Sera za kuwabeba "masikini" zinaua miji

Ndo nikuulize wewe unaewapondea masikini
Hujamwelewa mleta mada...

Pengine hata wewe hujui hata definition ya "masikini" ni nani..

Hebu rudia tena kumsoma jamaa, pengine utamwelewa sasa....

Ukishaelewa, tuambie sera za serikali kupunguza umaskini na masikini ni zipi...

Je, ni hivi serikali inavyofanya sasa kuruhusu mambo kufanyika hovyo hovyo pasipo kufuata utaratibu...?

Hili siyo tatizo la DSM tu bali karibu miji yote Tanzania...

Njoo ktk jiji la Mwanza au Arusha, hali ni ileile...
 
Siyo siri mkuu, bila sera za kuondoa umasikini ni kutwanga maji kwenye kinu.
Na unynge huo wa kufikiri haujifichi.
Huwezi kuwa glorify masikini bila sera za kuondoa umasikini.
Huwezi ondoa umasikini kwa kuwapa masikini a free ride on the society at large.
Open cheque ya kufanya lolote popote walipo.

DAR peke yake in watu milioni 5, na miji mingine vivyo hivyo.
Waingie watu wangapi wapange biashara barabarani ili kukidhi haja za watu masikini nchini.

Kuna tatizo hapa , hatujui masikini tunawatengeneza vipi na hatujui sera zipi kuondoa umasikini.
 
Unaelewa maana yake, ila hutaki kuipa fikra nzito.

Hiyo ni njia za kuzuia "BOMU" hata kama ni kwa muda mfupi.

Maana yake ni kwamba serikali haijui ifanye nini na hawa watu; kwa hiyo ni njia ya kupoza ili bomu lisilipuke haraka.

Si ajabu, magereza saa hizi yangekuwa na wengi wa hawa watu waliomo mitaani sasa; na siyo ajabu, hata wewe pale mtaani kwako ungekuwa ushabomolewa dirisha...; n.k.

Tatizo lililopo, wanaopoza bomu hilo kwa muda mfupi hawaonyeshi bidii ya kutafuta njia endelevu ya kuzuia bomu hili lisilipuke huko mbeleni.
 
LOoo, Jidu, huu ni mjadala mzito sana, lakini sijui utakwenda vipi huu.

Kwa mfano: angalia mlivyopishana na mkuu Napoleon hapo juu..., yeye anapiga hivi, na wewe ni kama unamsindikiza kiaina! Mawazo yenu ni mbalimbali kabisa!
 
LOoo, Jidu, huu ni mjadala mzito sana, lakini sijui utakwenda vipi huu.

Kwa mfano: angalia mlivyopishana na mkuu Napoleon hapo juu..., yeye anapiga hivi, na wewe ni kama unamsindikiza kiaina! Mawazo yenu ni mbalimbali kabisa!
Mkuu kuna mambo hayawezi kuepukika katika jamii.
Tatizo la umasikini lipo na ni lazima lipewe kipaumbele katik utatuzi wake.
 
Sasa hyo ndo point....ili tuweze jivunia miji yetu lazima serikal iwe na sera endelevu za kutokomeza umaskin..waje na mbinu tofaut tofaut...ajira tu imekua gumzo. Hao vinana wa vyuon ndo waamejazana barabaran na mitandaon na page za kuuzaa bidhaa..kujikwamua sabab mitaj yao ni midogo..unafkiri kuna mtu anapenda kaaa barabaran mkuu...heb tembea uwaone sura zao zinavyotia huruma..vijana wamejaa kkoo mwenge. Wale usidhan ni darasa la saba..wale ni graduates wa vyuo vikuu wanatafta mitaj wawekeze largely..so mim nawaangalia sana hao..wengne wanadaiwa mikopo...mkuu..hali ni mbaya unless uangalie situation ya hao vijana..mim nina magoli kama 9 hiv mitaan huko kuna vijana nmewaweka ..mi napata nao wanapata tunasaidia .huko huko masokon mabarabarani...n we make it..kama mtu anatengeza 800k a week huko huko mabandan y asifanye hvyo. Hao vijana wamepata ajira nao wanakula na family zao namim nakula pia in one way or other
 
Acha uongo chief
 
Kuahirisha matatizo hakujawahi kutatua tatizo.
Hili la kuwaruhusu machinga wakae barabarani ni bomu linalosubiri kupasuka.
 
Funga duka wape vijana bidhaa zako wauze kama machinga jioni wakuletee mauzo. Hii ndo mbinu wanatumia sasa wenzako.
 
Nchi yenye vijana karibia 70% halafu karibia wote ni machinga na bodaboda! Ujue km nchi kuna sehemu tunafeli, tunapaswa kujiuliza tumekosea wapi?

Kenya Tu! Hpo jirani yetu hta hajatuzidi Sana kiuchumi lakini mbona taratibu za mipango miji hazina changamoto km hpa kwetu?

Tuwe wakweli na tuache kutetea upuuzi kwa kisingizio cha umaskini.
 
We jamaa ni muongo Sana na propagandist uliyekubuhu !

Kuchinjana Rwanda na ubepari vinahusiana vipi?
 
Ahhh kumbe ndio maana unatetea huu uozo wa uharibifu wa miji yetu.
 
Ila jamani miji yetu imeharibika mno mno, hadi njia za kupita kwa miguu imekabwa na hawa machinga. Ni bomu baya sana kwani kuja kuwaondoa ni shughuli pevu kwa utawala ujao.
'Waacheni hawa ndio walinipa kura'
 
Yani we kwa akili yako unawadharau wachumi wetu kabisa afu unajoina mwerevu unaita wapumbavu wenzio. Mimi suggestion yangu nimeshatoa calculation ifanyike ya maisha ya mtu standard anafford matumizi gani kwa siku bei zipandishwe hadi hapo wataondoka watu taratibu wenyew maan zitawekwa sera za nje ya mjini ambazo ni nyepesi. Afu watu wanaoogopa mabomu ya machozi hawna courage hyo ya watutsi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…