Dr wa Manesi
JF-Expert Member
- Aug 19, 2024
- 6,479
- 4,974
Sipendezwi abadan na vitendo vinavyoashiria dharau kwa mahakama, serikali na nchi kwa ujumla vinavyoonyeshwa na baadhi ya watuhumiwa wawapo au waendapo mahakamani. Nitatoa mifano michache:
1. Nilishuhudia mmoja ya wale watuhumiwa waliotumwa kumbaka kwa kumrawiti na kumrekodi yule dada wa nyumbani akicheza muziki kwa kuchekesha kichwa bila wasiwasi wowote Huku akitabasamu kuashiria dharau. Mwingine akiwa anapelekwa kwenye ukumbi alionekana akimtisha mwandishi (mpigapicha) kwa kumuonyesha kidole na utoaji wa maneno kadhaa. Yaani umebaka, upo mahakamani Bado huonyeshi kujuta?!!!!
2. Wale waliofuja bilioni 6 wanaonekana wanatabasamu tu Kila wanapopelekwa mahakamani, tena wengine wamevalia kofia za kibongoman kabisa. Hii inanitia hasira sana Mimi kama mwananchi mzalendo kabisa wa nchi hii.
3. Kuna hawa matahira wengine ambao wakifika mahakamani kazi yao ni kunyoshanyosha vidole tu juu kama wanaocheza taarabu ya Hadija Kopa. Hii ni dharau kubwa sana kwa mahakama na serikali.
Athari ya haya;
Kubwa ni kwamba inapelekea uhamasishaji wa vitendo vya kiharifu.
Mapendekezo yangu:
1. Kuwe na sare maalum kwa mtuhumiwa yeyote yule aendaye mahakamani kujibu kesi. Hii ya Kila mtu kujivalia kivyake.
2. Kuwe na adhabu Kali ya papo kwa papo kwa mtuhumiwa yeyote atakayeonyesha vitendo vya utovu wa nidhamu. Kutosha, kucheka, kucheza na unyooshaji wa vidole juu naomba vichukuliwe kuwa ni utovu mkubwa wa nidhamu.
Nawasilisha nikiwa sifahamu chochote kuhusu Sheria.....🙏🙏🙏