Uchaguzi 2020 Sera ya majimbo itaua utaifa na uzalendo

Uchaguzi 2020 Sera ya majimbo itaua utaifa na uzalendo

Nimesikia chama kimoja kinazungumzia nchi kuigawa kwenye majimbo ya kiutawala na uendeshaji. Kwangu mimi kwa nchi ambayo imekuwa kwenye utawala wa mikoa kwa miaka zaidi ya 50 na kwa mfumo wa kugawana mapato kupitia serikali kuu na serikali za mitaa kwa baadhi ya mapato haileti mantiki kubadili mfumo kwenda kwenye majimbo ambayo yanaweza kuua utaifa na kuleta mfarakano. Mfumo wa sasa unaondoa u-mimi na maendeleo ya uchumi yanayopishana- Regional economic imbalances - ambao utaacha baadhi ya maeneo kwenye umasikini mkubwa. Baadhi ya athari zinazoweza kujitokeza ni pamoja na:

1. Maeneo yenye raslimali kidogo kuendelea kuwa maskini na maeneo mengine kuwa tajiri na hivyo kuwa na mchango mdogo wa GDP

2. Ajira ndogo kwenye baadhi ya maeneo yenye raslimali chache na hivyo ongezeko la idadi ya watu kwenye maeneo yenye utajiri wa raslimali

3. kila jimbo kuwa na sheria zake za kiutawala, bunge dogo, polisi nk hali inayoweza kujenga mwelekeo wa kujitenga. Rejea matatizo yakujitenga kwa Biafra Nigeria miaka ya nyuma.

4. Nchi zenye majimbo mf Msumbiji hazina hakikisho la maendeleo endelevu kuzidi ambazo hazina utaratibu huo ie Tanzania

5. Mfumo huo utakuwa na gharama kubwa kuuanzisha

Kimsingi hadi sasa mfumo uliopo hauna shida changamoto kubwa ni kuweka mifumo mizuri ya udhibiti matumizi na mapato ya serikali kwa kuyagawa kwa haki ili kila eneo la serikali liweze kunufaika. Na hususani kuimarisha mfumo wa Halmashauri uweze kukabiliana na changamoto za kiuchumi kwa kila eneo. Iwapo kuna changamoto za mgawanyo sawia basi tupitie upya sera na sheria zetu ndani ya mfumo uliopo tuboreshe.

6. Hata hivyo, Kwa maoni yangu badala ya utawala wa majimbo ni afadhali kuweka kanda za kiuzalishaji ili kuchochea uchumi wa kimaeneo kulingana na mazingira ya kiuchumi na uzalishaji kwa kila eneo.
Wewe rudia kuisoma sera uielewe.
Maana yake halisi ni kuwa watu wenyewe kwenye maeneo yao, yawe mikoa au wilaya, ndio wawe wanachagua au kuwateua viongozi wao, kama wakuu wa mikoa, wilaya na halmashauri.

Pia maeneo hayo, pamoja na Bunge, viongezewe madaraka ya kuamua badala ya Rais pekee.
 
Mfumo wa Majimbo utakuwa na athari hasi kwa Muungano wetu tuwe makini
Maana yake halisi ni kuwa watu wenyewe kwenye maeneo yao, yawe mikoa au wilaya, ndio wawe wanachagua au kuwateua viongozi wao, kama wakuu wa mikoa, wilaya na halmashauri.

Pia maeneo hayo, pamoja na Bunge, viongezewe madaraka ya kuamua badala ya Rais pekee.
 
Mnachosahau ni kwamba maendeleo halisi yanatofautiana kati ya mkoa mmoja na mwingine.

Ukianzisha majimbo umeanzisha aina fulani ya mashindano na dharau miongoni mwa watu wa majimbo hayo.

Leo hii hakuna majimbo unakuta watu wa kaskazini wanawadharau watu wa kanda ya kati, ukianzisha majimbo hizo dharau hazitapungua na zitaivunja nchi.

