Nairobi: Tukio la kushangaza lilitokea Alhamisi katika kampasi ya JKUAT Karen baada ya msafara wa Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna kuzuiwa kuingia katika chuo hicho.
Sifuna alikuwa amealikwa na viongozi wa wanafunzi kuhudhuria Law, Policy and Governance Forum, iliyolenga kujadili sheria, sera na utawala.
Video ya tukio inaonyesha magari ya msafara wa Sifuna yakiwa nje ya lango la JKUAT Karen huku maafisa wa usalama na watu wengine wakiwa eneo hilo.
Kwa mujibu wa taarifa za Daily Nation, Sifuna alizuiwa kwa muda kabla ya baadaye kuruhusiwa kuingia chuoni na kufanya kikao cha faragha na uongozi wa chuo. Haijabainika ikiwa forum hiyo itaendelea kama ilivyopangwa.
Sifuna alisema kupitia mitandao ya kijamii kuwa uongozi wa chuo ulikuwa umeghairi hafla hiyo ghafla na kumzuia yeye pamoja na ujumbe wake kuingia.
Hafla hiyo ilikuwa imeandaliwa na viongozi wa wanafunzi kama jukwaa la kujadili masuala ya sheria, sera na utawala.
Je, vyuo vikuu vinapaswa kuwa na nafasi zaidi kwa wanafunzi kujadili masuala ya uongozi na sera?
Source: Nation media