Sera ya matajiri wakubwa nchini kuwa Raia wenye asili fulani na kazi fulani iwe yenye malipo makubwa zibadilike!

Inasikitisha sana, hii tabia ya Waafrika kujiliza ifike mwisho sasa.

Mbaya tunangangania tupendwe na jamii nyingine, wapi umeona raia wa Japan, America, India, Germany, Uruguay n.k wakililia wapendwe iwe katika siasa zao, imani zao za kidini, kibiashara n.k Wao hufanya yao mazuri na kizuri chajiuza wakati kibaya chajitembeza kwa kulialia.
CHEMA CHAJIUZA KIBAYA CHAJITEMBEZA. kitu kizuri hakihitaji lebo wala nembo
Wamatumbi tuache kulialia fursa zipo kibao na tubadili mifumo yetu ya kimaisha ili tuondokane na minyororo ya umasikini wa kujitakia. Tuache kupoteza muda ktk shughuli za harusi, misiba, kujenga majumba ya mabilioni kwa ajili ya kuishi wakati ndiyo mtaji wenyewe, kuendesha magari kwa ajili ya starehe badala ya kutumika kama nyenzo ya kufuatilia biasha zako, kushinda ktk majumba ya imani za kidini za kuja n.k mambo ambayo yanatugharimu ktk jamii pakubwa kiiuchumi.

Wenzetu hata baiskeli huwa inatumika ktk shughuli za kiuchumi. Mambo ya kibiashara yakikua hununua pikipiki ya bei nafuu kuzidi kutumika kupanua biashara. Baada ya hapo biashara hiyo ikizidi kukua , hununua gari la bei ndogo na anaendelea kwa mtindo huo hadi kufikia ngazi ya gari la gharama kubwa kufuatana na mabilioni ya faida ktk biashara yake. Sisi wamatumbi tunaruka hatua hizo na kujitumbikiza katika matatizo makubwa ya kifedha na kiuchumi kwa kujiingiza ktk madaraja ambayo bado hatujafikia .

Kwa kifupi ukitaka kujua kama baiskeli au gari inakufaa kwa shughuli zake halali zinazokuingizia kipato basi fanya hesabu je nikipewa mkopo wa baiskeli au pikipiki kwa ajili ya usafiri kwenda kwenye shughuli zako utaweza kulipia mkopo huo kila mwezi, pia kipato chako halali kitaweza kununua chakula, mavazi, karo za shule kama una familia, pango / kodi la/ ya nyumba ? Kama ni hapana achana na hiyo baiskeli au gari tumia usafiri wa umma ndivyo wenzetu wanavyofanya ktk nidhamu ya fedha na kujijengea mtaji / capital.
 
Nimetazama video yoote........

Pure sanity, pure jiniazi.

Ng'ombe haharibugi msitu kinyume chake huubalansi ukanawiri zaidi.

Ngombe huzuia nchi kugeuka jangwa!! na msihisi natania au ni sarcasm hapana! bali huo ndio ukweli ulivyo
 
Walioporwa mali na biashara zao kutaifishwa wakati wa Azimio la Arusha wengi walikuwa ni WaAsia. Mpaka leo hawajalipwa fidia au kurudishiwa mali zao. Sasa hiyo dola ilikuwa wapi?
Ungejua jinsi walivyo "react" na ku syphone forex nyingi including viwanda na biashara kwenda nchi jirani na fedha kupitishwa kiharamia kwenda Ulaya nk. usingetamka hayo. Naweza kukuhakikishia tumeshalipa kutaifishwa kwa majumba yao kwa kiwango cha 200% and above. Tatizo letu mambo kama haya hayafanyiwi utafiti, mtu angepata PhD ya Uchumi kwa kazi hiyo. Kwani hujasikia India wanauza Tanzanite nyingi kuliko TZ? Kama huyajui usiyazungumzie sana, lakini kama wewe ni mhusika unajifanya mjanja jua siku ipo inakuja.
 
Mkuu kila mwamba ngoma kamba huvutia kwake.
Serikali kwa miongo mbali mbali imeshindwa na kwa kiwango kikubwa kuwapa wanyonge maendeleo na mafanikio makubwa.
Kwanza hakuna mnyonge ni mfumo tu.
Pili hao wapuuzi wanaotwambia wanyonge ni madalali kuwanyonya masikini,kila siku ni kama fundi Michael.
Serikali zetu wamekopa kwa mabenki rafiki kutupa maendeleo, maskani yeye anatotoa watoto tu wengi,unategemea maskini atatatoboa?
Mwalimu alipokuja na UMATI hakuwa mpumbavu.
 
