Serikali: Ardhi ya Tanzania ni mali ya Umma siyo ya Kabila moja, Katiba imemkabidhi Rais wa JMT aisimamie

Serikali: Ardhi ya Tanzania ni mali ya Umma siyo ya Kabila moja, Katiba imemkabidhi Rais wa JMT aisimamie

Wenzetu wanajua kutetea haki zao, hawakubali kuburuzwa na kuonewa na serikali. Watanzania wamebakia kusema wamasai wafukuzwe kama makabila mengine yalivyofukuzwa. Mawazo ya kijamaa.

Tuna hasara kubwa sana kama mtu mwenye PHD anaweza toa tafsiri ya sheria namna hii.

Ndio maana law firm yake imenyanganywa kesi na benki moja maarufu kwa kufanya kesi nyingi kwa uzembe.

Hakuna mahali mtu anadai ardhi flani ni ya kabila flani na hata hivyo mbona kila mkoa umegawanyika kwa makabila??
 
Nchi za wenzetu na UN wanatambua na kulinda haki za indiginous na minority groups.....nyie ni kujitia ujuaji na ku apply ubabe eti watu hawana haki na ardhi bali rais ndo anamiliki ardhi nchi nzima, kama kuna watu wanasaka maslahi binafsi kwenye hili lazima liwatokee puani......muda utaongea.
Wanataka wawatoe wamasai ili waiuze kwa mabwanyenye wa kiarabu,,,,.
 
Haki za indigenous people zina Mipaka na Exceptions. Pale Ngorongoro haki za Wamasai juu ya Ardhi wanayoishi zina mipaka ndio maana sheria imewapa limitations kwenye uendelezaji wa makazi yao na ufanyaji wa shughuli zao za kiuchumi. Hiyo ni kwa maslahi ya vizazi vya sasa na vya baadae.

Katika muktadha mpana, in longterm, wamasai hawafai kuwepo pale kwenye hifadhi kwasababu kama jamii yoyote jamii ya watu wanaoishi mbugani inakuwa kwasababu ya kuzaliana. Kadri inavyokuwa mahitaji ya eneo kwa ajili ya makazi na uzalishaji mali unaongezeka. Hii inamaana taratibu wataingia kwenye eneo la mbuga ili kukidhi mahitaji yao ya ardhi. Hilo litaathiri natutral habitat na baadhi ya ecosystems ktk hilo eneo. So ktk muktadha wa uhifadhi, in long term sio sustainable kabisa wao kuwa pale.
Kwanini tusiwahamishe wakojani na wangazija wa Pemba ili kulinda ecosystem ya kisiwa cha watalii??
 
Kwahiyo kwa Akili yako unaona haki za Binadamu zina mipaka ila haki za wanyama hazina mipaka na hapo umesomeshwa kwa Kodi za wananchi.
Hao wanyama hawaongezeki wew pimbi? Je kesho wakisema Kariakoo iwe hifadhi ya wanyama kwa kuwa nyati wameongezeka Sana na hawana makazi utakenua tuu meno yako?
 
Waziri wa Maliasili na Utalii Dr Damas Ndumbaro ametoa kauli ya serikali kuhusiana na mgogoro wa Ngorongoro. Dr Ndumbaro amesema ardhi ni mali ya Umma wa watanzania siyo mali ya kabila fulani na katiba ya JMT imempa Rais madaraka ya kuisimamia, kuiendeleza na kulipa fidia panapohitajika.

Ndumbaro amesema kwa sasa mkuu wa mkoa wa Arusha yuko kwenye majadiliano na mailagwanani wa kabila la Wamasai na akikamilisha ndipo tume ya serikali itakwenda na kuandaa ripoti ambayo itakabidhiwa bungeni.

Chanzo: ITV
Uonevu hauozi. Ni akiba.
 
Huyu naye ni Vuvuzela. Hakuna mtu anayeitetea ardhi kwa sababu ni mmaasai. Watu wanatetea ardhi wanayoishi.
Hata leo ukienda Iramba ukataka kuchukua ardhi, utakaowakuta wengi ni Wanyiramba au ukienda kwao Songea, waathirika wengi watakuwa nduhu zake Wangoni. Na wakilia, haimaanishi wanajiona ardhi ni ya kabila lao. Wanamaanisha ardhi yao kama sehemu ya Watanzania. Aache uvuvuzela bana.
 
Nchini DeMark ukitaka kuuza shmba inatangazwa na serikali. Huwezi kurthisha familia kama hana mafunzo angalau ya diploma ya kilimo. Naye utamuuzia na atalipiwa na serikali ni mkopo ndio aendeleze eneo kwa kilimo cha mazao au ufugaji. Je mwenye ardhi NI NANI HAPA. Usidanganywe ardhi mwishonicni mali ya serikali. KAMA YA KWAKO VIPI UNALIPIA KODI. Wanavyopima vijijini MWISHO UTAKUWA KULIPIA KODI NA NI MALI YA SERIKALI.
 
Kwanini tusiwahamishe wakojani na wangazija wa Pemba ili kulinda ecosystem ya kisiwa cha watalii??
Au tumuulize wale wanopakana na mbuga kama serengeti, mikumi, selous, manyara wao hawazaliani na kuingilia ecosystem ya mbuga hizo........au kuzaliana kupo kwa wamasai pekee, inashindikana nini ku limit eneo ambalo masai wanatakiwa wasiingie zaidi kwenye eneo la hifadhi kwa kuweka mipaka badala ya kuwaondoa wote kwenye eneo ambalo wameweka makazi kwa miaka mingi huku wakiendelea kudumisha mila na tamaduni na kuongeza chachu ya utalii.
 
Nchi za wenzetu na UN wanatambua na kulinda haki za indiginous na minority groups.....nyie ni kujitia ujuaji na ku apply ubabe eti watu hawana haki na ardhi bali rais ndo anamiliki ardhi nchi nzima, kama kuna watu wanasaka maslahi binafsi kwenye hili lazima liwatokee puani......muda utaongea.
Nchi za wenzetu zipi. Unajua walipo Red Indians kule Marekani? Vipi kuhusu aboriginal people of Australia wako wapi? Kwanini wanaharakati wasianzie uko

Hii dunia haitaki makasiriko wale watu walikuwa wanakaa porini wanapinga reli zisipite, airports wasingeruhusu zijengwe, viwanda wala machimbo ya madini. Huwezi mwambia mzungu upuuzi kama huo. Walihama tu

Hata Uingereza yenyewe ilihamisha thugs na ikawapeleka Australia na ndio mwanzo wa ile nchi kuwepo. Sasa hawa badala ya wapambane kupata sehemu ya kuhamia wanaleta habari za Middle Stone Age!
 
Back
Top Bottom