Serikali: Bei ya Mchele imefikia Tsh. 3,500, Maharage 3,500, Mahindi 1,500 kwa kilo

Serikali: Bei ya Mchele imefikia Tsh. 3,500, Maharage 3,500, Mahindi 1,500 kwa kilo

Sio kila lazima awe mkulima Kuna viwanda vinahitaji wafanyakazi, serekalin wanahitaji wafanyakazi, utalii unahitaji wafanyakazi ukitaka kila mtu hiko kitu hakitakaa kitokee na inaonyesha ulivyokua na upeo mdogo

Hata bidhaa za viwandan vina Bei elekezi sio tu kwenye kilimo ni karibia sekta zote Wana Bei elekezi
Endelea kumwaga povu,kama unajua sio kila mtu awe mkulima basi nunua Kwa bei zilizopo ndio zinamlipa mkulima..

Hutaki kalime.
 
yaani hawa watu wanaoishi kwa kodi zetu wanatuchezea sana akili hawa, yaani wakikalia v8 zetu na wakiwa wamepanda ndege zetu wanaishiaga kukenua meno tu, wanatusahau kabisa kwamba tunateseka. Yaani mchele hadi unafikia kilo moja 3500 yenyewe ipo ipo tu ofisini haina hata mipango ya kunusuru wananchi. Mimi inafika mahali huwa nawaombea wafariki tu, yeyote ambaye amesahau wajibu wake ila mshahara wake anakumbusha kuongezewa ila hakumbushii kuomba aongezewe majukumu 😎 nawaombea watangulie mbele za haki tutawakuta tu.....
Wakishindwa kutumia akili zao vizuri watoke waingie wenye mawazo ya kuwakomboa wananchi katika mapito kama haya jamani, mtanisamehe ila yanaudhi kwakweli😡😡
 
Ku
Unauhakika kila mwenye fikra pevu ni mkulima na unauhakika kila tajiri ni mkulima mbona una mawazo mgando hivyo

Kwa nchi hii hakuna mkulima mwenye fikra pevu,hakika nakuambia!Angekuepo nchi hii tungeuza nafaka mpaka Ukraine.
Ninyi viongozi mna fikra pevu Ila mnawakomoa wakulima makusudi,
Baa la njaa halizuiwi kwa kufunga mipaka(mawazo ya kilevi)

Eee mwenyezi Mungu mwingi wa rehema wape wakulima maarifa ya kibepari kidogo tuu,hakika ninyi wenye viribatumbo vya maofisini mtanyooka
 
Nikukumbushe tayari serekali imepiga ban kuuza mazao nje ya nchi na sio Tanzania hata India ilipiga ban kuuza ngano nje ya nchi huwezi kuwa na taifa la watu wenye njaa
Hakuna ban iliyopigwa na kama itakuwa hivyo next year tutalima Mazao yetu ya kula wenyewe na tuendelee na mambo mengine afu tuwaone huko mjini mtakavyofanya..

Labda serikali itawalimia,siwezi limia wa mjini afu nipangiwe Bei, never
 
Serikali imetangaza ongezeko la bei katika baadhi ya bidhaa za vyakula, huku kushuka kwa uzalishaji ikitajwa kuwa sababu.

Miongoni mwa bidhaa za chakula zilizopanda bei katika mwaka ulioishia Septemba mwaka huu ikilinganishwa na mwaka ulioishia Agosti mwaka huu ni mchele, maharage, mahindi.

Hayo yameelezwa leo Septemba 15 na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dk Ashatu Kijaji wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya mwenendo wa bei za bidhaa katika mwaka ulioishia mwezi Agosti mwaka huu.

Dk Kijaji amesema bei ya mchele imeongezeka hadi kufikia kati ya Sh2000 hadi Sh3500 katika Septemba mwaka huu.

"Ikilinganishwa na Agosti mwaka huu bei ya mchele sokoni ilikuwa kati ya Sh1700 na Sh3000,"

Bei ya maharage ilifika kati ya Sh1, 750 hadi Sh3500 ikilinganishwa na Sh1800 hadi Sh2, 600 iliyokuwapo Agosti mwaka huu.

Kuhusu mahindi bei yake imefikia Sh900 hadi Sh1,550 kwa kilo ikilinganishwa na Sh700 hadi 1,500 Agosti mwaka huu.

Kuhusu uzalishaji wa chakula, mahindi yalishuka kwa asilimia 7.1, uzalishaji wa mchele ulishika kwa asilimia 30.9 na maharage uzalishaji ulishuka kwa asilimia 11.1. Kati ya mwaka 2020/2021 ikilinganishwa na Mwaka 2021/2022.

Ongezeko hilo la bei katika baadhi ya bidhaa za chakula na zisizo za chakula zimefanya mfumuko wa bei wa Taifa kuongezeka kwa asilimia 0.1 katika mwezi Septemba ikilinganishwa na mwezi uliotangulia.
Sasa inatusaidia nini kutuambia bei zimepanda bila kutuambia mkakati wao ni upi kufanya bei zishuke? Kwani sisi hatuoni kama zimepanda?
 
Sababu za athari zitokanazo na "Russio-Ukraine war" hazipigiwi upatu tena eeh! Itatupasa tujifunze mambo ya uongozi na utawala kutoka nchini Kenya.

Angalia jinsi Dr. Ruto atakavyounda Baraza la Mawaziri, angalia vipaumbele vyake vya kiuchumi na kijamii, angalia jinsi anavyoendesha ujasusi wa kiuchumi kimkakati, hayo yote yanashadishwa na kauli mbiu yake ya "Kenya Kwanza"
 
Basi iambie hiyo ban ishushe Bei basi
Nikikuita mjinga ntakua nakuosea
 
Ingia shambani kaka

Sent using Jamii Forums mobile app
Ilaumu serekali na sio watu wa jf ambao hawana mamlaka yeyote
 
Back
Top Bottom