DOKEZO Serikali chukueni hatua za haraka dhidi ya Nabii Dominiki "Kiboko ya Wachawi"

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Nawasalimu wote kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania​

Utangulizi
Mimi ni raia wa Tanzania, Mkristo kwa imani. Lakini nasikitishwa na kile kinachoendelea katika huduma ya Nabii wa Uongo anayejiita “Nabii Dominiki, Kiboko ya Wachawi”, mwenye Huduma yake DSM, WILAYA YA TEMEKE, BUZA – MTAA WA LULENGE. Kwa bahati mbaya Serikali ya Tanzania imekuwa kimya, bila kuchukua hatua zozote dhidi ya huduma hii potofu. Je, serikali inasubiri yatokee maafa kama ya Kibwetere (Uganda) au Mchungaji Makenzie (Kenya) ndipo ishtuke? Kwa uchache tutaorodhesha yale yahusuyo huduma hii potofu (CULT):

B. Upotofu wa Huduma ya Nabii Dominiki

- Matangazo ya Uongo Redioni

Nabii Dominiki amerubuni kituo kimoja cha redio hapa Dar es Salaam kinachorusha SHUHUDA ZA UONGO, muda wa Usiku na kupotosha kuwa zipo familia zinatuhumiana kwa mambo ya uchawi (Kinyume na Maadili ya Watanzania). Redio hiyo hurusha Vipindi na kujifanya wanawahoji mashuhuda LIVE, na kumbe siyo kweli. Kupitia njia hii, mtu huyu anazidi kujijengea umaarufu na kupata watu wengi (waislamu kwa Wakristo) wenye shida za kuuguliwa au kufiwa na ndugu zao kwa matarajio kuwa watarudishiwa AFYA / UHAI pindi wakikutana na huyu Nabii feki, lakini kumbe siyo kweli.

- Wizi Ulio Wazi wa Ada za Viingilio
Katika eneo analofanyia hii huduma (Buza kwa Lulenge), ameweka raia wenzake wa nchi jirani ya DR-Congo kukusanya pesa za viingilio vya kumuona. Hadi mwezi Januari 2024, kiingilio cha kuonana naye ofisini kilikuwa Tsh. 200,000/- (Laki mbili) bila RISITI wala kuandikishwa majina yako kuonesha malipo uliyotoa. Changamoto ni kuwa, endapo nabii atachelewa kuja ofisini, au ukipatwa na dharura, pesa hii huwezi kuidai. Kwa sasa (Aprili 2024) zipo fununu kuwa kiwango cha Ada ya Kiingilio kimeongezeka zaidi ya Tsh. laki mbili (>200,000/=).

- Masharti magumu baada ya Kumuona Ofisini kwake
Kwa wale wanaopata fursa ya kuonana naye uso kwa uso, ni lazima uandikishe JINA lako, na KAZI unayofanya. Lengo kuu ni kutaka kulinganisha UWEZO wako wa kutimiza masharti ya pesa utakayotajiwa pindi ukiingia ndani kukutana naye.

- Mafundisho ya Imani Potofu (Cultism) – Kinyume na Mafundisho ya Ukristo
Imani ya Ukristo inayohubiriwa mahali hapa ni tofauti na mafundisho mama ya Biblia,inayosema kama ni kipawa chochote kile cha miujiza, “mmepewa bure na hivyo toeni bure” (Mathayo 10:8). Kwa huyu Nabii endapo utaingia Ofisini kwake kumuona na kwa shida yako, atahakikisha ili kutatua shida yako anakupa sharti gumu ikiwemo Kiwango cha Pesa kinachoendana na kazi au biashara unayofanya.

C. Nini Kifanyike?
Pesa inayokusanywa mahali hapa BUZA - MTAA WA LULENGE ni nyingi na wizi wa wazi. Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) na TAKUKURU chukueni hatua, kufanya upelelezi wenu na kuwasweka ndani hawa Manabii Wahuni. Hii ni filimbi ya kuiamsha serikali (WHISTLE BLOWER), na Andiko hili litabaki kama kumbukumbu na ushahidi kwamba Vyombo vya Serikali vilitahadharishwa kabla kwa lengo zuri tu la kuchukua hatua stahiki.

=====

Pia soma:
Huyu jamaa tapeli kubwa nipo kumsikiliza hapa.
 
Nimekuja kujua kumbe huyu jamaa ni mkongo.

Ma'body guards wake ni kina Mwarabu fighter
 
Dini ni kwa ajili ya wajinga wasioweza kuchaganua mambo. Hivyo, wacha wapigwe tu.

Kama watu wazima mnashindwa kubaini uongo na ukweli ulio dhahiri.. mnachukulia mambo ya kusadikika serious, tutawezaje kusaidia?
 
Huyu tapeli naona serikali bado inamuendekeza mama zetu na dada zetu wanazidi kutapeliwa.
 
Mtumishi yeyote feki neno la Mungu kwenye ibada linafundishwa kidogo sana au hakuna kabisa. Huyu sio mtumishi wa Mungu.
 
