Serikali: Ardhi ya Tanzania ni mali ya Umma siyo ya Kabila moja, Katiba imemkabidhi Rais wa JMT aisimamie

Wenzetu wanajua kutetea haki zao, hawakubali kuburuzwa na kuonewa na serikali. Watanzania wamebakia kusema wamasai wafukuzwe kama makabila mengine yalivyofukuzwa. Mawazo ya kijamaa.

Your browser is not able to display this video.
 
Tuna hasara kubwa sana kama mtu mwenye PHD anaweza toa tafsiri ya sheria namna hii.

Ndio maana law firm yake imenyanganywa kesi na benki moja maarufu kwa kufanya kesi nyingi kwa uzembe.

Hakuna mahali mtu anadai ardhi flani ni ya kabila flani na hata hivyo mbona kila mkoa umegawanyika kwa makabila??
 
Wanataka wawatoe wamasai ili waiuze kwa mabwanyenye wa kiarabu,,,,.
 
Kwanini tusiwahamishe wakojani na wangazija wa Pemba ili kulinda ecosystem ya kisiwa cha watalii??
 
Kwahiyo kwa Akili yako unaona haki za Binadamu zina mipaka ila haki za wanyama hazina mipaka na hapo umesomeshwa kwa Kodi za wananchi.
Hao wanyama hawaongezeki wew pimbi? Je kesho wakisema Kariakoo iwe hifadhi ya wanyama kwa kuwa nyati wameongezeka Sana na hawana makazi utakenua tuu meno yako?
 
Uonevu hauozi. Ni akiba.
 
Huyu naye ni Vuvuzela. Hakuna mtu anayeitetea ardhi kwa sababu ni mmaasai. Watu wanatetea ardhi wanayoishi.
Hata leo ukienda Iramba ukataka kuchukua ardhi, utakaowakuta wengi ni Wanyiramba au ukienda kwao Songea, waathirika wengi watakuwa nduhu zake Wangoni. Na wakilia, haimaanishi wanajiona ardhi ni ya kabila lao. Wanamaanisha ardhi yao kama sehemu ya Watanzania. Aache uvuvuzela bana.
 
Nchini DeMark ukitaka kuuza shmba inatangazwa na serikali. Huwezi kurthisha familia kama hana mafunzo angalau ya diploma ya kilimo. Naye utamuuzia na atalipiwa na serikali ni mkopo ndio aendeleze eneo kwa kilimo cha mazao au ufugaji. Je mwenye ardhi NI NANI HAPA. Usidanganywe ardhi mwishonicni mali ya serikali. KAMA YA KWAKO VIPI UNALIPIA KODI. Wanavyopima vijijini MWISHO UTAKUWA KULIPIA KODI NA NI MALI YA SERIKALI.
 
Kwanini tusiwahamishe wakojani na wangazija wa Pemba ili kulinda ecosystem ya kisiwa cha watalii??
Au tumuulize wale wanopakana na mbuga kama serengeti, mikumi, selous, manyara wao hawazaliani na kuingilia ecosystem ya mbuga hizo........au kuzaliana kupo kwa wamasai pekee, inashindikana nini ku limit eneo ambalo masai wanatakiwa wasiingie zaidi kwenye eneo la hifadhi kwa kuweka mipaka badala ya kuwaondoa wote kwenye eneo ambalo wameweka makazi kwa miaka mingi huku wakiendelea kudumisha mila na tamaduni na kuongeza chachu ya utalii.
 
Nchi za wenzetu zipi. Unajua walipo Red Indians kule Marekani? Vipi kuhusu aboriginal people of Australia wako wapi? Kwanini wanaharakati wasianzie uko

Hii dunia haitaki makasiriko wale watu walikuwa wanakaa porini wanapinga reli zisipite, airports wasingeruhusu zijengwe, viwanda wala machimbo ya madini. Huwezi mwambia mzungu upuuzi kama huo. Walihama tu

Hata Uingereza yenyewe ilihamisha thugs na ikawapeleka Australia na ndio mwanzo wa ile nchi kuwepo. Sasa hawa badala ya wapambane kupata sehemu ya kuhamia wanaleta habari za Middle Stone Age!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…