Sera ya Ushuru Sifuri ni fursa pia ni kichocheo kwa Afrika

Sera ya Ushuru Sifuri ni fursa pia ni kichocheo kwa Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,310
Reaction score
1,265
VCG31N1246105216.jpg


Hivi karibuni, "Ushuru Sifuri wa China" imekuwa mada muhimu kwenye vyombo vya habari nchini Kenya. Watu mbalimbali, kuanzia Makamu wa Rais hadi wafanyabiashara, wanaipokea sera hiyo (itakayotekelezwa kuanzia Mei mosi, 2026) sio kwa kuikaribisha tu, bali kujipangia mikakati mipya.

Sababu si tu kwamba China inazipa nchi 53 za Afrika zenye uhusiano wa kidiplomasia nayo hadhi ya kuwa na ushuru sifuri, bali pia wakati huu ulimwengu unakabiliwa na vitendo vya kujilinda kibiashara. China inatuma ujumbe wazi: mlango wake utazidi kufunguliwa. Uhakika huu umetajwa kama bidhaa adhimu ya umma duniani.

Tofauti na nchi nyingine, ushuru sifuri wa China hauna masharti ya kisiasa. Kama alivyosema makamu wa Rais wa Kenya Kithure Kindiki, hii ni nyongeza kwa wakulima na kuzidisha faida kwa wauzaji. Na tovuti ya Capital FM ilisema sera hii inabadilisha mkakati wa Kenya kutoka "kuuza tulivyo navyo" hadi "kuongeza thamani ya tulivyo navyo".

Zaidi ya kusamehe ushuru, sera hii inasaidia Afrika kuhama kutoka kuuza malighafi hadi kuuza bidhaa zenye chapa. Kama gazeti la Business Daily lilivyosema, ushuru sifuri unapunguza gharama za kuuza nje na kufungua mlango kwa sekta kama ya nguo, vyakula na ngozi. Hivyo China inaisaidia Afrika kuinua ngazi ya viwanda vyake kwa mantiki ya soko.

Bila shaka, ushuru sifuri ni mwanzo tu. Wateja wa China watanunua bidhaa si kwa sababu ya ushuru sifuri, bali ni kutokana naubora na bei nzuri. Ushuru sifuri ni ngazi iliyojengwa na China, na sasa Afrika ni lazima ipande ngazi hii yenyewe.

Hata hivyo, sera hii imeamsha mawazo mapya kuhusu maendeleo na mkakati wa biashara barani Afrika. Katika dunia ya leo, ambapo migogoro ya kijiografia imedhoofisha kwa kiasi kikubwa matarajio ya ukuaji wa uchumi wa dunia, China kutoa "tiketi hii ya kuuza bidhaa bila ushuru" kwa Afrika ni fursa, na pia ni kichocheo.
 
Back
Top Bottom