DOKEZO Serikali chukueni hatua za haraka kudhibiti wimbi la wahamiaji haramu hasa Wamalawi

DOKEZO Serikali chukueni hatua za haraka kudhibiti wimbi la wahamiaji haramu hasa Wamalawi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Tutabanana humu humu hakuna Cha kwenda wapi Wala wapi, tushawajua wanufaika wa wahamiaji haramu!.
Unataka nikatoe taarifa huko ili mnifanye Nini? Hujui hicho ni kimradi Cha watu?


Hizo ni imani potofu na uwoga wa bure tu.
 
Bora ungeongelea Wachina, hawa ndo kupe
Wote hao the same! Acheni kutetea uvunjifu wa Sheria za nchi, kama wameingia kinyume na Sheria ni kosa, haijaiishi Hawa wapole sijui wale wakorofi. Sheria na huruma ni vitu viwili tofauti
 
Acha roho mbaya, nchi yenu inanini cha maana ukatae watu waafrika wenzio? Unahisi serikali haijui? Unajua Watanzania wangapi wapo malawi kama hivi hivi?
 
Acha watu watafute maisha kijana. Kama wewe umeridhika na life la bongo ni wewe. Siamini kwamba wamalawi au the so called wahamiaji haramu ndo wanafanya maisha yako yawe magumu bongo. Ukiuliza wabongo ambao wameenda huko mambelezz kutafuta maisha. The story is the same or worse. Mimi naamini kila binadamu apewe fursa atafute maisha. Ilmradi ni raia mwema.

Na mara nyingi ukiangalia, the so called wahamiaji ndo wanachapa kazi maana wanajua wanatafuta nini. Sisi wabongo ni kulalamika tu. Itumie hii kama fursa. Hata kama ungefukuza wamalawi wote siamini kama itabadilisha maisha yako. Pambana kiume. Acha wamalawi watafute maisha. Life is tough bro!

Tabia za kimbea mbea tu, Mwanaume unaona wivu mwanaume mwenzio akija kwenye nchi yenu kufanya kazi za ajabu? Kwani Watanzania wangapi wapo Zambia au Malawi[emoji706] Jamaa alichofanya ni umbea na ni aibu kwa Mwanaume kama ni Mwanaume
 
Wameona fursa acha wajitafutie maisha yao, hiyo mipaka yenyewe isiyoeleweka mmewekewa na wakoloni, wahamiaji mara nyingi ni wachapa kazi na umesema mwenyewe ni walinzi, naamini uliyosema kuhusu mbususu au wezi ni chai tuu, acheni chuki kwa waafrica wenzenu
 
Wanakuja na Achimwene hao kutoka Mbeya..Bongo kama New york mkuu..sisi tunaona bongo miyeyusho lakini kuna nchi vijana wakikaa maskani wanaota kuja Bongo..hasa hapo mjini Daslam...🤣
Kichekesho mi Mmalawi kabisa,babu mzaa dingi alizamia bongo kitambo tu kakutana kidosho cha kinyaki toka ukoo kichief Tokyo huko hao wakatoroka wakaenda kuanzisha makazi yao mahali.
Bibi nae siku kaniweka kitako kunipa history.
Kumbe na yeye bibi yake katoka Ethiopia huko, alikuja mambo ya vita huko na mumewe kakimbilia moro kashia kule njombe ndani ndani.
Kaolewa na huyu chief Nyanya wangu.
Kwahiyo hakuna haja kujadili race ya mtu, as long si Waafrica tusaidiane tu.
Hao watu wanajaribu tu kustrugle.
Mikocheni na msasani tulikua nao kitambo tu mtaani walikua wamejaa haswa
hatujawai hata kuwauliza chochote.
Sasa we mtu akipigana miti huko ndani kwake inakuhusu nini?
Mwenyewe tukiangalia history yake utakuta katoka burundi au Kenya.
Tuache hayo mambo uracist.
 
Tabia za kimbea mbea tu, Mwanaume unaona wivu mwanaume mwenzio akija kwenye nchi yenu kufanya kazi za ajabu? Kwani Watanzania wangapi wapo Zambia au Malawi[emoji706] Jamaa alichofanya ni umbea na ni aibu kwa Mwanaume kama ni Mwanaume
Una elimu duni Sana ndugu!! Kwa kifupi pole!!
 
Back
Top Bottom