Serikali baada ya kukutana na viongozi wa dini ilitakiwa irudi tena kuwapa mrejesho mapendekezo yao Serikali imefikia wapi

Mimi naona viongozi wa dini wadai huo mrejesho kupitia mkutano maalumu wa vyombo vya habari. Halafu pia maoni ya viongozi hao wa dini wayaweke wazi!!
 
Serikali hairipoti kwa viongozi wa dini. Kumbuka hilo.

Serikali imeshaelezea kuhusu bandari vyakutosha, hatuoni sababu ya serikali kuendelea kujibizana na wajinga.

Sisi tubishane hapa JF, yesha. Ujinga wetu hapa ubaki hapahapa.
Wajinga ni kina nani? Mama aliwaahidi viongozi wa dini kuwa maoni yao yatazingatiwa lakini mkatabna ukapitishwa na bunge kama ulivyokuwa bila maoni yao kuzingatiwa!! Ndio maana wakatoliki wameamua kutoka hadharani na kutoa waraka wao. Maana huo wa viongozi wa dini umetupwa kapuni!! Tumewashtukia hao waarabu wenu hawatakuwa na ubavu wa kuingia Tanzania!! Tutachoma moto kanzu zao!!
 
Hawezi kutudanganya eti hakuna mwenye ubavu wa kuuza Taifa hili wakati keshaliuza tayari kwa waarabu!! Hivi kumpa mwarabu bandari zote za Tanzania bara aziendeshe na kuzisimamia bila ukomo wa muda kuwekwa wazi si ndio kuuza kwenyewe!! Muda wote huo watanzania hawatakuwa na la kusema kuhusu bandari zao. Na mbaya zaidi mkataba hautoi kipengele cha kuuvunja hata iweje!! Msituone wajinga!!! Kauzeni vya Zanzibar!!!
 
Nawachukia kwa wizi wao!!! Wakikubali kubadilisha mkataba uwe rafiki (win win) hapo sawa tutawakaribisha na kanzu zao!! Hatuwezi kumchekea mwizi wala kibaraka wao!! Acha ujinga, hizo trilioni unazotaja ziko kichwani kwako tu na hazitajwi na mkataba huo wa kijambazi!!
 
Dunia hii ni ya makubaliano kibiashara....
Nakubaliana na wewe kuhusu makubaliano ya kibiashara lakini yasiwe makubaliano ya upande mmoja kuporwa bandari zake jumla!! Tatizo liko hapo!! Mkataba wa hovyo wa kutoa bandari zetu zote jum;la bila ukomo!! Huu ujinga haukubaliki!! Kuna watui waqmeuza bandari zetu hapo!! Kama kuna kitu walichukua watajuana huko huko!! Mwarabu wa DP World hatatia mguu wake Tanzania kwa mgongo wa mkataba huu wa bandari!!
 
Hizo trilioni 26 zimeainishwa kwenye kifungu kipi cha mkataba!! Mkataba wote ninao hapa!!
 
Kwani serikali inawajibika kwa viongozi wa dini au kwa raia, inawapa je majibu kwani hao ni muhimili?
Kama inawajibika kwa raia na viongozi wa dini sio raia basi iendelee kushughulika na hao raia wake. Iache kuwatisha viongozi wa dini wanapoandika barua.
 
Kwani serikali inawajibika kwa viongozi wa dini au kwa raia, inawapa je majibu kwani hao ni muhimili?
Cjui nan kawaloga bongo zenu nyie watu!! Hao viongoz ni kwa vyeo tu lkn ni watanzania kama wengine, ambapo serikali ilipaswa kutoa majibu kwa wananch na sio viongoz wa dini kama vyeo!!
 
.... maamuzi magumu HAYANA kubembelezana......

#Hakuna mwenye misuli ya kuligawa taifa hili wala kuliuza [emoji120]
Aliewapa dhamana ya kuitetea serikali mitandaon kiukwel kbs amekosea san, mnashindwa kuwajibu watanzania kwa hoja, mnakuja kuongea kauli za hovyo zisizo na tija!!
 
Mtamuuzia nani? Hiyo imekamatwa ili tapeli arudishe fedha zao. Alidhani atapitisha kwa mabavu kama walivyozoea.
Kama haiuziki wameikamata ya nini? Waiweke makumbusho?
 
Kumbe kishauza bandari zote? Basi wewe poyoyo kweli kweli, Bandari mpaka zinauzwa ulikuwa wapi?
 
Kwani walikubaliana timeline ya mambo hayo?
 
Kwani serikali inawajibika kwa viongozi wa dini au kwa raia, inawapa je majibu kwani hao ni muhimili?
Kwanini serikali iliwaita kuongea nao tena waziri Mbarawa ndiye aliewakilisha serikali.
 
Kwani walikubaliana timeline ya mambo hayo?
Raisi angejibu kwenye hotuba kule Moshi miaka 60 ya KKKT angetumia hiyo nafasi vizuri kusema tunaendelea kushughukia maoni yote ya wananchi wote wakiwemo viongozi wa dini

Statement ya vitissho aliyotoa iko chini ya kiwango

Wakiamwandikia hotuba wanechemka

Viongozi wa dini huwezi watishia nyau tena wa kanisa kubwa kama katoliki

Raisi apange safe mpya ya washauri

Hasa kwenye issue zihusuzo mahusiano ya serikali na viongozi wa dini

Kuna washauri hopeless na hawajielwi watatumbukiza nchi kwenye shida kwa kukosa hekima ndogo tu

Nchi ikitumbukia kwenye vita wanajeshi ndio watakesha usiku na mchana kupambana na wananchi wakati wanasiasa watakuwa wanalala fofo na wake zao au waume zao wakikumbatiana na kubusiana wanajeshi wakiwa vitani

Huu ujinga jeshi na vyombo vya usalama vikae mbali waache serikali na bunge wajibu hoja za wananchi sababu likiibuka la kuibuka wao ndio watakesha mitaani.wanasiasa watalala fofofo na watoto wao na wake na waume zao watawapeleka uarabuni, ulaya na Marekani nk wananchi wa kawaida wakiwa hawana kwa kwenda

Huu muziki wa DP World uachwe wananchi na serikali na bunge wapambane .Jeshi na mahakama wakae mbali
 
Mimi naona viongozi wa dini wadai huo mrejesho kupitia mkutano maalumu wa vyombo vya habari. Halafu pia maoni ya viongozi hao wa dini wayaweke wazi!!
Vyombo habari vyote kuna taarifa za chini chini jukwaa la wahariri kasoro jamii forums wamehongwa hela nyingi mno kutotoa taarifa .Viongozi wa serikali walikutana na jukwaa la wahariri It was fine haina shida

Shida kuna tuhuma za bahasha za rushwa za kuhongwa jukwaa la wahariri.Ndio maana kanisa katoliki likaona isiwe kesi kama vyombo vya habari wahariri wamehongwa waraka utasomwa direct makanisa yote nchi zima mijini na vijijini kusiko na TV,wala magazeti wala Fm Radio
 
Usemi wa zama za kale hata leo Bado unatumika, "Roma ikishazungumza, mjadala umekwisha" Achana na matapeli wa kidini na kisiasa, wanaotafutia watoto wao chakula serikalini, lisikilizeni kanisa, mkiacha kusikiliza lenyewe halina cha kupoteza, mtakaopoteza ni nyinyi na vizazi vyenu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…