DOKEZO Serikali chukueni hatua za haraka kudhibiti wimbi la wahamiaji haramu hasa Wamalawi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kama umekiona wewe ukaja kutusimulia kwanini hutaki na sisi tusimulie yetu,
Mkuu tafuta pesa , tafuta pesa, tafuta maisha wacha kupiga chabo wamalawi wakizagamuana ohoo...!!
 
Una amini TISS ipo?
Ingekuwepo Mhutu asingekuwa Numero Uno
 
We umenielewa! Kama wamekuja kutafuta maisha ni jambo zuri lkn kutuletea vitamaduni vya kwao huko hapana aisee
Wale jamaa tabia zao Huwa zinashangaza sana nahisi wakat mwingine kama nati zimelegea.

Kuna siku tuko nyomi la watu tumekaa kwenye kiwanja Cha mwananyamala kwa kopa kulikuwa na game ya kimashindano ya kimtaa sasa tumeuzunguka ule uwanja wote ila Kuna barabara Huwa inapita ndani ya uwanja,

Game ikiwa katikat wakawa wanapita wanyasa wakiume na wa kike kama 6 hivi Cha ajabu wakawa wamesimama ndani kabisa ya kiwanja wanapiga story yaan as if hawaelew ni nini kinaendelea mule kiwanjani ghafra bin vuu mpira ukawa unaelekea upande wao wamesimama tu wachezaji walipofika karibu katka kugombea mpira SI wakawavaa basi wote chini uwanja mzima unacheka.
 
Uzuli wa hawa watu kibarua kazi wasizo zitaka wabongo au kuzifanya kwa bei kuwa wao ukusanyika na kufanya kazi hizo kwa malipo nafuu wengi wao wamejazana kwenye makampuni ya ulinzi
Aibu haijawahi kushibisha tumbo
 
Yaani jamaa umeamua kuwaita watanzania wenzako wamalawi
 

Iko hivi labda mleta maada hujawahi kutoka au kwenda kuishi inje ya Tanzania,kwangu mimi hicho ni kitu cha kawaida,hata Viongozi wanajua,yaani wananchi wa kawaida kwenda kutafuta maisha kwenye ichi nyingine,na hii inategemeana na nguvu ya uchumi wa ichi husika

Mfano kipindi nafika Malawi miaka ya 1998 nilikuta watanzania ni wengi sana,tena asilimia kubwa walikuwa wa kutoka Mbeya,mpaka wamalawi walikuwa wanajua labda lugha ya Taifa ya Tanzania ni kinyakyusa.

Miaka ilivyoenda hawa watanzania wakawa wana Mahotel yao na mtandao mkubwa Lilongwe katika mtaa mmoja wa Devil street,kiasi kwamba ulikuwa ukifika mgeni,unazani kwamba uko mbeye au Tanzania

Kwa Mozambique watanzania wamejaa, baadhi ya sehemu kama machimboni,kiasi kwamba lugha inayotumika ni kiswahili na hela wanayotumia ni shilingi ya Tanzania ndani ya Mozambique

Sema kilichotofautiana ni ukubwa wa uchumi wa Tanzania kwa hizi inchi,kiasi kwamba hutakuja kuwaona watanzania kwenye hizi ichi wakifanya kazi za ulinzi,bali asilimi kubwa wako kibiashara
 
Waacheni wamalawi ndugu zetu ....miaka nyuma sisi tulienda sana sana lilongwe mzuzu etc kufanya biashara sasa uchumi wetu mzuri waache nao wafanya kazi ....wasife njaa
....
 
Acha chuki kijana. Wamalawi hawana tatizo na mtu ni shida tu zinawakimbiza huko kwao. Wewe mwenyewe kwa uandishi wako wa hovyo utakuwa mrundi ila watu wamekukaushia. Waache wajitafutie maisha. Unadhani vyombo vya usalama vimelala? Ni kwamba hata wao wana utu na kujua Malawi mambo kwa sasa ni magumu mbo hasa baada ya mafuriko. MLETA UZI UNA VIASHIRIA VYA USHIRIKINA
 
Wewe kweli hamnazo sasa ndo umeandika Nini? Hebu ludia tena kusoma ulichokiandika uone ni jinsi gani ulivyo mjinga
 
Waacheni wamalawi ndugu zetu ....miaka nyuma sisi tulienda sana sana lilongwe mzuzu etc kufanya biashara sasa uchumi wetu mzuri waache nao wafanya kazi ....wasife njaa
....
Kweli kazi wafanye lkn uhalifu na matendo ambayo yapo kinyume na mira,desturi zetu hapana aisee
 
Halafu wepesi kujifunza kiswahili hao. Yaani wakishakaa miezi 6 tu wanaongea fluent Swahili. Sema wanakuwa na ka lafudhi Kama watu wa Mbozi. Sio rahisi kuwatofautisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…