Kwanza niwapashe nyinyi wafuasi wa Lissu kuwa mnaposhabikia mambo anayosema Lissu vile vile mtumie akili ku analyse mambo badala ya kutukana na kumuona Lissu kama ndiye Mungu.Salamu kwako Tundu Antiphas Lissu, Shalom,
Leo napenda kukwambia rasmi kuwa , Kura yangu iko kwako! Na hii ndo sababu yangu kuu ya kukupa kura!
Katika maisha yangu nimekuwa nikifanya utafiti sana juu ya dhana ya umasikini wa watanzania na Tanzania kwa ujumla, Moja ya sababu ambayo niligundua kwenye utafiti wangu ni kuwa Tanzania tuna mfumo mbovu sana wa utawala ambao vyovyote vile hatuwezi kuendelea kwa mfumo huu!
Mfumo huu ninaousema ni mfumo kuwa fedha zote za watanzania zinakusanywa na kuwekwa chini ya mtu mmoja( raisi ambayo yeye ndo anayeamua kuwa hizo fedha zigawanywe kivipi)
Madhara ya mfumo huu ni kuwa umeondoa uwajibikaji kwa wananchi na viongozi, umeondoa ubunifu kwa wananchi na viongozi na mwisho umepelekea tabia ya ombaomba na unafiki kwa wananchi na viongozi
Mfumo huu pia umechochea ufisadi wa kiwango kikubwa sana kwa wananchi na viongozi na kama Kuna mtu anabisha Leo hii aniambie maisha ya ukwasi wanayoishi maraisi wastaafu yametokana na nini???
Hapa Tanzania hakuna raisi mstaafu mwenye maisha ya utajiri wa kuwaida. Wengi wana utajiri mkubwa wa real estate, kilimo kikubwa na hata pia makampuni makubwa ya uzalishaji. Na kibaya ni kuwa vyote hivi huwa wanavipata wakiwa maraisi. Sababu ya haya yote ni kuwa tumekuwa na mfumo wa kuziweka fedha zote za nchi chini ya mtu mmoja.
Leo hii raisi ni kama Mungu hapa Tanzania. Kila aendapo watu ni kulia shida, awafanyie hiki na awaletee hiki, haya yote ni kwa sababu ya mfumo mbovu tulionao ambao umeondoa uwajibikaji na ubunifu kwa watanzania na viongozi wetu
Kwa nini Mfumo wa Majimbo ndo suluhisho wa haya yote?
1. Mfumo wa majimbo utafanya hela zote zinazokusanywa kwenye sehemu husika zitumike kwa matakwa ya wananchi wa sehemu husika mf. Kujenga barabara , hospitali, shule bora na huduma bora za Maji na umeme!! Hili litafanya wananchi wasiwe wajinga kwa viongozi wao na kamwe was iwe ombaomba na watu wa kujipendekeza kwa viongozi wao.
2. Mfumo wa majimbo utachochea ubunifu kwa wananchi kufanya shughuli mbalimbali bora za uzalishaji ili majimbo yao yakusanye fedha za kutosha kwa ajili ya maendeleo yao.
Kama jimbo husika linategemea kilimo basi wananchi wa hilo jimbo watafanya kilimo bora na watakifanya cha biashara ili wapate mapato mazuri ya kuendeleza jimbo lao kimiundombinu na Pia kimaendeleo. Hakuna sehemu watu watalala au kuwa wazembe na watakuwa wakali kwa viongozi wao kuwahamasisha wawe agressive kwenye kubuni miradi bora ya maendeleo kwa maendeleo yao.
Mfumo huu utatengeneza wananchi wanaojiamini na Kuwajibika kweli katika kutunza rasilimali zao ili ziwasaidie wao na uzao wao. Wananchi hawatakuwa wazembe na watawawajibisha kweli viongozi wasio wabunifu kwenye kutengeneza vyanzo vya mapato kwa sababu watakuwa wanajua bila vyanzo vya mapato bora na vya uhakika kwenye maeneo yao basi watakuwa nyuma kimaendeleo na hawataweza kunsurvive.
Mfumo wa majimbo utafanya kama sehemu Kuna mbuga za wanyama basi wananchi wa maeneo husika wazitunze rasilimali kweli kwa sababu watajua kweli bila mbuga hizo utalii utakufa na hawatapata mapato ya kulipa mishahara wafanyakazi wao, kujenga barabara na mitaa bora, kuhudumia Bima za afya na madawa hospitali. Kwa iyo Kama jimbo litategemea utalii basi watautunza na kuuthamini kweli utalii.
