Kuna vyanzo vingi vya habari duniani tena ikichangiwa na hii mitandao ya kijamii inayoibuka kila siku so mtu unaweza ukaamini lolote unalolisoma au kulisikia
Movie industry inategemea sana faida (profit) kuliko kitu kingine chochote kama biashara nyingine yoyote sasa ikitokea kuna hasara (loss) sidhani kama mtu atakuwa tayari kupata hiyo harasa(loss) na soko la series biashara yake kubwa ipo kwenye idadi ya watazamaji, kituo cha tv kinachorusha hiyo series kinapata faida(profit) kubwa sana iwapo kutakuwa na watazamaji wengi( nitarudi kuelezea biashara wanafanyeje kutokana na wingi wa watazamaji) na kama show itakosa watazamaji wengi inakuwa cancelled coz ni biashara ambayo haina faida
Tukirudi kwenye suala la THE EVENTS ni series iliyopataga reception kubwa sana iliporusha Pilot yake Kwa mara ya kwanza mwaka 2010 mpaka baadhi ya wachambuzi wakasema ndio mbadala wa 24,Lost na 4400 lakini waliicritisize kwamba inamaswali mengi sana ya kijibu ambapo ilipokuwa inaendelea watazamaji wakawa wanapingua kila siku mpaka ikafikia katika ep ya 15 watazamaji walipungua kwa 48% hivyo ikawa ni biashara haina faida( profit) wakaamua kuicancel
Suala unalosema kaka
Innocizy ni kweli kwamba katika kazi kuna conflicts lakini haziwezi kiathili biashara kiasi hicho maana kuna njia nyingi ya kuzitatua bila kuathili utendaji ila upo long kwenye suala la kwamba eti ilihatarisha usalama wa nchi
USA ndiyo nchi inayoongoza kwa uhuru na democrasia ya kujielezea ni nchi pekee na chache ambazo raisi anaweza kutukanwa hadharani
Lazima pia tujue makundi ya kijamii yanayoangalia sana TV ukiangalia kwa haraka haraka wanawake na watoto ndio wanaoongoza kuangalia TV sebureni hii inamaana kwamba vipindi na show zinazopendwa sana na wao ndio sitakazo pata watazamaji wengi,sorry kama sijakosea hata hiyo The event yenyewe ilicanceliwa ili kuipa nafasi show flani hivi ya kike kike sema nimeisahau sema,
Wanaume sisi tunapenda sana show za kibabe,kisayansi na kitafiti lakini hatukai sebureni kuangalia sie ni wazee wa torrent na kupakua bure na kwa uwizi ndio maana show zinazopendwa na wanaume nyingi zinakuwa cancelled
Show kama Disparate house wives ilipata sana umaarufu sababu tu ya kupendwa na kutazamwa sana wanawake
Pia zipo show nyingi sana ambazo zimecanceliwa baada ya kuonyesha Pilot