Serikali bado haijaelewa maana ya maandamano siku hizi. Serikali itatue kero za waandamanaji

Serikali bado haijaelewa maana ya maandamano siku hizi. Serikali itatue kero za waandamanaji

Mimi bado naamini wanaochochea hisia za watu kuandamana wapo kwenye mfumo na wanafanya hivyo makusudi ili kujipata pesa kilaini isiyo na Querry kwa Mkaguzi wa hesabu za Serikali.
Vijana wengine nao kama nyumbu wanatumika kuwasaidia watu kula pesa bila kujua.
Jana kuna mtu nimetoka kumwambia kitu kama hiki, hata wale mashekhe ubwabwa akina Mwapopo sijui na yule mashavu hizi project zao sijui za kupinga maandamano wanapiga sana hela na wanatamani hii hali iwe endelevu wapige hela
 
Kuna Mapolisi wanatamani kumshkuru alietangaza maandamano ya Mchongo maana hizi posho zitapush ada za shule sana.
 
Ahaa ila siwanapewa posho za bure mkuu.

Ukiangalia haya mambo unaona wa chini atazidi kukandamizwa na wajuu atainuliwa .

Kwakuwa Leo 7/7 ilikuwa ni siku ya wavuja jasho kupata pesa kwa kufanya kazi na biashara ila wapo ndani na kesho Ada zinahitajika

Maana Leo ni Saba Saba na ndo siku watu waliitegemea wapate pesa
Na ndiyo wanazidi kuichukia serikali kwa kuleta taharuki isiyokuwa na msingi hata kuwalaza njaa wao na familia zao,em waza hivi......

What if hao serikali wangewaruhusu hao waliojiita waandamanaji kuandamana kwa kuwapa zone maalum kila wilaya kila mkoa kwamba maandamano yaanzie hapa mpaka pale yakiwa chini ya ulinzi ujumbe wao upokelewe huku sehemu nyengine watu wakiendelea na shughuli zao unaona ikileta shida?ujinga tu jana nafanya mazoezi barabara ya Morogoro nimekutana na magari ya jeshi niliyahesabu 24 yamejaa tena wamefanya kushindiliwa hii yote ya kazi gani?
 
Jana kuna mtu nimetoka kumwambia kitu kama hiki, hata wale mashekhe ubwabwa akina Mwapopo sijui na yule mashavu hizi project zao sijui za kupinga maandamano wanapiga sana hela na wanatamani hii hali iwe endelevu wapige hela
Ufinyu wa akili. Halafu wakipiga hizo hela watahama nchi?
 
Jana kuna mtu nimetoka kumwambia kitu kama hiki, hata wale mashekhe ubwabwa akina Mwapopo sijui na yule mashavu hizi project zao sijui za kupinga maandamano wanapiga sana hela na wanatamani hii hali iwe endelevu wapige hela
Yah, hii ni win win situation sasa hivi, wanaharakati wanahamasisha maandamano nao wana malengo yao, huku mtaani kuna wanaoyapinga maandamano nao wanamikakati yao na kila mtu ana malengo yake. Na kuyaendea yote hayo kuna faida wanapata. Maisha yanasonga mbele.
 
Kaka ,Hakuna posho za bure,wale askari wanateseka,wanashinda Juani wanaficha sura zao na masoksi meusi,na joto la Dar unaweza kuelewa wanachopitia,wale askari wako psychologically torched maana wanafanya tu kazi sababu hawana namna...

Na kuhusu watu kukosa kipato hiyo ndio indicator ya kwanza kwamba serikali imefeli,maana serikali nzuri ni ile yenye stability na yenye mazingira salama kwa kwa raia wake.Sasa kama wananchi hawaingizi kipato unadhani kodi itapatikana wapi kwa hiyo serikali?na leo sio 7/7 tu iliyosimama,Kariakoo imesimama,sector ya utalii lazima imesimama hapa hakuna cha wajuu kuinuliwa wala nini hapa ni serikali inazidi kuzorota....Yaani wahamasishaji wamefanikiwa kuidhoofisha serikali
Wewe sikia,
Hao askari barabarani iyo ndo kazi yao.!
Kwanza hawanaga kazi nyingine.,bora hata mara moja moja wafanye mazoezi kidogo ya kushughulikia wavunja amani ya nchi.
 