Kama jimbo linategemea viwanda au biashara basi jimbo hilo litatunga Sera bora ili kuhamasisha uwekezaji mkubwa wa viwanda na biashara kwa sababu wananchi wa sehemu husika watajua bila hivyo basi hawawezi pata mapato ya kununulia dawa, kupata Maji safi na salama na kujenga barabara nzuri!
Kama jimbo husika linategemea kilimo na migodi basi wananchi wa viongozi wa maeneo husika wataumiza kichwa kuweka Sera bora katika hayo maeneo ili kuhakikisha zinawapatia mapato makubwa ya kufanya miradi ya maendeleo. Watu watajiona kweli kuwa wao ni sehemu sahihi ya maendeleo husika.
Imefika wakati watanzania lazima tuseme kuwa mfumo wa utawala wa Chama cha mapinduzi, umechochea sana ufisadi, umasikini, kujipendekeza, uzembe, ubabaishaji na kutowajibika kweli kwa Watanzania!!!
Mfumo huu wa sasa umefanya watanzania tudharauliwe na viongozi na kuendeshwa Kama watoto wadogo kuwa tusipowachagua watu wao basi tusahau maendeleo kwa sababu wao ndo wanaamua hela zetu wazigawe vipi!! Hii sio sawa kabisa
Mfumo huu wa sasa umesababisha watu kuwa ombaomba na watumwa kwenye nchi yao kuwa kila wakimuona Raisi basi wamnyenyekee kama Mungu n kumuomba hiki na kile. Kama Raisi tunaomba Maji, barabara, umeme na shule bora
Kwa maendeleo ya kweli ni lazima Watanzania tuamue kwenye uchaguzi huu kumchagua Tundu Antiphas Lissu ili atubadirishie mfumo.
Hamasisha watu wengi zaidi kumchagua Lissu na Chadema kwa maendeleo ya kweli ya Tanzania na Watanzania!
Sambaza kwa watu wengi zaidi waelimike pia!!
Asanteni!
Lord denning.
Sera ya majimbo kama ukitokea muujiza Lissu ashinde (sababu haiwezekani kushinda) basi lazima nchi isambaratike.
Ingawa mnatolea mifano Marekani na Ujerumani na Kenya kama mifano ya majimbo ambayo imedumu lakini nchi hizo mbili za wazungu zina uchumi mzuri na wanacnhi wake wameelimika na wanajua kuchambua mambo hivyo hawaburuzwi na wanasiasa. Kwa Kenya bado kipindi ni kifupi kuweza kuwajaji.
Mifumo ya majimbo kwa hao wenzetu kwanza ilijadiliwa ikakubalika na kuingizwa kwenye katiba hivyo chama chochote kikiingia madarakani kinafuata mfumo huo. Hapa kwetu ni sera ya CHADEMA sio muafaka wa nchi, na kwa kuwa hakuna chama kitakachodumu daima madarakani, baada ya muda CHADEMA wakiondolewa madarakani chama kingine kinaweza kubadilisha huo mfumo kwa sababu hauna ridhaa ya nchi hivyo kama nchi tutakuwa tunayumba kila chama kipya kinapoingia madarakani.
Pili Mtambue huo mfumo umewahi kusambaratisha nchi nyingi vilevile nitazitaja:
Yugoslavia: Hii ilikuwa majimbo (federal system) wakati wa utawala wa Rais Tito majimbo (republics) sita yaliitwa Serbia, Croatia, Slovenia, Mecedonia, Montenegro, Bosnia and Herzegovina; na pia mikoa ya Kosovo na Vojvodina iliyokuwa ndani ya Serbia. Baada tu ya kifo cha huyo rais licha ya kuwa aliweka utaratibu wa urais wa mzunguko kwa kila jimbo kupokezana urais wa Yugoslavia hatimaye zilisambaratika tena kwa kupigana vita vikali.
