mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,897
- 18,477
Mimi naona viongozi wa dini wadai huo mrejesho kupitia mkutano maalumu wa vyombo vya habari. Halafu pia maoni ya viongozi hao wa dini wayaweke wazi!!Sintofahamu inayoendelea sasa hivi Issue ya Dp World ilitakuwa kuwa solved kidogo tu.
Viongozi wa serikali walikutana na viongozi wa dini kuhusu hilo swala Wakaeleza kutoridhikia na wakatoa maoni yao na kusihi serikali na bunge waangalie ushauri wao wawape mrejesho.
Matokeo serikali na bunge wakakaa kimya no feedback na badala yake moto unawashwa ohh viongozi wa dini waache siasa na vitisho kibao.
Hilo sio afya kwa taifa. Serikali International mrejesho wa walipofikia kulikuwa na shida gani? Hata huo waraka wa maaskofu usingetoka na maskofu wangefanya kazi kuelimisha waumini wao hatua serikali au bunge wamechukua kurekebisha kasoro.
Lakini hii foka foka ya viongozi wa Serikali na bunge si afya sana kwa taifa.
Hoja zijibiwe kwa hoja. Wananchi wakitaka feedback wapewe.
Na kukaa kimya sio sahihi ni sawa na kusema bora liende.