2014 hiv mpaka 15, lakini siku niliisikia ngoma ya wote, huwezi amini niliisaka, nikaisikiliza kwa kuirudia rudia, ndio nikazikuta ngoma nyingine nilizoziorodhesha... Nikajikuta namtengenezea playlist na yeye.

Maana ngoma zangu nyingi ni za kitambo
 
Aendelee kuvuta jani korofi ndio linaleta burudani zote hizo+kipaji,,Jani likikukubali lina hisia tamu katika kile ufanyacho
 
Duh! Siyo nzuri hiyo ina haribu akili
Kila Kitu Ni Kwa Kiasi Na Kwa Wakati Mamito,,Vyote Tutumiavyo Ukizidisha Tu Ni Either Uharibu Akili,,,Mwili Au Nafsi Au Vyote Kwa Pamoja Au Kimojawapo Kati Hivyo Au Viwili Kati Ya Hivyo Vitadhurika,,,Tujifunze Kuwa Na Kiasi Na Kufanya Vitu Kwa Kuzingatia Wakti Utafurahi Na Roho Yako Kipenzi Changu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…