Uchaguzi 2020 Sera ya majimbo itaua utaifa na uzalendo

Sera ya Majimbo mimi kwa uelewa wangu ni sawa na familia ya baba na mama ambao wamefanikiwa kuwa na watoto na wajukuu... Ishara na kitovu cha ugatuzi wa madaraka!

Kila mtoto/mjukuu atakua nae ataanzisha familia yake "jimbo lake".
Serikali kuu kama baba na mama... Serikali za majimbo kama uzao wao...!! Na uhusiano/ushirikiano unaendelea vizuri tu!
Kuna mambo mengi muhimu tu ya kuendelea kutegemea kutoka kwa baba na mama... Lakini kuna mengine mengi tu ambayo kila jimbo linatakiwa liwajibike kuyamaliza...

Common sense inaelekeza kuwa mtu mzima kuendelea kumtegemea baba na mama kwa kila jambo ni udumavu wa akili na maendeleo...!! Ebu fikiria kama inaingia akilini baba na mama ndo wakupangie ama wakuamulie kila kitu kwenye maisha yako ndani ya jimbo lako...

Kama binadamu walivyo na changamoto; mfumo wa majimbo nayo lazima utakuwa na changamoto zake... Jukumu letu ni kuzibaini changamoto na kuzitatua ipasavyo...

Itoshe tu kusema kuwa faida za majimbo kwa "linchi likubwa" kama Tanzania ni kubwa kuliko hasara zake...!
Mfumo wa sasa ni wa kikoloni na kinyonyaji! Ebu fikiria juzi kwenye kampeni JPM kafika eneo fulani alafu anampigia Jafo simu atume pesa ili ikafanye kazi ya kukamilisha barabara...!! Ni wazi kuwa wale wananchi wangelimaliza lile tatizo wenyewe Kama lingekuwa ndani ya uwezo wao bila kumsumbua Jafo/JPM ambao hakuona umuhimu wa kulimaliza kabla...

Yaani uzalishaji tufanye sisi... kodi tulipe sisi alafu maji ya matope tunywe sisi...na wewe hadi ujisikie ndo utupatie ufumbuzi... Kwingineko tunaambiwa kuwa tutaendelea kukosa maendeleo kisa hatuchagui kama unavyotaka wewe...

Yaani viongozi wote uwalete wewe.... Why tukaliwe kiasi hiki...!!

Woga wetu ndo kikwazo cha maendeleo yetu...!!!
 
Acha kubisha kitu usichokifahamu mkuu tafuta habari ziko mtandaoni, AU haina jeshi rasmi, ila ukitokea mzozo wa kundi fulani kugawa nchi, kila mwanachama wa AU atatoa wanajeshi wake kwenda kupambana na kundi la uasi!
Wewe ndio huelewi unadandia manbo juu juu. Yale majeshi ya Tanzania yaliyoko Kongo nani anagharamia? Kule Somalia nani anagharamia yale majeshi ya Afrika? Au unafikiri ni suala la kuchanga majeshi tu? Africa nzima haina uwezo wa kuendesha operesheni yeyote kijeshi bila kugharimiwa na mataifa nje ya Afrika financially, logistically na kwa vifaa.

Soma vizuri hoja yangu halafu ndio ujibu.
 
Mfumo wa Majimbo utakuwa na athari hasi kwa Muungano wetu tuwe makini
 
Tayari mmechafuka kwa hiii sera ya majimbo, bora mjitoe tu uchaguzi hamtaaminiwa tena. Mmeatamia jiko la moto, ukiatamia jiko la moto litakuunguza tuuu, hata lisipokuunguza kama halina moto litakuchafua kwa majivu.Poleni wana chadema siasa ndiyo hiyo. JIANDAENI NA UTETEZI MWINGINE KWA SERA YENU YA KUWEKA DHAMANA MALI ZA NCHI ILI MUWEZE KUKOPA.Hahahahahaha mwaka huu mnalo.

Sasa hivi ccm wanawabomoa kwa sera zenu mlizotunga wenyewe.Inaonekana zilitengezwa na wazungu mkapewa kwenye bahasha bila ku proof read. Yaani ccm sasa hivi wanabonyeza kitufe cha sera za chadematu kitu kinalipuka
 
Tunaomba aliye na ilani ya chadema aiweke humu, mgombea wa ccm ndugu Magufuli katushauri tuisome tushangae yaliyomo
 
Tumechafukwa kivipi wakati watanzania wanaiunga mkono sana???
 
Kwahiyo Wamarekani hawana utaifa wala uzalendo au?
China Japan South Africa Uk kote wanatumia mfumo wa majimbo ambao ni vigumu Serikali kuu kuchukua pesa za jimbo kienyeji kufanya mambo yasiyo na tija kama CCM walivyofanya kununua Ndege kujenga chato Airport kienyeji pasipo idhini ya bunge
 
Kwahiyo Wamarekani hawana utaifa wala uzalendo au?
Jimbo moja tu la Texas lina ukubwa sawa na Tanzania.