Sisi tuna utaifa wenye miaka mingi. Maury’s kaoa mnyakyusa, Mhaya kaoa mgogo, mmakonde kaoa mhaya.

Tangu mwanzo kabisa wa ujenzi wa nchi nguvu ilitumika kujenga utaifa, ukija na sera ya majimbo huo utaifa hautabaki salama.
Maana yake halisi ni kuwa watu wenyewe kwenye maeneo yao, yawe mikoa au wilaya, ndio wawe wanachagua au kuwateua viongozi wao, kama wakuu wa mikoa, wilaya na halmashauri.

Pia maeneo hayo, pamoja na Bunge, viongezewe madaraka ya kuamua badala ya Rais pekee.
 
Nimesikia chama kimoja kinazungumzia nchi kuigawa kwenye majimbo ya kiutawala na uendeshaji. Kwangu mimi kwa nchi ambayo imekuwa kwenye utawala wa mikoa kwa miaka zaidi ya 50 na kwa mfumo wa kugawana mapato kupitia serikali kuu na serikali za mitaa kwa baadhi ya mapato haileti mantiki kubadili mfumo kwenda kwenye majimbo ambayo yanaweza kuua utaifa na kuleta mfarakano. Mfumo wa sasa unaondoa u-mimi na maendeleo ya uchumi yanayopishana- Regional economic imbalances - ambao utaacha baadhi ya maeneo kwenye umasikini mkubwa. Baadhi ya athari zinazoweza kujitokeza ni pamoja na:

1. Maeneo yenye raslimali kidogo kuendelea kuwa maskini na maeneo mengine kuwa tajiri na hivyo kuwa na mchango mdogo wa GDP

2. Ajira ndogo kwenye baadhi ya maeneo yenye raslimali chache na hivyo ongezeko la idadi ya watu kwenye maeneo yenye utajiri wa raslimali

3. kila jimbo kuwa na sheria zake za kiutawala, bunge dogo, polisi nk hali inayoweza kujenga mwelekeo wa kujitenga. Rejea matatizo yakujitenga kwa Biafra Nigeria miaka ya nyuma.

4. Nchi zenye majimbo mf Msumbiji hazina hakikisho la maendeleo endelevu kuzidi ambazo hazina utaratibu huo ie Tanzania

5. Mfumo huo utakuwa na gharama kubwa kuuanzisha

Kimsingi hadi sasa mfumo uliopo hauna shida changamoto kubwa ni kuweka mifumo mizuri ya udhibiti matumizi na mapato ya serikali kwa kuyagawa kwa haki ili kila eneo la serikali liweze kunufaika. Na hususani kuimarisha mfumo wa Halmashauri uweze kukabiliana na changamoto za kiuchumi kwa kila eneo. Iwapo kuna changamoto za mgawanyo sawia basi tupitie upya sera na sheria zetu ndani ya mfumo uliopo tuboreshe.

6. Hata hivyo, Kwa maoni yangu badala ya utawala wa majimbo ni afadhali kuweka kanda za kiuzalishaji ili kuchochea uchumi wa kimaeneo kulingana na mazingira ya kiuchumi na uzalishaji kwa kila eneo.
Okey okey jimboni kwa January makamba hakuna hata lami ya kwenda kwenye choo cha ded sababu ni uwepo wa serikali ya majimbo amma nn twende kwa hoja?
Wakatoriki wana majimbo ya kiutawala ni masikini na wana migawanyiko wale?
South Africa wana majimbo ni masikini?
Okey okey jibu hoja acha ujinga wako kama jiwe
 
Hata kinachofanyika sasa ni aina ya majimbo kwanamna tofauti ila ili tunaita Jimbo kuu la ikulu kwasababu Ikulu ndio jimbo lenyewe alafu yenyewe ndio inaamua wapi pakupeleka nini.Sasa kuna ubaya gani tukiwa na majimbo mengi nchi nzima yakuhudumia maeneo yao.Ukishakua na kanda zakuzalisha na kutumia kwamatumizi sahihi nazile ambazo hazizalishi zikichangiwa kwauwiano sawa kuna ubaya gani hapo.Au unataka mambo yakila anayekaa jumba jeupe ndiye aamue atakavyo?
 
