DOKEZO Serikali chukueni hatua za haraka dhidi ya Nabii Dominiki "Kiboko ya Wachawi"

DOKEZO Serikali chukueni hatua za haraka dhidi ya Nabii Dominiki "Kiboko ya Wachawi"

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hizi ni Decoys mkuu wanatupofusha macho mambo yao yapite
 
Lengo la huh Uzi ni nini..!?

Ni Nabii kutumia Matangazo unayoyaita Fake Radioni ama..!?

Ni kitendo cha Kuwalipisha kiwango kikubwa cha pesa watu wanaoenda kuonana nae face to face...!?

Ama malalamiko yako yanamaanisha kwamba Ni Nabii Taperi asiye na ukweli wowote.....!?

Binafsi sikubaliani na namna yeye anavyowalipisha Watu pesa ili kumuona, Angetumia Ubunifu kama wa Mwamposa, pale anapowataka watu kuchangia kusambaza Injili, kwa sababu kuna gharama kubwa kurusha Matangazo iwe TV ama Radio...!

Aisifuye Mvua imemnyea, yakikukuta wewe mwenyewe utajua Manabii wote wanapatikana wapi.....!

Kile watu wasichojua Kuna mstari mdogo sana kati ya Nabii na Mganga wa Kienyeji, Mganga wa Kienyeji mpiga Ramli akiamua kuokoka akitaka kumtumikia Mungu, anakua Nabii straight, utofauti ni kwamba akiwa Mganga alikua anafanya kazi kwa Usaidizi wa Mizimu na Majini, na sasa ni Nabii anafanya kazi kwa usaidizi wa Roho Mtakatifu.

Kuna Matatizo ya Watu yanawahitaji Manabii moja kwa moja, kumsaidia mtu atoke shimoni then uanze kumfundisha kuomba, kufunga n.k....!

Mtu ana matatizo lukuki, ni Mgonjwa, hatembei, Macho hayaoni kwa sababu ya Husda za Wanadamu,hafu unamwambia asome Biblia, afunge, akemee, anaanzia wapi.... Unahitaji Nabii atayekwambia tatizo lako na kutatua then akufundishe kumtegemea Mungu.
Siyo kila anayejiita nabii na anahubiri jina la Yesu ni mkristo. Ukristo una principles zake. Ndiyo maana Yesu alisema siku ya mwisho kuna watu atawakataa lakini watamjibu walifanya miujiza kwa jina lake lakini ajibu SIWAJUI. Miujiza SI KIGEZO CHA UKRISTO au kwamba mtu ameitwa/ametumwa na MUNGU.
 
Siyo kila anayejiita nabii na anahubiri jina la Yesu ni mkristo. Ukristo una principles zake. Ndiyo maana Yesu alisema siku ya mwisho kuna watu atawakataa lakini watamjibu walifanya miujiza kwa jina lake lakini ajibu SIWAJUI. Miujiza SI KIGEZO CHA UKRISTO au kwamba mtu ameitwa/ametumwa na MUNGU.
Aisifuye Mvua imemnyea Mkuu, mimi ni Mhanga wa Matatizo ya Kiroho, na hao Manabii ndo walinisaidia.....!!

Watu wote wanaojaa kwenye hayo Makanisa, sio Wajinga, yamewafika.....! Ndo maana Bulkdozer huwa anasema Makanisani ni "Mtakuja" yatakapokufika wewe mwenyewe utaongoza njia...! Ama ndugu zako watakubeba kukupeleka ukiwa hujiwezi.
 
Mkuu, hoja yako ni ya msingi sana, lakini sio rahisi sana kwa dola yetu [polisi/serikali]kuingilia kati, kwasababu (1) waumini wa hayo makanisa huenda kwa hiyari yao [hawalazimishwi], na hakuna walalamikaji wa kuibiwa ama kutapeliwa.(2)Hawa wachungaji/maaskofu/mitume na manabii/makuhani n.k.wana ushirikiano mzuri na serikali,polisi huwahakikishia usalama, maeneo yao ya ibada...

Lakini,huu wizi,utapeli/ulaghai unaofanywa na baadhi ya viongozi wa hayo makanisa,ni wazi kuwa serikali inajua,ni kwanini hawachukuliwi hatua? Hapa nchini kuna NGO's,/mashirika mengi tofauti ambayo yanatambulika ni kwaajili ya kutoa misaada mbalimbali kwa jamii, lakini baadhi yao yamegundulika yanaharibu maadili yetu hasa kwa watoto na vijana,lakini bado yapo, serikali ipo pia.Jiulize ingekuwaje kama mwananchi/wananchi wa kawaida tu,wakutwe na sifa hizo,tungesikia na kuona kwenye vyombo vya habari wakisindikizwa kwa mitutu.Naweza kufananisha hili na maigizo ya serikali ya Congo dhidi ya kikundi/vikundi vya waasi.

