Inside10
Platinum Member
- May 20, 2011
- 34,776
- 42,933
Kutoka kwa Prof. Kitila akiwa bungeni muda huu amesema,
Hadi kufikia Machi 2025, deni la Taifa lilifikia Sh107.7 trilioni kutoka Sh91.7 trilioni katika kipindi kama hicho mwaka 2024 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 14.9.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo ameyasema hayo leo Juni 12, 2025 wakati akiwasilisha bungeni taarifa ya hali ya uchumi kwa mwaka 2024 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2025/2026.
Profesa Mkumbo amesema kati ya kiasi hicho deni la ndani lilikuwa Sh34.76 trilioni pekee.
“Ongezeko la deni lilitokana na Serikali kuendelea kupokea mikopo mipya kutoka vyanzo mbalimbali kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, reli, viwanja vya ndege, umeme na maji,” amesema.