Risasi moja tu ya jicho kutoka kwa mwamba Jackal inamhusu.
Season 2 jamaa atakuwa anatoroka nchi na private jet baada ya msako mzito kutoka kwa Zina upande mmoja na MI6 agents kadhaa kwenye ma Range meusi waliokuwa wakimfukuza barabarani na yeye kuingia kwenye parking building na kubadilisha magari na kuwapoteza.
Atafanikiwa kuingia kwenye ka airstrip cha don mmoja mwenye winery nje ya mji kwenye kashamba flani ka mizabibu. Atatoka kwenye hangar vizuri tu na ki Gulfstream G8 chake na kuclear runway vizuri tu, ila ndege ikiwa hewani na ka stewardess kakiwa kana mmiminia champagne, ghafla mlango wa rubani unafunguliwa na rubani anatoka. Rubani ni nani? Jackal mwenyewe.
Wanaongea mawili matatu halafu Jackal anampiga ile "F@#k you" kama ya kale katapeli kengine ja kijerumani na kumpiga moja ya jicho.