Hivi ni kweli DRC inahitaji msaada wa kijeshi toka nje pamoja na jeshi la UN dhidi ya watu wasio wasofika laki moja [maximum]ambao wangeweza kuwasambaratisha bila hata kuwafuata msituni?

Ni maigizo... Maana yangu ni kuwa, hivi vitu havipo kwa bahati mbaya,ni mipango inayo ratibiwa na,amlaka [isiyotaka kujulikana]yenye nguvu sana nyuma yake,watawala wetu wanajua na hawawezi kupingana nayo,iwe kwa zuri au baya, linahitaji viongozi aina ya JP Magufuli[kwa tahadhari sana].

Hata hivyo,haya hayana budi kutokea kwasababu yalishatabiriwa kuwapo kwa nyakati za mwisho wa dunia kwamba watatokea, manabii wa uongo ila tutawajua kwa matendo yao, lakini kwasababu ya uvivu wa kusoma vitabu/Biblia,watu hawana,maarifa ya kulinganisha/kutofautisha huduma na miujiza aliyoifanya YESU KRISTO dhidi ya hii inayofanywa na hawa mawakala wa Shetani/Ibilisi.
 
Alafu mkongomani huyu
Hawa wengi matapeli tu
Wanacheza na akili za watu

Mfano leo hii,mm nianze kumshobokea kakob wakati
Wengine tumekuwa na tunamuona kakob anauza cd kko
Leo hii nabii 😄
Ukiishi kwa kuona mengi elimu tosha kabisa huwezi kubabaishwa
Na mtu

Ova
Kumbe ndio maana wayahudi wakampotezea Yesu kisa waliona huyu dogo fundi seremala tu
 
WATU wanapenda sana miujiza. Huyu sijui ndo yuko times fm anafoka saa zote!
kumna shost angu anakwambia kanunua mafuta ya 5000 kwa kuhani musa alivyopaka mbaya wake akampigia simu kumwambia yeye ndo anamroga! Anakwambia mama ake mdogo kayanunua ya laki moja ananiambia hayo ndo kiboko! Nikamjibu haya
 
Watanzania tunaangamia kwa kukosa maarifa

Why unaamini huyo tapeli?
 
Sure ,watu sijui wanadanganyika vipi na usanii wanaoufanya ,Tapeli Dominic anachofanya anaingia studio anarecord mazungumzo ya kisanii ya mpiga simu then wanyarusha Furaha Redio,Efm au Times FM.

Kuna siku kuna dada alimpigia simu kwamba hajui amepewa mimba na nani hivyo akampigia Kiboko ya wachawi amtajie ,then Nabii akamtajia kwamba ni Fundi Ujenzi ndiyo aliyempa ujazito kati ya wanaue wake sita.

Mimi huwa namsikiliza kama ze comedy huwa nafurahi sana anavyoigiza.
saa ngap mkuu wanaanza namimi nirefresh mind baada ya kusikiliza michezo
 
Alafu mkongomani huyu
Hawa wengi matapeli tu
Wanacheza na akili za watu

Mfano leo hii,mm nianze kumshobokea kakob wakati
Wengine tumekuwa na tunamuona kakob anauza cd kko
Leo hii nabii [emoji1]
Ukiishi kwa kuona mengi elimu tosha kabisa huwezi kubabaishwa
Na mtu

Ova
mkuu shikamoo
 
Kwani we ni mchawi hadi umuogope nabii anatishia nguvu zako.
Kama wanatoa kwa hiari Yao na pesa zao wewe shida Nini? Mbona kwa waganga wanatoa zaidi ya hizo.
Unayapimaje mafundisho kuwa ni ya kweli au uongo.
Kama avunji Sheria ya nchi hana kosa
 
Kuna jamaa wa karibu namjua amemchomoa milioni 2 .
Kumwambia kamtoa kitu tumboni akamwambia bado 2 kalete milioni 2 uje nimalizie kuvitoa.
Ka shida alokuwa nayo ikabidi akachukue bank akampa vikatolewa.
 
Serikali iko kimya,inajuwa wananchi wake mazoba na imeachqna nao wapigwe tu

Ova
 
Back
Top Bottom