Inasikitisha sana, hii tabia ya Waafrika kujiliza ifike mwisho sasa.
Kumbe mzee Mengi alikuwa ana Lia Lia!!?sera huyo ipo hapa NCHINI!

The state ndio wakaamua nani awe tajiri nani asiwe regardless na working capacity ya mtu!!
Elewa HAYO niyasemayo

Ina MAANA wats wote ni wavivu hawana discipline ya fedha Sio!!?

MENGI hakukurupuka KWENYE kitabu chake!!cha I can, I must I will!!
 
Point tupu umetema

Ova
 
Kuna ukweli ua uwakute kidimbwi
 
Rostam aziz babu zake walianza biashara tabora zaidi ya miaka 170 iliyopita,gsm baba alihama tanga akahamia songea kufuata fursa za kilimo..mengi alitapeli NBC akapata mtaji...utajiri hauji ghafla,labda wa kipaji Kama mpira,kikapu,movie na tech Facebook,weusi baba akifa tunagawana tunaongeza wake,vilabuni watatukoma..waasia anatafutwa mtu mwenye uwezo anasimamia Mali iendelee kuzaa,serikali Haina sera ya kutajirisha mtu
 
Huu ukiritimba wa kupenda ngozi nyeupe tunao sana tukiuacha tutapiga hatua kubwa.
 
Huu ukiritimba wa kupenda ngozi nyeupe tunao sana tukiuacha tutapiga hatua kubwa.
Huyo naniliu uliyemtaja hapo sio tajiri huyo ni mkwepa kodi mkubwa na kivuli cha jamaa mmoja hivi yupo mkoa wa jirani ya jiji la maraha.

Fedha zake zinatokana na kukwepa kodi. akibanwa hutamsikia vizuri hutamsikia tena.
 
Nimesoma hii story mkuu hakuna mtanzania hapo. Ni sawa kujisema eti fifty ama Obama Ni mwafrika just rangu Ila mind sio.
Mtu amezaliwa China na marekani mpaka saivi Wana 30+ unaita watanzania na huku hata uraia wa tz hawana.
Hakuna anayekula ugali akafanya haya yote
 
Label destroy us. Let us treat each other as human first. Watu wenye mawazo ya kibaguzo wengi wana asili ya uchungaji ambao kimsingi hata wao ni wahamiaji. Na huenda kwasasa wako dar, lkn kabla ya kuja dar hakuwahi kuishi na mchanganyiko wa makabila mengine zaidi ya ngombe, mbuzi au kondoo na watu wa kabila lake
 
Kumbe Kumbe Mengi alipoandika serikali ilipendelea wageni kwenye fursa za uwekezaji alikuwa mchungajibwa mbuzi na ng'ombe!!?akili kumkichwa
 
Hebu tupe habari zaidi kuhusu kutapeli NBC. mwaka gani ilitokea? kiasi gani aliitapeli NBC; Ilikuwa mkopo hakurudisha au ilikuwa je mkuu! Bank zinauwezo wa kutumia sheria zilizopo na kukamata mali za aliyeshindwa kurudisha mkopo nk na kupiga mnada, ni kwanini NBC ilikubali kutapelika kirahisi wakati inafahamika alikuwa na mali nyingi tuu?
 
Niliona sehemu mengi ni cpa za mwanzo tz
 
Ccm ni mavii ...tena kwa sasa ni zaidi baada ya sa100 kuchukua nchi hali ni mbaya sasa hivi hadi jeshi linakwenda kuwekwa chini ya muarabu
 
Hivi dhana ya kuwawezesha wazani INA maana gn. Wakati wale walalamishi ndio waliokabidhiwa mashirika ya umma wakayafilisi akiwwmo tajiri mwenda zake. 95% ndio wameshika nafasi nyeti za kufanya maamuzi. Sasa sijui una maana gn mnapolilia upendeleo
 
Siku mbili mnakuja na Uzi haya ndo makabila yenye mfanikio Tanzania..Better wageni waongoze milele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…