Nabii anatembea na mabaunsa wakina mwarabu fighter
 
20240707_042400.jpg
20240707_042400.jpg
 
Nawasalimu wote kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania​

Utangulizi
Mimi ni raia wa Tanzania, Mkristo kwa imani. Lakini nasikitishwa na kile kinachoendelea katika huduma ya Nabii wa Uongo anayejiita “Nabii Dominiki, Kiboko ya Wachawi”, mwenye Huduma yake DSM, WILAYA YA TEMEKE, BUZA – MTAA WA LULENGE. Kwa bahati mbaya Serikali ya Tanzania imekuwa kimya, bila kuchukua hatua zozote dhidi ya huduma hii potofu. Je, serikali inasubiri yatokee maafa kama ya Kibwetere (Uganda) au Mchungaji Makenzie (Kenya) ndipo ishtuke? Kwa uchache tutaorodhesha yale yahusuyo huduma hii potofu (CULT):

B. Upotofu wa Huduma ya Nabii Dominiki

- Matangazo ya Uongo Redioni

Nabii Dominiki amerubuni kituo kimoja cha redio hapa Dar es Salaam kinachorusha SHUHUDA ZA UONGO, muda wa Usiku na kupotosha kuwa zipo familia zinatuhumiana kwa mambo ya uchawi (Kinyume na Maadili ya Watanzania). Redio hiyo hurusha Vipindi na kujifanya wanawahoji mashuhuda LIVE, na kumbe siyo kweli. Kupitia njia hii, mtu huyu anazidi kujijengea umaarufu na kupata watu wengi (waislamu kwa Wakristo) wenye shida za kuuguliwa au kufiwa na ndugu zao kwa matarajio kuwa watarudishiwa AFYA / UHAI pindi wakikutana na huyu Nabii feki, lakini kumbe siyo kweli.

- Wizi Ulio Wazi wa Ada za Viingilio
Katika eneo analofanyia hii huduma (Buza kwa Lulenge), ameweka raia wenzake wa nchi jirani ya DR-Congo kukusanya pesa za viingilio vya kumuona. Hadi mwezi Januari 2024, kiingilio cha kuonana naye ofisini kilikuwa Tsh. 200,000/- (Laki mbili) bila RISITI wala kuandikishwa majina yako kuonesha malipo uliyotoa. Changamoto ni kuwa, endapo nabii atachelewa kuja ofisini, au ukipatwa na dharura, pesa hii huwezi kuidai. Kwa sasa (Aprili 2024) zipo fununu kuwa kiwango cha Ada ya Kiingilio kimeongezeka zaidi ya Tsh. laki mbili (>200,000/=).

- Masharti magumu baada ya Kumuona Ofisini kwake
Kwa wale wanaopata fursa ya kuonana naye uso kwa uso, ni lazima uandikishe JINA lako, na KAZI unayofanya. Lengo kuu ni kutaka kulinganisha UWEZO wako wa kutimiza masharti ya pesa utakayotajiwa pindi ukiingia ndani kukutana naye.

- Mafundisho ya Imani Potofu (Cultism) – Kinyume na Mafundisho ya Ukristo
Imani ya Ukristo inayohubiriwa mahali hapa ni tofauti na mafundisho mama ya Biblia,inayosema kama ni kipawa chochote kile cha miujiza, “mmepewa bure na hivyo toeni bure” (Mathayo 10:8). Kwa huyu Nabii endapo utaingia Ofisini kwake kumuona na kwa shida yako, atahakikisha ili kutatua shida yako anakupa sharti gumu ikiwemo Kiwango cha Pesa kinachoendana na kazi au biashara unayofanya.

C. Nini Kifanyike?
Pesa inayokusanywa mahali hapa BUZA - MTAA WA LULENGE ni nyingi na wizi wa wazi. Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) na TAKUKURU chukueni hatua, kufanya upelelezi wenu na kuwasweka ndani hawa Manabii Wahuni. Hii ni filimbi ya kuiamsha serikali (WHISTLE BLOWER), na Andiko hili litabaki kama kumbukumbu na ushahidi kwamba Vyombo vya Serikali vilitahadharishwa kabla kwa lengo zuri tu la kuchukua hatua stahiki.

=====

Pia soma:
Sheia zinazohusiana na masuala ya dini na imani zimekaaje jina lake lenyew limekaa kiubabaoshaji
 
Usihusishe serikali na vitu vya kipumbavu kila mtu amepewa akili hapo inategemea unaitumiaje akili uliyopewa,wanaoenda huko wameenda kwa ridhaa zao wenyewe wacha tu wapigwe
Inaonekana hata maana ya serikali huijui unajiropokea.
 
Hivi kwanin wanawake wengi wa kiafrica hasa Tanzania uwezo binafs wa kufikiri uko chini mno hivi!
Aliyesoma na mbumbumbu wote sawa tu!
Mbaya zaidi ndo wamepewa jukumu la kuendeleza kizazi.
Ukute ndo maana wazungu walichoka ujinga wakaoana wanaume.
Wengi hawaamini mambo hutokea kiasilia na hukabiliwa kwa kanuni za logic kikawaida.
Wanapenda mkato wa miujiza iwe kwa mganga au dini.
Elimu ya kujitambua wanayo ya mapenzi tu.
NItashangaa kukuta aliyeishi na mke dunian hapatikan ahera!
 
Huu uzi niliuignore ila baada ya kuona hadi Laurence Masha kaenda huko buza mhhhh
 
Hivi kwanin wanawake wengi wa kiafrica hasa Tanzania uwezo binafs wa kufikiri uko chini mno hivi!
Aliyesoma na mbumbumbu wote sawa tu!
Mbaya zaidi ndo wamepewa jukumu la kuendeleza kizazi.
Ukute ndo maana wazungu walichoka ujinga wakaoana wanaume.
Wengi hawaamini mambo hutokea kiasilia na hukabiliwa kwa kanuni za logic kikawaida.
Wanapenda mkato wa miujiza iwe kwa mganga au dini.
Elimu ya kujitambua wanayo ya mapenzi tu.
NItashangaa kukuta aliyeishi na mke dunian hapatikan ahera!
Wao ndio hawana akili kuliko hata wanyama thus wanaowana jinsia moja
 
Back
Top Bottom