Soviet Union: Hii wengi wanaifahamu kama Urusi. Ilikuwa na Jamhuri 15. Baada ya mageuzi ya kuleta uhuru wa kusema aliofanya Gorbachev hatimaye zilisambaratika. Russia Federataion ambayo ndiyo Urusi ya sasa nayo nusura isambaratike.baadae kama insingetumika nguvu kubwa kuzima muelekeo wa kujitenga uliokuwa umeanza kushika kasi. Ilianza Chechnya ikajitenga, baadae ikaisaidia Inguetshia nayo ikiajitangazia uhuru ndipo Putin akatumia nguvu kuizuia Inguetshia na pia kubadili uamuzi wa kuiruhusu Chechnya ijitenge lakini kwa kumwaga damu.
Ethiopia: Hii nchi inatumia mfumo wa majimbo (federal system). Baada ya vita vya kumng;oa Mengistu vilivyoongozwa na Tigray, walianzisha mfumo huo wa majimbo, Baada ya serikali kuanza kuongozwa na huyu Waziri Mkuu wa sasa Mr Abiy Ahmed, ambaye ni kutoka kabila la Oromo, watigray wengi ambao walikuwa wamedominate serikali walipoteza ushawishi wao. Sasa wameanza chokochoko za kuchallenge mamlaka ya Addis ababa. Hivi karibuni waliamua kuitisha uchaguzi wa jimbo lao kinyume cha katazo la serikali ya Shirikisho kwa sababu uchaguzi ni mamlaka ya serikali kuu sio ya jimbo. Kutokana na chokochoko hiyo ya uasi Waziri Mkuu alikuwa anashinikizwa apeleke jeshi ili kudhibiti Tigray lakini yeye bado anasita. Hivyo kuna wasiwasi kuwa Ethiopia nayo inaenda kusambaratika kutokana na yanayoendelea sasa nchini humo. Jimbo la Oromo nalo haliko nyuma katika vuguvugu hilo. Kwa kifupi majimbo ya Ethiopia yana manung;uniko mengi na kuiona kama hawanufaiki vile walipaswa kunufaika.
Tatu, Hoja za kiuchumi: kuna watu humu eti wanatolea mfano kuwa Dar es salaam wana bandari hivyo watachukua mapato ya bandari, majimbo ya mipakani yatachukua mapato ya mpaka hivyo hakuna jimbo litakalokosa mapato. Kitu ambacho hamuelewi ni kuwa katika mfumo wa shirikisho mapato ya ushuru wa forodha (customs) yaani bandari na mipakani yanakusanywa na serikali kuu sio serikali za majimbo. Hivyo baadhi ya majimbo hayatakuwa na rasilimali za kutosha.
Nne, ongezeko la gharama za serikali: Mfumo wa majimbo ukiruhusiwa maana yake kwa Tanzania kutakuwa na serikali nne hivyo gharama za kuziendesha zitakuwa kubwa sana na italazimika kuwa na kodi kubwa ili kupata fedha za kuendesha serkali hizo. Kwanza serikali ya mtaa (Jiji/Manispaa/ Wilaya) na baraza lake la madiwani, pili serikali ya jimbo na bunge lake, tatu serikali kuu ya Tanganyika na bunge lake, nne Serikali ya Muungano wa Tanganyika na Zanzubar na bunge lake. Sijui kama mashabiki wa LIssu wanayaoa haya na athari yake kwao. Huu utakuwa mzigo mzito sana kubebwa na watanzania na wengi humu watajuta kama mfumo huo ukianzishwa.
Tano, Ubaguzi na kujitenga zaidi: Baadhi ya Halmashauri ndani ya majimbo ambazo ni tajiri zinaweza zikadaai zipate mgao mkubwa au wote wa rasilimali zinazotoka ndani ya maeneo yao, mfano Geita wanaweza kudai wanufaike wao zaidi na dhahabu yao kuliko Jimbo zima la kanda ya ziwa kunufaika na mapato ya dhahabu inayotoka Geita. Jambo hilo litapelekea kusambaratisha jimbo na nchi. Aidha hata ajira zinaweza kutolewa kiubaguzi kwa kuajiri watu wanaotoka katika majimbo husika tu. Pia Majimbo yanaweza kutunga sheria za kibaguzi mfano kupiga marufuku pombe na baa; mapenzi ya watu waliokubaliana kwa hiyari nk.
Mwalimu wa idielogy wa Mao Tsetung aliwahi kusema kuwa ninanukuu: “A country is not like a machine which you can take it apart and then assemble it again”