Kwa yoyote anaeifahamu hii sera vizuri hawez ipinga. Ikumbukwe majimbo sika mkoa. N zaid ya mikoa kadhaa na mikoa yote ya tanzania inautajiri haswa. Mtoa post inawezekana nawe n mwoga na hujui sera ya majimbo ikoje. Hebu kaitafute then uje utoe maelezo ya kina
 
Yaani wewe kwa akili yako unajiamini kabisa kuwa nchi haijaendelea, kama WB na IMF wameiweka tanzania kufika uchumi wa kati wewe nani useme haijapata maendeleo.

Uthibitisho wa ubovu wa sera yenu ya MAJIMBO mtauona kuanzia tarehe 28/octoba ndiyo utawajua watanzania kuwa ni wapenda utaifa na uzalendo. kufikia tarehe 30 octoba, Lissu atakuwa amekimbia nchi kwa aibu, lakini kwa kuwa anahitajika kujibu hoja pale mtaa wa bibi titi atashuhudia aibu yake akiwa hapahapa.
Mkuu sidhan ka issue ya majimbo n mbaya. Ubaya n kuwa watu hawajaifuatilia na wameanza kuingiziwa propaganda. Mbona nchi nying zina utawala wa majimbo na maisha yanaenda kama kawaida?
 
Salamu kwako Tundu Antiphas Lissu, Shalom,

Leo napenda kukwambia rasmi kuwa , Kura yangu iko kwako! Na hii ndo sababu yangu kuu ya kukupa kura!

Katika maisha yangu nimekuwa nikifanya utafiti sana juu ya dhana ya umasikini wa watanzania na Tanzania kwa ujumla, Moja ya sababu ambayo niligundua kwenye utafiti wangu ni kuwa Tanzania tuna mfumo mbovu sana wa utawala ambao vyovyote vile hatuwezi kuendelea kwa mfumo huu!

Mfumo huu ninaousema ni mfumo kuwa fedha zote za watanzania zinakusanywa na kuwekwa chini ya mtu mmoja( raisi ambayo yeye ndo anayeamua kuwa hizo fedha zigawanywe kivipi)

Madhara ya mfumo huu ni kuwa umeondoa uwajibikaji kwa wananchi na viongozi, umeondoa ubunifu kwa wananchi na viongozi na mwisho umepelekea tabia ya ombaomba na unafiki kwa wananchi na viongozi

Mfumo huu pia umechochea ufisadi wa kiwango kikubwa sana kwa wananchi na viongozi na kama Kuna mtu anabisha Leo hii aniambie maisha ya ukwasi wanayoishi maraisi wastaafu yametokana na nini???

Hapa Tanzania hakuna raisi mstaafu mwenye maisha ya utajiri wa kuwaida. Wengi wana utajiri mkubwa wa real estate, kilimo kikubwa na hata pia makampuni makubwa ya uzalishaji. Na kibaya ni kuwa vyote hivi huwa wanavipata wakiwa maraisi. Sababu ya haya yote ni kuwa tumekuwa na mfumo wa kuziweka fedha zote za nchi chini ya mtu mmoja.

Leo hii raisi ni kama Mungu hapa Tanzania. Kila aendapo watu ni kulia shida, awafanyie hiki na awaletee hiki, haya yote ni kwa sababu ya mfumo mbovu tulionao ambao umeondoa uwajibikaji na ubunifu kwa watanzania na viongozi wetu

Kwa nini Mfumo wa Majimbo ndo suluhisho wa haya yote?
1. Mfumo wa majimbo utafanya hela zote zinazokusanywa kwenye sehemu husika zitumike kwa matakwa ya wananchi wa sehemu husika mf. Kujenga barabara , hospitali, shule bora na huduma bora za Maji na umeme!! Hili litafanya wananchi wasiwe wajinga kwa viongozi wao na kamwe was iwe ombaomba na watu wa kujipendekeza kwa viongozi wao.

