DOKEZO Serikali chukueni hatua za haraka dhidi ya Nabii Dominiki "Kiboko ya Wachawi"

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Sasa huyo Nabii simngemkamata na kumpeleka Polisi afunguliwe mashitaka?
Sasa huyo mchangiaji anapinga kwamba serikali haipaswi kumkamata maana kuna uhuru wa kuabudu!! Na kwamba kila mtu ana uhuru wa kuamini anachotaka. Sasa sielewi toka lini utapeli wa pesa ni uhuru wa kuabudu?
 
Jamaa anashirikina na mtu anitwa furaha Dominic kutapeli wanawake
 
Acha watapeliwe haya mawanawake hayataki kufanya kazi yana penda bwerereee, tapeli baba hadi wakimbie wenyewe.. fungua matawi nchi nzima..., funga betting machine hapo, wakati wanakusubiria hapo nje wana beti kwa kwenda mbele, funga mchine za kutabiri mechi utavuna mashabiki wa Yanga/Simba +Azam with Ihefu, fungua bar ndani ya kanisa lako, wasiliana na Dr. Sulle afungue tawi, bila kumsahau Ustadh majini.
 
Nawasalimu wote kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania​

Utangulizi
Mimi ni raia wa Tanzania, Mkristo kwa imani. Lakini nasikitishwa na kile kinachoendelea katika huduma ya Nabii wa Uongo anayejiita “Nabii Dominiki, Kiboko ya Wachawi”, mwenye Huduma yake DSM, WILAYA YA TEMEKE, BUZA – MTAA WA LULENGE. Kwa bahati mbaya Serikali ya Tanzania imekuwa kimya, bila kuchukua hatua zozote dhidi ya huduma hii potofu. Je, serikali inasubiri yatokee maafa kama ya Kibwetere (Uganda) au Mchungaji Makenzie (Kenya) ndipo ishtuke? Kwa uchache tutaorodhesha yale yahusuyo huduma hii potofu (CULT):

B. Upotofu wa Huduma ya Nabii Dominiki

- Matangazo ya Uongo Redioni

Nabii Dominiki amerubuni kituo kimoja cha redio hapa Dar es Salaam kinachorusha SHUHUDA ZA UONGO, muda wa Usiku na kupotosha kuwa zipo familia zinatuhumiana kwa mambo ya uchawi (Kinyume na Maadili ya Watanzania). Redio hiyo hurusha Vipindi na kujifanya wanawahoji mashuhuda LIVE, na kumbe siyo kweli. Kupitia njia hii, mtu huyu anazidi kujijengea umaarufu na kupata watu wengi (waislamu kwa Wakristo) wenye shida za kuuguliwa au kufiwa na ndugu zao kwa matarajio kuwa watarudishiwa AFYA / UHAI pindi wakikutana na huyu Nabii feki, lakini kumbe siyo kweli.

- Wizi Ulio Wazi wa Ada za Viingilio
Katika eneo analofanyia hii huduma (Buza kwa Lulenge), ameweka raia wenzake wa nchi jirani ya DR-Congo kukusanya pesa za viingilio vya kumuona. Hadi mwezi Januari 2024, kiingilio cha kuonana naye ofisini kilikuwa Tsh. 200,000/- (Laki mbili) bila RISITI wala kuandikishwa majina yako kuonesha malipo uliyotoa. Changamoto ni kuwa, endapo nabii atachelewa kuja ofisini, au ukipatwa na dharura, pesa hii huwezi kuidai. Kwa sasa (Aprili 2024) zipo fununu kuwa kiwango cha Ada ya Kiingilio kimeongezeka zaidi ya Tsh. laki mbili (>200,000/=).

- Masharti magumu baada ya Kumuona Ofisini kwake
Kwa wale wanaopata fursa ya kuonana naye uso kwa uso, ni lazima uandikishe JINA lako, na KAZI unayofanya. Lengo kuu ni kutaka kulinganisha UWEZO wako wa kutimiza masharti ya pesa utakayotajiwa pindi ukiingia ndani kukutana naye.

- Mafundisho ya Imani Potofu (Cultism) – Kinyume na Mafundisho ya Ukristo
Imani ya Ukristo inayohubiriwa mahali hapa ni tofauti na mafundisho mama ya Biblia,inayosema kama ni kipawa chochote kile cha miujiza, “mmepewa bure na hivyo toeni bure” (Mathayo 10:8). Kwa huyu Nabii endapo utaingia Ofisini kwake kumuona na kwa shida yako, atahakikisha ili kutatua shida yako anakupa sharti gumu ikiwemo Kiwango cha Pesa kinachoendana na kazi au biashara unayofanya.

C. Nini Kifanyike?
Pesa inayokusanywa mahali hapa BUZA - MTAA WA LULENGE ni nyingi na wizi wa wazi. Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) na TAKUKURU chukueni hatua, kufanya upelelezi wenu na kuwasweka ndani hawa Manabii Wahuni. Hii ni filimbi ya kuiamsha serikali (WHISTLE BLOWER), na Andiko hili litabaki kama kumbukumbu na ushahidi kwamba Vyombo vya Serikali vilitahadharishwa kabla kwa lengo zuri tu la kuchukua hatua stahiki.

