Serikali: Bajeti ya sensa ni Tsh bilioni 629

Serikali: Bajeti ya sensa ni Tsh bilioni 629

Kiruuuuuuuuu, mtaani kwetu nyumba zilizohesabiwa hazifiki 8 na nyumba moja mtu anakaa masaa 5-6. This is a joke...
Kinachoendelea waTanzania tuko kwenye shida. Hapa wanapokea data sidhani kama wanauhakika na watakacholeta mezani.

Japo kikubwa kwao ni KUTOA mafanikio sana ya asilimia 110 tuendelee kishangaa. Ili mradi hizo data zitawaendea wafadhili wanaowaita mabeberu ilinwapate pesa ya Maendeleo na watatia mfukoni tu.

Katika hizo siku Saba waje pia na taarifa za vifo na wazaliwa kinyume ya hapo ni feki taarifa.!
 
Sio kwa Watanzania hawa.
Upuuzi wamefanyiwa mara nyingi hakuna walichokifanya.
Hakuna Mtanzania wa kuipinga serikali
Hujawahi shuhudia wehu ngoja muwatibue vizuri tena nakwambia ogopa sana mtu mkimya. Balaa lake huwa zito na baya sana.
 
Hii sensa ilipaswa kufanywa na kada ya walimu nafikiri ingefanyika kwa ufanisi zaidi, nilivyiwaangalia hawa makarani ni kama walikuwa wanafanya bora liende

Mimi nimehesabiwa leo mkuu, kwakweli karani aliyenihesabu imebidi tu nimjibu kwakuwa amenikuta nyumbani.
 
Nilivyoona tu siku ya kwanza ya sensa, nikajiambia mwenyewe kwamba hakuna sensa itakuwa na data za uongo kuliko hii tangu Tanzania hii kuumbwa.
 
Na huku ndiko tunakokwenda. Kama mpangaji hataki/hawezi, basi akatafute chumba mahali pengine.

Yaani ujenzi ulivyokua wa gharama kiasi hiki, halafu nitoe tu kirahisi 10% kugawana na serikali ambayo haijanichangia chochote kwenye ujenzi! Na bado kila mwezi nakatwa 1000 kwenye LUKU kama kodi ya jengo!
Unafurahia tu amani,mfumo uliopo...yaani usalama,huduma za afya,barabara,mpangilio wa makazi nk...hela ya ku-organize inatoka wapi!?..lipeni Kodi,mlizowea kuishi kijamaa Kama nguchiro kichuguuni
 
Kamisaa wa sensa Anna Makinda alieleza kuwa zoezi la sensa linakadiriwa kuwafikia watanzania milioni 64. Huku bajeti ya sensa ukiwa ni bilioni 629, kwa hesabu za St. Kanyunyuli darasa la 5C ni kuwa kila mtanzania amehesabiwa kwa sh. 11,000, ukizingatia hadi sasa wamehesabiwa 93%.

Tanzania nchi yangu, mama anakupiga mwingi, asali zimetujaa midomoni hadi tunashindwa kumeza.
 
Vifaaa vya kufanyia kazi unajua gharama zake ,zile tablet n.k..


Unajua gharama ya kuwapa watu semina na mafunzo mpaka kuelewa masomo ,muda ,chakula ,vipeperushi ....

Unajua gharama za kumuweka mtu mtaani kufanya kazi hio ,ndani ya siku Saba ?

Wewe ni mjinga tu ,unakimbilia cheap popularity huku jf ....
 
Tablets 200000+
Makarani + Maafisa maudhui + Tehama = 200000+
TTCL Internet
Reflector - 300000+
Vitabu vya miongozo
Kumbi za mikutano
Nk nk nk

Unapotoa tathmini yako zingatia sana hizo data.
 
Back
Top Bottom