Atakayekuja na wazo la kuiunganisha afrika ikawa ni nchi moja yenye sarafu moja, huyo atakuwa na nia ya kuigeuza Tanzania ikawa ni jimbo mojawapo kati ya majimbo ya Afrika.
 
China Japan South Africa Uk kote wanatumia mfumo wa majimbo ambao ni vigumu Serikali kuu kuchukua pesa za jimbo kienyeji kufanya mambo yasiyo na tija kama CCM walivyofanya kununua Ndege kujenga chato Airport kienyeji pasipo idhini ya bunge

Kununua ndege ni jambo halina tija?..mkuu naona umechafukwa.

Hao uliowataja misingi ya mataifa yao haifanani na misingi ya kwetu. Wengine walipigana vita hivyo hayo majimbo yao hayakuibuka tu.
 
Mfumo wa majimbo ni bora zaidi ya mfumo tuliokuwa nao sasa wa kuwa na RC ambao ni mfumo wa hovyo usio na tija ndiyo maana mpaka sasa Tanzania ina miaka 59 haina maendeleo pesa zote za viwanda zinatumika kudhoofisha chadema kuua upinzani kuhujumu kukandamiza demokrasia badala ya maendeleo
 
CCM wengi hata hawaelewi ukiwauliza mfumo wa majimbo ukoje Yaani wamekaririshwa tu na ukilaza wao. Wengine wanaamini Majimbo ya wabunge ndo yatakuwa majimbo wengine wanasema Eti Mkoa ndo utakuwa jimbo, yaaani ni vilaza watupu 😂😀😀
 
Kununua ndege ni jambo halina tija?..mkuu naona umechafukwa.

Hao uliowataja misingi ya mataifa yao haifanani na misingi ya kwetu. Wengine walipigana vita hivyo hayo majimbo yao hayakuibuka tu.
Ndege zikinunulia kwa mfumo bora kwa bei nafuu huleta tija lakini kununua Ndege kwa cash huku wajanja wachache wakiwa na 10% humo ni ufisadi na ununuzi wa Ndege wa aina hii hauna tija kwani Ndege hazitengenezi faida sana sana zimekuwa mziko kwa Taifa
 
CCM wengi hata hawaelewi ukiwauliza mfumo wa majimbo ukoje Yaani wamekaririshwa tu na ukilaza wao. Wengine wanaamini Majimbo ya wabunge ndo yatakuwa majimbo wengine wanasema Eti Mkoa ndo utakuwa jimbo, yaaani bi vilaza watupu 😂😀😀
Ha ha ha CCM watajifunza kupitia South Africa inatosha au wajifunzie kenya basi
 

Yaani mshukuru kuwa waTanzania mmewafanya mazezeta waamini katika ahadi zenu hewa miaka nenda rudi hata katika yale yaliyo haki kwao...

Siku wakizinduka mtabaki historia...
Hizo Sera za CDM zinatekelezeka kuliko za zilizofeli tokea nchi ipate Uhuru... Ndo maana mnaahidi hiki mnatekeleza msiyoahidi...

Hao wazungu msiowataka kila leo mnawainamia na kuwasujudu wawasaidie...
Shame on you bigots; rubbish pits!
 
Usione vyaelea. Unajua imewagharimu kiasi gani kufika hapo walipo?.
Kwahiyo unataka rais aendelee kuwa ndiyo mgawa riziki ktk mikoa? Tunatka madaraka yarudi kwa wananchi.
 
Rais anateua wakuu wa mikoa,wakuu wa Wilaya, wakurugenzi wote wa Halmashauri,makstibu wakuu,mabalozi, mawaziri nk nk. Tunachotaka wakuu wa mikoa na wakuu wa Wilaya wagombea na kupigiwa kura Kama wabunge.
 

Mnachosahau ni kwamba maendeleo halisi yanatofautiana kati ya mkoa mmoja na mwingine.

Ukianzisha majimbo umeanzisha aina fulani ya mashindano na dharau miongoni mwa watu wa majimbo hayo.

Leo hii hakuna majimbo unakuta watu wa kaskazini wanawadharau watu wa kanda ya kati, ukianzisha majimbo hizo dharau hazitapungua na zitaivunja nchi.

Sisi tuna utaifa wenye miaka mingi. Maury’s kaoa mnyakyusa, Mhaya kaoa mgogo, mmakonde kaoa mhaya.

Tangu mwanzo kabisa wa ujenzi wa nchi nguvu ilitumika kujenga utaifa, ukija na sera ya majimbo huo utaifa hautabaki salama.
 
Kwanza Embu tuambie unaelewaje ukisikia sera ya majimbo?
 
Kwani sera ya majimbo inasema hakuna kuoana??? China Mtu wa Shanghai hawezi kuoa Beijing??? Ndo unavyoelewa hivyo Sera za majimbo wewe kilaza wa Lumumba???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…