2. Mfumo wa majimbo utachochea ubunifu kwa wananchi kufanya shughuli mbalimbali bora za uzalishaji ili majimbo yao yakusanye fedha za kutosha kwa ajili ya maendeleo yao.

Kama jimbo husika linategemea kilimo basi wananchi wa hilo jimbo watafanya kilimo bora na watakifanya cha biashara ili wapate mapato mazuri ya kuendeleza jimbo lao kimiundombinu na Pia kimaendeleo. Hakuna sehemu watu watalala au kuwa wazembe na watakuwa wakali kwa viongozi wao kuwahamasisha wawe agressive kwenye kubuni miradi bora ya maendeleo kwa maendeleo yao.

Mfumo huu utatengeneza wananchi wanaojiamini na Kuwajibika kweli katika kutunza rasilimali zao ili ziwasaidie wao na uzao wao. Wananchi hawatakuwa wazembe na watawawajibisha kweli viongozi wasio wabunifu kwenye kutengeneza vyanzo vya mapato kwa sababu watakuwa wanajua bila vyanzo vya mapato bora na vya uhakika kwenye maeneo yao basi watakuwa nyuma kimaendeleo na hawataweza kunsurvive.

Mfumo wa majimbo utafanya kama sehemu Kuna mbuga za wanyama basi wananchi wa maeneo husika wazitunze rasilimali kweli kwa sababu watajua kweli bila mbuga hizo utalii utakufa na hawatapata mapato ya kulipa mishahara wafanyakazi wao, kujenga barabara na mitaa bora, kuhudumia Bima za afya na madawa hospitali. Kwa iyo Kama jimbo litategemea utalii basi watautunza na kuuthamini kweli utalii.

Kama jimbo linategemea viwanda au biashara basi jimbo hilo litatunga Sera bora ili kuhamasisha uwekezaji mkubwa wa viwanda na biashara kwa sababu wananchi wa sehemu husika watajua bila hivyo basi hawawezi pata mapato ya kununulia dawa, kupata Maji safi na salama na kujenga barabara nzuri!

Kama jimbo husika linategemea kilimo na migodi basi wananchi wa viongozi wa maeneo husika wataumiza kichwa kuweka Sera bora katika hayo maeneo ili kuhakikisha zinawapatia mapato makubwa ya kufanya miradi ya maendeleo. Watu watajiona kweli kuwa wao ni sehemu sahihi ya maendeleo husika.

Imefika wakati watanzania lazima tuseme kuwa mfumo wa utawala wa Chama cha mapinduzi, umechochea sana ufisadi, umasikini, kujipendekeza, uzembe, ubabaishaji na kutowajibika kweli kwa Watanzania!!!

Mfumo huu wa sasa umefanya watanzania tudharauliwe na viongozi na kuendeshwa Kama watoto wadogo kuwa tusipowachagua watu wao basi tusahau maendeleo kwa sababu wao ndo wanaamua hela zetu wazigawe vipi!! Hii sio sawa kabisa

Mfumo huu wa sasa umesababisha watu kuwa ombaomba na watumwa kwenye nchi yao kuwa kila wakimuona Raisi basi wamnyenyekee kama Mungu n kumuomba hiki na kile. Kama Raisi tunaomba Maji, barabara, umeme na shule bora

Kwa maendeleo ya kweli ni lazima Watanzania tuamue kwenye uchaguzi huu kumchagua Tundu Antiphas Lissu ili atubadirishie mfumo.

Hamasisha watu wengi zaidi kumchagua Lissu na Chadema kwa maendeleo ya kweli ya Tanzania na Watanzania!

Sambaza kwa watu wengi zaidi waelimike pia!!

Asanteni!
Lord denning.
Nimeona u miongon mwa mnafahamu sera ya majimbo. Keep it mkuu si ka wale wasemai italeta ukabila na umasikin.
 
