PSEUDOPODIA
JF-Expert Member
- Aug 9, 2020
- 392
- 798
Mimi mkazi wa Songea Kitai, nilikuwa naumia sana kuona katika eneo letu ndipo yanapatikana makaa ya mawe yanayolisha karibu viwanda vyote nchini, na mengine yanasafirishwa kwenda Rwanda, Uganda, Burundi na Kenya na kuingizia nchi mamilioni ya pesa. Chakusikitisha barabara katika eneo letu ni Mungu tu ndo anajua, Yaani inafika kipindi cha mvua magari yanashindwa hata kupita kwenda kupakia makaa, barabara ni mbovu, eti suluhisho wameona matipa ndo yaende kupakia huko migodini yalete mjini ndo yapakiwe kwenye magari na kusafirishwa.
Kinachoniuma ni kuwa pamoja na mamilion tunayoingiza, pia sisi ni wakulima wakubwa, tuna lisha nchi na kuingizia mamilioni, isitoshe kuna uvuvi katika ziwa Nyasa vyote hivi vinaingiza mamilioni, lakini tunashindwa kujengewa barabara , Maji safi ya kunywa kwetu ni ndoto, hospital paka uende mjini, umeme tunauona tukienda mjini.
Naamini hii Sera ya majimbo kwamba kile kinachopatikana sehemu kilete maendeleo kwanza eneo lile husika ingekuwa imeanza siku nyingi basi wakazi wa Kitai tungekuwa kama calfonia,.
Kuna maeneo hapa Tanzania yatakuwa kama ulaya, ndio maana nchi kama Afrika kusini miji yake karibu yote imeendelea. Fikiri jimbo la Iringa lingekuwaje nafkiri kama Durban, Mtwara wana gesi, wana korosho, wana uvuvi wangekuwa kama Chicago. Moshi, Arusha, Mwanza, Mbeya sijui yatakuwaje.
Kwa kifupi hii Sera kwangu Mimi ndio Sera rahisi zaidi ya kuleta maendeleo kwa kurudisha mamlaka ya matumizi ya pesa kwa wananchi wa eneo husika. Wao ndo wanaamua tufanye nini na hii pesa yetu. Nafkiri hii ingekwepo chato wasinge amua kujenga uwanja wa ndege, Bali wangetumia zile pesa kwa jambo lenye manufaa zaidi ya uwanja. Pia wananchi wasingenunua ndege bali hiyo hela wangefanyia jambo lenye manufaa zaidi.
Pia Sera ya majimbo itapunguza mtu mmoja kuwa na maamuzi ya nchi nzima na kufanya aabudiwe kama mungu. Maana asingekuwepo mtu wa kusema msimchagua Fulani sileti maendeleo kwenu. Maana maendeleo yatakuwa yanaamuliwa na wananchi wenyewe na si kama ilivyo sasa amabapo pesa zote za nchi nzima zinakusanya sehemu moja alafu rais ndo anapanga afanye nini na hizo pesa. Matokeo yake ndo tunaon mtu anajiamulia tu sijui ajenge uwanja wa ndege, sijui anunue ndege, anaona pesa nyingi paka nyingine anaona bora agawe barabarani.
Pia hii Sera itapunguza ufisadi kwa kiasi kikubwa, maana wananchi watakuwa wanajua mapato na matumizi ya majimbo yao. Kama kuna ufisaidi mahali itakuwa rahisi kujulikana, tofauti na sasa ambapo CAG kasema kuna ufisadi wa Trillion 1.5 hazijulikani zilipo, ila serikali wanasema hakuna pesa iliyopotea na matokeo yake CAG akafukuzwa kazi kwa kusema ukweli. Pia tungekuwa tunajua kuwa tumenunua ndege kwa kiasi gani, tumejenga uwanja kwa kiasi gani tofauti na sasa ambapo gharama za ndege anajua mtu mmoja tu. Na gharama za uwanja anajua mtu mmoja tu Yaani yeye ndo mnunuzi, ndo dalali, ndo mtoa pesa, ndo mwandika mkataba, ndo msaini mkataba, ndo mwanasheria, ndo mhasibu, ndo daktari ndo kila kitu.
Faida za majimbo ni nyingi sana siwezi kuziandika zote, lakini nchi zote zenye mfumo wa majimbo karibu zote zimepiga hatua katika sekta ya maendeleo.
#LissuTumekuaminiTuvushe#