Serikali awamu ya sita inalipa mishahara mapema kabisa tarehe 22, imevunja rekodi ya Hayati Magufuli wa akilipa tarehe 25 mpaka 27. Hongera Rais Samia

Serikali awamu ya sita inalipa mishahara mapema kabisa tarehe 22, imevunja rekodi ya Hayati Magufuli wa akilipa tarehe 25 mpaka 27. Hongera Rais Samia

M
kwani magufuli kachaguliwa na nani na kwa uchaguzi gani wacheni utani bora huyu aliyewekwa kwa uwezo wa mungu kuliko magufuli aliyeuwa na kutesa ili aingie madarakani.
Magufuli alichaguliwa na wananchi wa Tanzania.Kasoro ww ndio hukumchagus
 
Siku ni 30 zilezile, Hakuna kitu kinaitwa mshahara kuwahi.
Hata ukilipwa tarehe 15 ya kila mwezi na mwingine akilipwa tarehe 30 kila mwezi , wote mmelipwa sawa Hakuna aliyewahi Wala kuchelewa
Mawazo ya Kinyonge sana haya,
Ukipewa mshahara mapema utakwisha mapema.
ukicheleweshewa utachelewa kuisha, lakini gape ni ile ile na matumizi ni yale yale.
Swali JE MSHAHARA UNATOSHA NA KUKIMU MAHITAJI YA LIA SIKU?
 
Trh 22 mpaka trh 22 ni mwezi mmoja na trh 27 mpaka trh 27 ni mwezi. Btw UMOJA party moja ya sera zetu ni kulipa mishahara mitatu trh 1, trh 10 na trh 25. the ends must meet by any means
Naona tangu umeachwa yatima na jiwe siku hizi masharubu yako yamefifia kama jua la jioni.
 
Kutoka tarehe 27 ya mwezi wa tatu mpaka tarehe 27 ya mwezi wa nne ni siku 30.

Kutoka tarehe 22 na mwezi wa watu mpaka tarehe 22 ya mwezi wa nne ni siku 30.

Kujali watumishi sio kupunguza namba za tarehe bali ni kuongeza namba za mmshahara

Ingekuwa ina logic endapo kila mwezi anapunguza siku tatu katika kulipa mshaharaa

Yaani mwezi wa kwanza amelipa tar 23
Mwezi wa pili analipa tar 20
Mwezi wa tatu analipa tar 17
Mwezi wa nne analipa tar 14 kama hivyo yani,kinyume na hapo nothing new.
[emoji123][emoji123]
 
Mambo mengine kwa kweli unaweza kusema ni ndoto.

Ilikuwa kawaida watumishi wa umma kuanzisha nyuzi za kuuliza mishahara kama imetoka, nyuzi hizo hapa JF zimekufa kifo Cha asili (natural death). Mama Samia analipa mishahara mapema kabisa kuliko Rais yeyote tangu nchi ipate uhuru.

Hakika anajali watumishi wa umma.

Viva mama SSH, nchi iko mikono salama.

Kazi inaendelea.

Eeeehh mama ajenga nchi....eeehh mama ajenga nchi *3
Hoja si kulipa mshahara tarehe ya mapema zaidi; bali kulipa mshahara siku iliyopangwa. Nilipokuwa mtumishi wa serikali miaka ya 70/80 siku ya mshahara ilikuwa tarehe 25. Siku hiyo ilikuwa haipiti bila mfanyakazi kulipwa. Wafanyakazi wa East African Community walikuwa wakilipwa siku ya mwisho ya mwezi: kwa mfano tarehe 28 Februari; tarehe 31 Marchi; na tarehe 30 Aprili. Nao mishahara yao ilikuwa haikawizwi kufikia tarehe 1 ya mwezi unaofuata. Kutopitisha siku iliyopangwa ndiko kwa kusifia.
Wakati wa Kikwete, ikawa wafanyakazi wa Serikali wanasubiri hadi katikati ya mwezi unaofuata; na wengine, kama waalimu, wanakaa hata miezi miwili/mitatu bila mshahara. Hilo ndilo alikuja kulishughulikia Magufuli. Baada ya miezi michache tu ya kuwa madarakani, akalipa malimbikizo yote ya stahili za watumishi wa serikali, na akarudia utaratibu wa kulipa mishahara tarehe iliyopangwa.
Kulipa mshahara kabla ya tarehe iliyopangwa siyo kitu cha kusifia, na haipashwi kuwa hivyo, kiuchumi na kiutawala. Labda kama siku ya mshahara inaangukia Jumapili, au siku ya sikukuu, ndipo mshahara ulipwe siku ya mwisho ya kazi kwa wiki hiyo. Kumsifia Mama kwamba amelipa mshahara tarehe ya mapema zaidi hakuna mshiko.
 
Kutoka tarehe 27 ya mwezi wa tatu mpaka tarehe 27 ya mwezi wa nne ni siku 30.

Kutoka tarehe 22 na mwezi wa watu mpaka tarehe 22 ya mwezi wa nne ni siku 30.