Tatizo kubwa siasa inaturudisha nyuma kwa kutoelewa nini maana yake.! Kabla ya kukataa majimbo tafakari na kuelewa nini maana yake.
Huduma ya kimaendeleo inakuwa karibu sana na wananchi wa eneo husika na kuwajibika kwa waliowachagua wenyewe.
Hii ya kumfanya mtu mmoja kumiliki kila kitu kugawa hela anavyotaaka haitujengi ukweli upo.
 
Hoja yako hasa ni nini? UN inagharamia sawa nakubali so nachotaka kukuelewesha ni dhumuni la kuundwa AU mojawapo ni kuzilinda nchi wanachama zinapokumbwa na mzozo wa kugawa nchi vipande viwili
AU ni ka mbwa wa mapambo
 
Ulinganisho wa ukubwa sio issue, Logic inabakia pale pale kuwa, nchi inagawanywa katika kanda zenye mifumo ya kujitawala ndani kwa ndani ili kurahisha maendeleo ya watu badala ya kuwa na mtawala mmoja (Rais) mwenye kuamua hadi choo cha kijiji kijengwe wapi na lini.
Oh asilimia kubwa ya watu wanaitikadi za chama na hawajawahi fuatilia issue ya majimbo kwahiyo wakiambiwa chochote wanaitika yafaa wafundishwe issue ya majimbo ipoje maana unaweza poteza energy yako kutoa fact mtu hata hajui chochote. Mkuu hao vilaza nimekuachia ujaribu wafundisha
 
Kama hujui mfumo wa sasa ni mbaya kiasi gani nenda vijijini. Utashangaa miaka 59 tumefanya nini! Kuna umaskini wa ajabu na badala ya kwenda mbele tunarudi nyuma! Mungu tusaidie!
 
Huo utaifa upo? Katika kipindi hiki cha Jiwe kuna utengano mkubwa sana miongoni mwa watanzania! Kwake yeye ukichagua upinzani basi hilo jimbo halitapata maendeleo kamwe! Ni mfumo wa majimbo pekee utakaoondoa aina hii ya usultani!
Wenye uelewa na masuala ya Tanzania huwezi ukawauzia sera ya majimbo halafu wakaendelea kukusikiliza.
 
Maana yake halisi ni kuwa watu wenyewe kwenye maeneo yao, yawe mikoa au wilaya, ndio wawe wanachagua au kuwateua viongozi wao, kama wakuu wa mikoa, wilaya na halmashauri.

Pia maeneo hayo, pamoja na Bunge, viongezewe madaraka ya kuamua badala ya Rais pekee.
Angalau wewe umejaribu kuongea kwa lugha ya ushawishi.
 
Sizungumzi kuhusu kuwakilisha hapa.

Ninazungumza kuhusu MAMLAKA YA SERIKALI ZA MITAA kuwaletea wananchi wake maendeleo bila kusubiri huruma za magufuli.

Kila kitu Rais Rais Rais Rais. Mtu mmoja anakuwa MUNGU wa nchi nzima, uliona wapii?
Unaposikia Rais Rais uelewe kuwa hao wanaosema hivyo wanayo majukumu yao pia.

Wanaopigiwa kura wanazo kazi za kufanya,wanalo jukumu la kuwa wabunifu.

Kila mtu akitimiza wajibu wake hii nchi itapaa kiuchumi.
 
Hii si mbaya kama watu wanavyoifikiria, tena itasaidia maeneo mengine kukua sio hela zote zinazopatikana zinapelekwa chato, kuna maeneo ambayo yanachangia kuingiza hela nyingi sana kwenye uchumi ila yamebaki kua mashamba hayaendelezwi, hela yanayoleta zote zinaingia kwenye kununua ndege kwa cash au kujenga uwanja wa ndege chato.
 
Geita ilipo chato unajua kuna migodi ya dhahabu mikubwa inayoingizia nchi Mabilioni ya pesa za kigeni ? Au unadhani chato ni singida wanakotegemea mauzo ya alizeti
 
Back
Top Bottom