=====

Pia soma:
Huyu naye ni tapeli kama matapeli wengine. Siku moja nilimsikia akiongea kwenye redio nikashangaa kwanini TCRA na serikali wanamruhusu aendelee kuwadanganya, kuwahadaa na kuwaibia fedha wananchi maskini kwa njia rahisi kama zile. Inasikitisha sana.
 
Huyu sasa ni fungakazi.
Upigaji wake sio wa kawaida.
Unaambiwa kalete lako 5, kalete milioni 2 n.k
Ukileta anakutoa vitu tumboni n.k
 
Mweee! Basi huyu ni sangoma anayetumia biblia kufanya ramli chonganishi na kuwatapeli wananchi masikini. Serikali inapaswa kuchukua hatua madhubuti kumdhibiti muhuni huyu kabla hajawaliza waanchi wengi sana. Huyu ni zaidi ya DECI aisee!
 
Nawasalimu wote kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania​

Utangulizi
Mimi ni raia wa Tanzania, Mkristo kwa imani. Lakini nasikitishwa na kile kinachoendelea katika huduma ya Nabii wa Uongo anayejiita “Nabii Dominiki, Kiboko ya Wachawi”, mwenye Huduma yake DSM, WILAYA YA TEMEKE, BUZA – MTAA WA LULENGE. Kwa bahati mbaya Serikali ya Tanzania imekuwa kimya, bila kuchukua hatua zozote dhidi ya huduma hii potofu. Je, serikali inasubiri yatokee maafa kama ya Kibwetere (Uganda) au Mchungaji Makenzie (Kenya) ndipo ishtuke? Kwa uchache tutaorodhesha yale yahusuyo huduma hii potofu (CULT):

B. Upotofu wa Huduma ya Nabii Dominiki

- Matangazo ya Uongo Redioni

Nabii Dominiki amerubuni kituo kimoja cha redio hapa Dar es Salaam kinachorusha SHUHUDA ZA UONGO, muda wa Usiku na kupotosha kuwa zipo familia zinatuhumiana kwa mambo ya uchawi (Kinyume na Maadili ya Watanzania). Redio hiyo hurusha Vipindi na kujifanya wanawahoji mashuhuda LIVE, na kumbe siyo kweli. Kupitia njia hii, mtu huyu anazidi kujijengea umaarufu na kupata watu wengi (waislamu kwa Wakristo) wenye shida za kuuguliwa au kufiwa na ndugu zao kwa matarajio kuwa watarudishiwa AFYA / UHAI pindi wakikutana na huyu Nabii feki, lakini kumbe siyo kweli.

- Wizi Ulio Wazi wa Ada za Viingilio
Katika eneo analofanyia hii huduma (Buza kwa Lulenge), ameweka raia wenzake wa nchi jirani ya DR-Congo kukusanya pesa za viingilio vya kumuona. Hadi mwezi Januari 2024, kiingilio cha kuonana naye ofisini kilikuwa Tsh. 200,000/- (Laki mbili) bila RISITI wala kuandikishwa majina yako kuonesha malipo uliyotoa. Changamoto ni kuwa, endapo nabii atachelewa kuja ofisini, au ukipatwa na dharura, pesa hii huwezi kuidai. Kwa sasa (Aprili 2024) zipo fununu kuwa kiwango cha Ada ya Kiingilio kimeongezeka zaidi ya Tsh. laki mbili (>200,000/=).

- Masharti magumu baada ya Kumuona Ofisini kwake
Kwa wale wanaopata fursa ya kuonana naye uso kwa uso, ni lazima uandikishe JINA lako, na KAZI unayofanya. Lengo kuu ni kutaka kulinganisha UWEZO wako wa kutimiza masharti ya pesa utakayotajiwa pindi ukiingia ndani kukutana naye.

- Mafundisho ya Imani Potofu (Cultism) – Kinyume na Mafundisho ya Ukristo
Imani ya Ukristo inayohubiriwa mahali hapa ni tofauti na mafundisho mama ya Biblia,inayosema kama ni kipawa chochote kile cha miujiza, “mmepewa bure na hivyo toeni bure” (Mathayo 10:8). Kwa huyu Nabii endapo utaingia Ofisini kwake kumuona na kwa shida yako, atahakikisha ili kutatua shida yako anakupa sharti gumu ikiwemo Kiwango cha Pesa kinachoendana na kazi au biashara unayofanya.

C. Nini Kifanyike?
Pesa inayokusanywa mahali hapa BUZA - MTAA WA LULENGE ni nyingi na wizi wa wazi. Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) na TAKUKURU chukueni hatua, kufanya upelelezi wenu na kuwasweka ndani hawa Manabii Wahuni. Hii ni filimbi ya kuiamsha serikali (WHISTLE BLOWER), na Andiko hili litabaki kama kumbukumbu na ushahidi kwamba Vyombo vya Serikali vilitahadharishwa kabla kwa lengo zuri tu la kuchukua hatua stahiki.

=====

Pia soma:
Wajinga siku zote ndiyo waliwao
 
Tanzania Inachezewa Sana Yaani Mtu Anafungua Huduma Anawakamua Wananchi Na Bado Wizara Ya Mambo Ya Ndani Ifute Kibari Cha Nabii Endapo Walimpa. Huu Mwendo Kwa Taifa Siyo Mzuri Yaani Kama Hatuoni.
... msiisumbue serikali, WIZARA YA MAMBO YA NDANI INAANZIA AKILINI MWENU ... PIGENI VITA UTUMBAFU!
 
Back
Top Bottom