Lengo langu lilikuwa nikisoma niwe na uelewa ambao utaniwezesha kuunda vitu,,,kwa mfano niweze kujua formula za kuunda chuma, hizi sahan za plastic niziunde au hata za udongo, rangi nitengeneze mwenyewe, nilitaman vidonge watu watengeneze Tanzania, nilipoingia secondary hiyo elimu sikuikuta nikaambiwa hapo unasoma ni intro tu nikaamini nikifika advance ntaikuta iyo elimu ambayo naifikilia mimi nilipofika nikaona bado sijaipata iyo elimu ikanibidi nipambane tu kufaulu mitihani kwa kukalili maandishi na maformula nikiamini labda ntaikuta chui huwezi amini nimefika chuo ndo kwanza mnaingizwa deep mnasoma vitu ambavyo havionekani hata kwa uso wa kawaida,,kwa mfano ilikuwa kawaida sana kukalukuleti joto kama zile heat ethalapy nilkuwa nakalukuleti huku naumia hivi hichi ndo kilichonifanya nilipie ada mamilioni,, nikasema mbona hii ni manual tu ambayo hata nisipoijua naishi na kuna watu hawaijui na wanaishi, nikaanza kujizalau sanaaa,,em chukulia mfano ndugu yangu ile rice cooker ina material kama plastic, chuma, aluminium, switch, nyaya ya kuchomekea kwenye umeme, diode(LED) nilitegemea ivi vitu ndo tufundishwe jinsi ya kuviunda ila ikawa tofauti tunaanzia kwenye joto linalopanda na kuanza kuheat mchele afu kwa mahesabu makubwa yanayosumbua ubongo,,, jamani Afrika hatutoendelea kamwe kama hatutobadilika na elimu yetu hii