DOKEZO Serikali chukueni hatua za haraka dhidi ya Nabii Dominiki "Kiboko ya Wachawi"

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hizi ni Decoys mkuu wanatupofusha macho mambo yao yapite
 
Siyo kila anayejiita nabii na anahubiri jina la Yesu ni mkristo. Ukristo una principles zake. Ndiyo maana Yesu alisema siku ya mwisho kuna watu atawakataa lakini watamjibu walifanya miujiza kwa jina lake lakini ajibu SIWAJUI. Miujiza SI KIGEZO CHA UKRISTO au kwamba mtu ameitwa/ametumwa na MUNGU.
 
Aisifuye Mvua imemnyea Mkuu, mimi ni Mhanga wa Matatizo ya Kiroho, na hao Manabii ndo walinisaidia.....!!

Watu wote wanaojaa kwenye hayo Makanisa, sio Wajinga, yamewafika.....! Ndo maana Bulkdozer huwa anasema Makanisani ni "Mtakuja" yatakapokufika wewe mwenyewe utaongoza njia...! Ama ndugu zako watakubeba kukupeleka ukiwa hujiwezi.
 
Mkuu, hoja yako ni ya msingi sana, lakini sio rahisi sana kwa dola yetu [polisi/serikali]kuingilia kati, kwasababu (1) waumini wa hayo makanisa huenda kwa hiyari yao [hawalazimishwi], na hakuna walalamikaji wa kuibiwa ama kutapeliwa.(2)Hawa wachungaji/maaskofu/mitume na manabii/makuhani n.k.wana ushirikiano mzuri na serikali,polisi huwahakikishia usalama, maeneo yao ya ibada...

Lakini,huu wizi,utapeli/ulaghai unaofanywa na baadhi ya viongozi wa hayo makanisa,ni wazi kuwa serikali inajua,ni kwanini hawachukuliwi hatua? Hapa nchini kuna NGO's,/mashirika mengi tofauti ambayo yanatambulika ni kwaajili ya kutoa misaada mbalimbali kwa jamii, lakini baadhi yao yamegundulika yanaharibu maadili yetu hasa kwa watoto na vijana,lakini bado yapo, serikali ipo pia.Jiulize ingekuwaje kama mwananchi/wananchi wa kawaida tu,wakutwe na sifa hizo,tungesikia na kuona kwenye vyombo vya habari wakisindikizwa kwa mitutu.Naweza kufananisha hili na maigizo ya serikali ya Congo dhidi ya kikundi/vikundi vya waasi.

Hivi ni kweli DRC inahitaji msaada wa kijeshi toka nje pamoja na jeshi la UN dhidi ya watu wasio wasofika laki moja [maximum]ambao wangeweza kuwasambaratisha bila hata kuwafuata msituni?

Ni maigizo... Maana yangu ni kuwa, hivi vitu havipo kwa bahati mbaya,ni mipango inayo ratibiwa na,amlaka [isiyotaka kujulikana]yenye nguvu sana nyuma yake,watawala wetu wanajua na hawawezi kupingana nayo,iwe kwa zuri au baya, linahitaji viongozi aina ya JP Magufuli[kwa tahadhari sana].

Hata hivyo,haya hayana budi kutokea kwasababu yalishatabiriwa kuwapo kwa nyakati za mwisho wa dunia kwamba watatokea, manabii wa uongo ila tutawajua kwa matendo yao, lakini kwasababu ya uvivu wa kusoma vitabu/Biblia,watu hawana,maarifa ya kulinganisha/kutofautisha huduma na miujiza aliyoifanya YESU KRISTO dhidi ya hii inayofanywa na hawa mawakala wa Shetani/Ibilisi.
 
Kumbe ndio maana wayahudi wakampotezea Yesu kisa waliona huyu dogo fundi seremala tu
 
WATU wanapenda sana miujiza. Huyu sijui ndo yuko times fm anafoka saa zote!
kumna shost angu anakwambia kanunua mafuta ya 5000 kwa kuhani musa alivyopaka mbaya wake akampigia simu kumwambia yeye ndo anamroga! Anakwambia mama ake mdogo kayanunua ya laki moja ananiambia hayo ndo kiboko! Nikamjibu haya
 
Watanzania tunaangamia kwa kukosa maarifa

Why unaamini huyo tapeli?
 
Yani mjinga mmoja kajipeleka kwa ridhaa yake unakuja kushutumu watu humu
 
saa ngap mkuu wanaanza namimi nirefresh mind baada ya kusikiliza michezo
 
mkuu shikamoo
 
Kwani we ni mchawi hadi umuogope nabii anatishia nguvu zako.
Kama wanatoa kwa hiari Yao na pesa zao wewe shida Nini? Mbona kwa waganga wanatoa zaidi ya hizo.
Unayapimaje mafundisho kuwa ni ya kweli au uongo.
Kama avunji Sheria ya nchi hana kosa
 
Kuna jamaa wa karibu namjua amemchomoa milioni 2 .
Kumwambia kamtoa kitu tumboni akamwambia bado 2 kalete milioni 2 uje nimalizie kuvitoa.
Ka shida alokuwa nayo ikabidi akachukue bank akampa vikatolewa.
 
Serikali iko kimya,inajuwa wananchi wake mazoba na imeachqna nao wapigwe tu

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…