Serikali fungueni mipaka wakulima wauze wenyewe mahindi, NFRA inawanufaisha wachache

Serikali fungueni mipaka wakulima wauze wenyewe mahindi, NFRA inawanufaisha wachache

Daa umenikumbusha mbali sana,nilishawahi kupeleka mahindi NFRA nilijuta na sitasahau na sitarudia tena,nilipoteza pesa nyingi,hao wenyevitengo bila ya rushwa lazima utasumbuka,mara chekecha mahindi,mara moisture yani ilimradi tu wakulegeze uwatoe,waliokwisha tengeneza mifumo utawaona wanapeta tu!
Ukweli ni kwamba NFRA inawasaidia wafanyabiashara wakubwa sio wakulima.
Pole mkuu ila usikate tamaa
 
Acha kuigombanisha Serikali ya awamu ya Sita Na wakulima Mkuu, mipaka Iko wazi,ule Ubabe wa kipumbavu wa kutunishiana misuli na majirani uliisha April
 
Sirikali ya wapiga dili iko kazini. Huko manyoni wanagombea mashamba ya kulima korosho. Mashamba yote pembezoni ni ya vigogo kuanzia PM na hata mama.

Huko Chamwino watu hao hao wanagombea viwanja. Ukiende njia ya kondoa toka dom town watu walewale wanagombea mashamba. Huu ulafi ni hatari.
 
Acha kuigombanisha Serikali ya awamu ya Sita Na wakulima Mkuu, mipaka Iko wazi,ule Ubabe wa kipumbavu wa kutunishiana misuli na majirani uliisha April
We pimbi tu kama iko wazi hayo mahindi mbona serkali inayanunua kupitia NFRA! Basi wapeleke nchi jirani si mnajidai mmeboresha mahusisno lakini vichwani empty!
 
Sirikali ya wapiga dili iko kazini. Huko manyoni wanagombea mashamba ya kulima korosho. Mashamba yote pembezoni ni ya vigogo kuanzia PM na hata mama. Huko chamwino watu hao hao wanagombea viwanja. Ukiende njia ya kondoa toka dom town watu walewale wanagombea mashamba. Huu ulafi ni hatari.
Sasa braza Kama wewe hulimi.wenzako wanawekeza kwenye kilimo tatizo liko wapi?

Mimi nahimiza wenye pesa wawekeze kwenye kilimo ili kilimo kikue
 
Baada ya kusikia serikali imetoa bilioni 50 kwa ajili ya manunuzi ya mahindi.

Nikaona huu ndio wakati muafaka wa kuuza nikajaza howo zangu tatu mzigo kupeleka kwenye kitengo.

Dah nilichokutana nacho tajiri atabaki kuwa tajiri nae maskini atazidi kuwa maskini hasa kwenye nchi zetu za Kiafrika.

Kiufupi mkulima mdogo hauzi wanaopewa kipaombele mwenye junia kuanzia mia nashukuru nilibeba tu gunia 412 nikajiuzia si unajua ukiwa na jina hapa nchini.

Sikuwa mbinafsi nikamfuata mkulima mdogo aliebeba gunia 30 nikaanza piganae stori akaniambia anasiku ya nne na kila akitaka uza vikwanzo kibao mara maind machafu.

Mara punje ndogo kiujumla ni vikwazo tu ambavyo havina msingi

Nikarudi kwa katajili kenzangu ambako nako kalileta maindi akaniambia kaka huu ndio muda wa kupiga pesa.

Akiwa na maana anaenda walalia wakulima wadogo kwa kilo 260 unapeleka kwenye kitengo 500.

Sikujibu kitu nilichokifanya nikaenda kwa yule mkulima nikamkusanya na wenzake nikaenda wauzia asee walinishukuru.

Tuludi kwenye mada
Kwenu watu wa serikali nimewapa hiyi stoli ili mjionee hela mliyotoa haina msaada wala tija na mpate pakuanzia

Ila kama haya yana mkono wenu endeleen kuwaumiza wananchi kwa ufinyu wa akili zenu

Mngekuwa mnataka kumsaidia mwananchi haya tusingeyaona

Ila ipo siku yenu na mm ndio yule mtu aliekuwa akisubiliwa najua hamuwez kuelewa wala kusikia wala kuambiwa
Muda unakujaa

Asante
Mahindi yatapanda bei sana hivi karibuni...mwakani hali ni mbaya...kuuza kwa 50000 bado ni hasara kubwa. Kama una ghala wewe hifadhi. Ukame ushaanza Kenya...
 
Poleni wakulima wa Mahindi wa Tanzania.

Mwaka huu nasikia kuna makampuni yananunua Soya kupeleka katika Soko la China.

Ulizieni hayo makampuni yanapatikana wapi ili mlime soya na kuyauzia.

Mimi nilishaachana na biashara ya Mahindi.

Kitambo sana.

Biashara ya kuteseka kulima bila kujua unauza wapi.
Soya ipi mkuu
 
Back
Top Bottom