Uchaguzi 2020 Sera ya majimbo itaua utaifa na uzalendo

Watu wanadhani utatuzi wa shida zao utaletwa na majimbo.

Ni roho za choyo zinazowasumbua.
 
Ubaguzi wao hautokani na ugawaji wa majimbo. Ni ishu ya tangu ukoloni kama ilivyo Rwanda ama Burundi. Jingine?

Mkuu jimbo la kaskazini unaweza kulilinganisha na la kusini?.

Acheni hizi hulka za kibinafsi hazilisaidii taifa.
 
Marekani, Hispania, Ujerumani, canada, Nigeria,..... kuna majimbo pia, utaifa wao umekufa? Ili kulisaidia taifa lazima tutuo hoja zenye ushahidi. Rasilimali zetu hazitumiki na hazilindwi ipasavyo kwakuwa zinaonekana kama vile hazina mwenye, mwenyewe yuko Ikulu. Serikali ya jimbo ina tabia ya kuthamini na kuwa na wivu na rasilimali zilizomo jimboni. Serikali ya jimbo ina tabia ya kubuni na kutumia kila kitu ndani ya jimbo ili kuinua hali ya maisha ya wanajimbo wake na kuichangia serikali kuu pia kwaajili ya zile kazi za kitaifa kama ulinzi, usalama, fedha, nk. Tofauti na sasa ambapo wilaya na mikoa inasubiri serikali kuu ilete maendeleo na matumizi ya wilaya na mikoa.
 
Mimi ni muumini wa mabadiliko, Lakini hii sera ya majimbo sikubaliani nayo kwa kweli. Inaweza kuchangia kutugawa kama yanayoanza kujitokeza India ya kuanza mabifu baina ya state hii na hii, India kumeanza tension japo ni ndogo bado baina ya Maharashtra na Bihar tena mpaka kwa wananchi, na pia kudumazisha baadhi ya maeneo ambayo hayana resources nzuri za uzalishaji wa kuleta maendeleo.
Nakubwa kiupande wangu ni ile hali ya kila jimbo kuwa na sheria zake zakiutawala hilo ndio taizo kuu. Unaweza kukuta eneo la huku jimbo Fulani ni uhalifu eneo la huku siuhalifu. hapo nipo penye tatizo Sheria ikiwepo itumike kwa sote.

Ila Pia mikoa imekua ni mingi sana, inahitajika kupunguzwa sana, Nchi imeja ma RC na DC wasiokua nu uweledi wowote.
 
Utaifa wa kuchukua fedha za Ngorongoro,Kilimanjaro,Serengeti,Korosho,Gas na Tanzanite kwenda kujengea Chato International Airport bado unautaka.
 
kanda za majimbo zinahitaji uazishwaji idara nzima nzima za kiuongozi kama polisi,bunge la seneta na idara nyingi tu kiuongozi na kisheria

kanda za uchumi kutakuwepo na uwekezaji zaidi kwenye mihundo mbinu ya kiuchumi kama usafirishaji,umeme na masoko kulingana na kanda usika mfano dar es salaam ni kanda ya uchumi katika nyanda ya biashara zaidi kuliko uzalishaji
 
Kwani sasa hatuna polisi??? Haiwezi kutamkwa tu kuwa watakuwa wanahudumu eneo la jimbo fulani na ikawekwa kisheria???
Kwani sasa hivi hatuna bunge??? Hatuna mabaraza ya madiwani????? Tofauti ni nini???
 
Umeona nyomi la Lissu Geita leo..huyo mtu wenu hata anakojifanya kwao hawamtaki.....
 
Sera za majimbo haziendani na desturi,tabia na utamaduni wa kitanzania wenye kuishi pamoja kwa kuchangia raslimali zilizopo. Iwapo kuna hofu ya matumizi mabaya ya raslimali kwa mfumo uliopo zipo sheria za nchi zisimamiwe ipasavyo.
 
Upo uzalendo wa Aina tofauti kwa jinsi tulivyo jipambabua kamataifa hivi leo, Kwanza ni uzalendo maslahi na pili ni uzalendo halisi. Hivyo hapa tulipo mengi yanayohitaji mabadiliko ili kuelekea uzalendo wakweli. Sasa hivi uzalendo maslahi umemeenea kwa mfumo uliopo kwa kichaka Cha uzalendo.
 
Kwahiyo Wamarekani hawana utaifa wala uzalendo au?
Mkuu umeenda mbali sana kuna Majimbo hizi nchi jirani ambazo hazitajwi... watutajie ni nchi ipi wenyewe hawana uzalendo na taifa lao kisha watuambie ni kwanini hapa kwetu kila uchao tunapoteza upendo na mshikamano wa kitaifa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…