Sera za kuwabeba "masikini" zinaua miji

Tangu lini ccm ikawatayari kuondoa umaskini wa watu? Hao maskini ni mtaji wa siasa wa maccm

Utoke kwenye umaskini Ili usiwachague? Haiwezi tokea
 
Hili tatizo limetengenezwa na vyama vyote vya siasa hapa nchini.

Kuna wamachinga, wapiga debe na boda boda.

Haya ni mambo ambayo vyama vyetu vya siasa vimeamua tuyabebe.
 
Acha siasa ndugu, hakuna nchi isiyokua na utaratibu. Serikali inakwepa lawama na kuchukua point kwa watu wanaoitwa 'masikini' nchi haiwezi kuendelea kwa wauza ugali dagaa stand..
Hatukatai wafanya biashara wadogo duniani kote wapo ila kuna utaratibu wa biashara... Stand ni stand, barabara ni barabara

Sent from my Android using JamiiForums mobile app
 
Vijana hawana Ajira Sera za kuwahusisha na Kilimo na Ufugaji hakuna. Rural to Urban Migration ni kubwa na haina udhibiti. Uzazi wa mpango hautiliwi maanani. Chokoraa na ombaomba kila Kona. Matumizi ya Barabara na Sidewalk hayazingatiwi. Barabara tunazijenga Kwa Billions zinaishia kuweka majiko ya Mishikaki, Chips, mahindi Choma na Mama ntilie. Watu wanakula ovyo popote. Kila Kijana akiibuka ni Bodaboda na Bajaji. Posta umekuwa kama Mbagala. Haki za Watembea Kwa Miguu Maskini wenzao zimesahaulika. Ukitaka kuona Uchafu na Side effect ya Maskini DSM Nenda kituo cha Mabasi kilichohamwa!!!
 
Hili suala jamani Serikali ilifanyie kazi.Ni miji yote nchini.Miji imeharibika.Utafutwe utararibu mwingine Hii ya kutandaza bidhaa barabani siyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…