Serikali fungeni shule na vyuo kuokoa maisha

Haya yote hayasaidii kwani nchi za wenzetu hawakufanya haya??? Korona imepungua??? Tuache kutishana bure kama ni kufa utakufa tu sio kwa korona hata malaria yatakuua tu! Tuache kujitoa ufahamu
 
Kufunga shule haitasaidia kitu, maana bado mishe mishe za maisha zitabaki vile vile. Napendekeza, barakoa kila mahali, kusiwe na mikusanyiko yoyote, daladala hakuna kusimamisha abiria, watu wapeane distance wanapopata huduma kama za kibenki.
Benki zile alama za viatu si zipo ila watu hawahangaiki nazo sikuhizi
 
Kufunga shule ili iweje. Serikali itoe chanjo bac. Ianze na watoa huduma za afya, iende kwa wazee, then vijana na imalizie na waatoto.
 
Comment ya kijinga tokea Tanzania ipate uhuru
 
Hivi umewahi kuwaza sisi wa Manzese, Kwa Mtogole, Mpitimbi, na Nyakanazi watoto wakiwa shule ndiyo wanakuwa salama zaidi kuliko nyumbqni?

Ni watanzania wangapi wanaweza kuwazuia watto wao wasichanganyijane na wengine?
 
Namba 2 TRA hawajaiona? Chanzo cha mapato hicho
 
... watabaki mayatima wengi sana! Serikali itawahudumia? Shule zifungwe kwa muda sote (wazazi na watoto) tuwe salama au nchi ibaki na maelfu ya mayatima? Au unawaza usawa wa pua?
 
Unawezafikiri unawaza jema kuhusu kufunga shule, Kenya walifunga shule toka mwaka Jana kaulize madhara yake kwa taifa. Inawezekana wewe ni mfanyakazi wa serikali unayekula pesa yetu, hebu jaribu kuwafikiria na ndugu zako wanaoishi kupitia hizi shule mwisho wao utakuwa nini.

Kungekuwa na uwezekano raisi afunge shule lakini pia asimamishe mishahara yenu mpaka shule zitakapofunguliwa ili tuzungumze lugha moja huku mtaani. We are too selfish. Mwacheni raisi wetu ana mengi ya kufikiri juu ya taifa hili.

Na nyinyi walinzi tunaomba mumlinda sana raisi wetu maana kuna watu wakisikia anaumwa hata Mafua watashangilia sana.
 
Huu ugonjwa itabidi watu wawe tayari kufa, kufa na kufa tena maana tunaona wateule wa Jiwe wanaona aibu kuvaa barakoa huku wakiwa wengi ni wazee wenye kisukari,pressure & ukimwi
 
Ila jamaa kasema kwa mwezi mmoja kama umemsoma vema, nafikiri ili kujipanga.
 
Kwa nini wote mna ushauri wa kukurupuka.
Kufunga shule wengi wataumia.

Hapa walete chanjo. Wazee na watu wa afya wapigwe chanjo
Chanjo ipo na ishaanza kutumika.

Upumbavu wa meko ni mzigo.
Mutant ya sA inatakiwa impige maana kawa kama farao
 
Hao wachache wakiwa sucriface kwa ajili ya kuokoa Taifa au wengi sio tatizo,acha ubinafsi wa kijinga.

By the way ni wajibu wa serikali kuangalia Hali zao na kusaidia
 
Mkuu kwa upanda wangu shuluisho hapa siyo kufunga shule na vyuo,
Sema serikali iweke mikakati dhabiti ya kuandaa mazgr. kwa kila taasisi kuwa na tahadhiri effectively
Kwa maana wizara ya Afya watoe semina na mafunzo namna gani wanavyo weza kupamvana na viral disease
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…