Kujali watumishi sio kupunguza namba za tarehe bali ni kuongeza namba za mmshahara

Ingekuwa ina logic endapo kila mwezi anapunguza siku tatu katika kulipa mshaharaa

Yaani mwezi wa kwanza amelipa tar 23
Mwezi wa pili analipa tar 20
Mwezi wa tatu analipa tar 17
Mwezi wa nne analipa tar 14 kama hivyo yani,kinyume na hapo nothing new.
Afanye hivi tarehe 15/ya mwezi alipe advance ya 50% na mwisho wa mwezi 30/mwezi alipe salio.ikumbukwe akilipa tarehe 30 Hadi 30 ya mwezi unaofuata ni siku 30,tunataka increment,top up,bonus,promotion ,
 
Siku ni 30 zilezile, Hakuna kitu kinaitwa mshahara kuwahi.
Hata ukilipwa tarehe 15 ya kila mwezi na mwingine akilipwa tarehe 30 kila mwezi , wote mmelipwa sawa Hakuna aliyewahi Wala kuchelewa
Nyie mchokozeni mkilipwa tarehe 38 ndipo mtaelewa. Vita Ukraine havijaisha.
 
Mnasifiana kulipa mishahara wakati mnakopa kujenga vyoo.
 
Mambo mengine kwa kweli unaweza kusema ni ndoto.

Ilikuwa kawaida watumishi wa umma kuanzisha nyuzi za kuuliza mishahara kama imetoka, nyuzi hizo hapa JF zimekufa kifo Cha asili (natural death). Mama Samia analipa mishahara mapema kabisa kuliko Rais yeyote tangu nchi ipate uhuru.

Hakika anajali watumishi wa umma.

Viva mama SSH, nchi iko mikono salama.

Kazi inaendelea.

Eeeehh mama ajenga nchi....eeehh mama ajenga nchi *3
Kama unakumbuka vizuri, Mwamba Magufuli aliwahi kulipa mishahara tarehe 19.
 
Kama unakumbuka vizuri, Mwamba Magufuli aliwahi kulipa mishahara tarehe 19.
Hamna kitu kama hicho, labda alikuwa analipa wakandarasi wa kichina kwa wakati pamoja na kampuni ya mayanga, kwa upande wa kampuni ya mayanga,alikuwa anawapigia mameneja wa tanroad moja kwa moja kuwauliza kwa nini hawajailipa mayanga
 
Kaa na ujuha wako. Na kwa taarifa yako, data ziko wazi, hakuna mwezi Mwamba Magufuli alilipa mshahara tarehe 25. HAKUNA! Ila sasa hivi Kuna hofu miongoni mwetu watumishi kwamba, zikiisha pesa alizokuwa amekusanya Mwamba Magufuli tutaanza kulipwa tarehe 40! Na hiyo haipo mbali!
 
Mwezi wa saba utacheka, chapa kazi, mama anapandisha maslahi ya watumishi. Kazi iendelee
Mkuu mimi nina matumaini na mama samia kuliko maelezo kwa sababu naamini ni mtu mwema tu
 
Mambo mengine kwa kweli unaweza kusema ni ndoto.

Ilikuwa kawaida watumishi wa umma kuanzisha nyuzi za kuuliza mishahara kama imetoka, nyuzi hizo hapa JF zimekufa kifo Cha asili (natural death). Mama Samia analipa mishahara mapema kabisa kuliko Rais yeyote tangu nchi ipate uhuru.

Hakika anajali watumishi wa umma.

Viva mama SSH, nchi iko mikono salama.

Kazi inaendelea.

Eeeehh mama ajenga nchi....eeehh mama ajenga nchi *3
Hili nalo Lina maana gani wakati kutoka tarehe 22 hadi tarehe 22 ni siku 30 sawa tuu na anaelipa tarehe 30 ya kila mwisho wa mwezi?
 
Mambo mengine kwa kweli unaweza kusema ni ndoto.

Ilikuwa kawaida watumishi wa umma kuanzisha nyuzi za kuuliza mishahara kama imetoka, nyuzi hizo hapa JF zimekufa kifo Cha asili (natural death). Mama Samia analipa mishahara mapema kabisa kuliko Rais yeyote tangu nchi ipate uhuru.

Hakika anajali watumishi wa umma.

Viva mama SSH, nchi iko mikono salama.

Kazi inaendelea.

Eeeehh mama ajenga nchi....eeehh mama ajenga nchi *3

Niishie tu kusema hili Taifa bado lina watu wajinga sana!
 
Mkuu, nchi iliharibiwa sana na JPM, mama anaisuka, Tulia, safari ya kaanani iko asilimia 80
Nilikwambia na narudia tena, tafuta jamaa wa kutoka Mara (wajita) wakupe maana ya avatar name yako, vinginevyo utaendelea kuandika utumbo mpaka siku unafunguka akili.

22th march to 22th april is almost 30days to pay salary, next time utulie usiandike 🤮, kama unahamu ta kuwadanganya watu nenda tbc, channel 10 au uhuru media, humu hupati mtu zaidi ya nyie wenyewe.
 
Back
Top Bottom