Mimi ni realistic , Kuna baadhi ya mambo hauwezi kuyabadilisha ila unabidi kuangalia namna ya ku fix mambo ili uifikie target yako ktk maisha

Politicians plus activists wote Hawa ni wasaka fursa so ukiwaona Wana push ajenda ujue wameshajua maslahi yao yatakuaje.

Ni kweli we need mabadiliko ila sio kwa aina ya watu tulizonao
Ukisema kuna baadhi ya mambo huwezi kuyabalisha unakosea big time!hakuna kichoweza kubadilika ni suala la muda tu!unakumbuka CCM ya mwaka 90?yaani ukisikia zile nyimbo za John Komba nchi inasimama,vipi leo?leo ni aibu hata kuvaa tisheti au kofia yenye rangi ya kijani japo haina hata chata ya CCM,yaani ile rangi tu! Je kwa nini?sababu mambo yanabadilika.
Halafu wewe ni aina ya watanzania wengi ambao hamna imani kwa serikali lakini pia hamna imani katika mabadiliko yaani mko katikati,hapo sasa inabidi mchague upande mmoja kusimama na serikali au na wananchi wanaotaka mabadiliko na sio kuwa mpo mpo tu .
 
Wewe sikia,
Hao askari barabarani iyo ndo kazi yao.!
Kwanza hawanaga kazi nyingine.,bora hata mara moja moja wafanye mazoezi kidogo ya kushughulikia wavunja amani ya nchi.
Kwamba ukimuona Padre kwenye altare au Sheikh kwenye mimbari amesimama hutakiwi kumuonea huruma.😀
 
Ukisema kuna baadhi ya mambo huwezi kuyabalisha unakosea big time!hakuna kichoweza kubadilika ni suala la muda tu!unakumbuka CCM ya mwaka 90?yaani ukisikia zile nyimbo za John Komba nchi inasimama,vipi leo?leo ni aibu hata kuvaa tisheti au kofia yenye rangi ya kijani japo hana chata ya CCM,kwa nini?sababu mambo yanabadilika.
Halafu wewe ni aina ya watanzania wengi ambao hamna imani kwa serikali lakini pia hamna imani katika mabadiliko yaani mko katikati,hapo sasa inabidi mchague upande mmoja kusimama na serikali au na wananchi wanaotaka mabadiliko na sio kuwa mpo mpo tu .

Kwahiyo unavyodhani wanahitaji mabadiliko ni GEN Z vijana wa miaka 18+30 tu

Ila nyie watu wa miaka ya 70 na 80s hamtaki mabadiliko

Kwanini mnadhani GEN Z peke yao ndo Victim wa serikali ya CCM

Kama unataka mabadiliko usiiishie kuandika andika hapa chukua bango uingie barabaran uandamane

Be the change u wanna see , usifikiri Kuna MTU anabidi kuandamana kwa ajili yako hayupo na hatokuja kuwepo
 
Dunia ya sasa imebadilika sana teknolojia inabadili kila kitu, leo tunaona Genz wa Tanzania wamengundua njia nyingine ya kuichosha Serikali, wanaitasha maandamano kwenye mitandao, matokeo yake serikali inahangaika kutawanya vyombo vya dola na kutumia rasimali pesa nyingi kukambiliana na hofu ya maandamano
Matokeo yake, jumuia ya kimataifa inaiona serikali hii ni ya kidikiteta, wawekezaji wanaanza kuona nchi hii sio sehemu salama tena ya kuwekeza mitaji yao, vyombo vya dola navyo vinaanza kuichoka serikali, just imagine leo ndio siku kuu ya sababa wale wafanyabiashara pale kwenye maonesho hakuna watu.
Mwisho wa siku ni anguko kwa serikali hii.
 
Back
Top Bottom