Senegal: Mwalimu wa Madrasa akamatwa kwa tuhuma za Kubaka Wasichana 27

Senegal: Mwalimu wa Madrasa akamatwa kwa tuhuma za Kubaka Wasichana 27

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
1686116660890.png

Jeshi la Polisi Nchini #Senegal, linamshikilia Mwalimu huyo ambaye amekuwa akitafutwa kwa wiki kadhaa baada ya kuripotiwa kuwafanyia kitendo hicho Wanafunzi wake wa Kike aliokuwa akiwafundisha kusoma Kurani.

Mshukiwa alitoweka baada ya shutuma hizo kuibuka mapema mwaka huu (2023) kufuatia malalamiko kutoka kwa baadhi ya Wazazi wa waathirika kuweka wazi vyeti vya matibabu vilivyoonesha waliingiliwa kimaumbile.

Kwa mujibu wa ripoti, kati ya waliofanyiwa vitendo hivyo ni pamoja na Watoto wenye chini ya miaka 15. Ikumbukwe kuwa Ubakaji haukuwa kosa la jinai Nchini humo hadi kufikia mwaka 2020 Serikali ilipoharamisha kwa kutunga Sheria inayohusu vitendo vya Ngono.

============

A Senegalese Koran teacher suspected of raping 27 of his female students was arrested on Monday after several weeks on the run, a police source said.

The man is accused of assaulting the students at his school in the holy city of Touba in central Senegal, a local police official said.

The suspect went missing after the accusations emerged earlier this year following a complaint from alleged victims who produced medical certificates, the source added.

He was arrested on Monday "after handing himself over to the police. After questioning, he was handed over to the gendarmerie," the official said.

The source said the teacher is accused of "raping 27 students" but did not provide precise details on the dates of the alleged crimes or the age of the complainants.

Local media reported that the alleged victims were "minors", implying they were under 15, and that the Koranic school has been closed.

The newspaper "Le Jour" wrote last week that the affair came to light when one of the girls refused to return to the school, where students learn about Islamic teachings, because the teacher "had sexual relations with her and all the other girls".

Touba is considered a holy city by the Mourides, a major Islamic brotherhood in the Muslim-majority West African country.

The arrest comes after opposition figurehead Ousmane Sonko was sentenced to two years in jail for inciting a young woman to "debauchery", although he was cleared of a rape charge.

Sonko's legal battles over the rape allegations had captured media attention for two years, but the issue of sexual violence faded into the background as the affair became increasingly politicised.

Senegal criminalised rape in 2020.

NATION
 
Ana umri gani huyo Mwalim? Inabidi watu wa hivi wasihishie kuhukumiwa tu, bali wapimwe na akili pia.

Watu wanaweza kuconclude kwamba ili jambo ni kawaida kwa walim wa madrassa, lakini kumbe ni ugonjwa wa akili ambao upo underrated/ignored.
 
Sasa hivi Ustaadh atahusishwa na dini nzima kuwa imebaka. Ni swala la muda tu huu uzi utabadilika kuwa battlefield ya waislam na wakristo.
 
Sasa hivi Ustaadh atahusishwa na dini nzima kuwa imebaka. Ni swala la muda tu huu uzi utabadilika kuwa battlefield ya waislam na wakristo.
Hakuna aliye salama!

Ni hali tunaipitia wote wenye watoto sasa hivi ni hofu kuu,hata wasiokuwa na dini hii hali inawakuta maana popote iwe mtaani hata shuleni haya yanaweza kutokea
 
Hakuna aliye salama!

Ni hali tunaipitia wote wenye watoto sasa hivi ni hofu kuu,hata wasiokuwa na dini hii hali inawakuta maana popote iwe mtaani hata shuleni haya yanaweza kutokea
huu ni uelewa wa wachache sana ndugu yangu.
 
Sasa hivi Ustaadh atahusishwa na dini nzima kuwa imebaka. Ni swala la muda tu huu uzi utabadilika kuwa battlefield ya waislam na wakristo.
Huwa hakuna Wakristo ambao huji engage kwenye hizo battlefield. Hao ni wale wanaojidhania kuwa ni Wakristo wakati sivyo. Ukristo si kuwadumaza wengine na kuwafanya waonekane hawana thamani.

Misingi ya Ukristo ni kutambua uwepo wa wengine pasipo kuwahukumu huku akijihesabia yeye haki juu ya wengine.
 
Wasichana 27, alifanya ubakaji kwa kipindi cha muda gani?? Mara nyingi sana stories za namna hii huwa ni za uwongo. Kuna mtu hapo anataka kumuweka kijana wake na aliopo yupo ngangari sasa anatafutiwa sababu.
 
Hakuna kitu kama hicho, acha uongo bibi. Ni Asalaam sio Adalaam.
Kasome vizuri post namba moja, utakutana na kipande hiki "Ikumbukwe kuwa Ubakaji haukuwa kosa la jinai Nchini humo hadi kufikia mwaka 2020 Serikali ilipoharamisha kwa kutunga Sheria inayohusu vitendo vya Ngono."

Kama ni uongo, mwambie mleta mada.

Huwa sikisii.
 
Back
Top Bottom