Serikali haikagui vyakula, kipi kinawazuia wenye migahawa kupika mizoga, mchele wa plastiki, viungo expired, mafuta ya transfoma / nguruwe, n.k

Ni ngumu japo hii nchi ni kubwa hivyo inawezekana.
Kuwezekana inawezekana maana wapo wanaofanya haya mambo, kukiwa na chombo watakamatwa tu.

ila kwa sasa umewahi kusikia wapi kuna kesi mahakamani ya mwenye mgahawa au mama ntilie anaefanya haya mambo ?
 
Reactions: Tsh
Wachache wenye utu wanafata miongozo ya upishi bora
 
Kuwezekana inawezekana maana wapo wanaofanya haya mambo, kukiwa na chombo watakamatwa tu.

ila kwa sasa umewahi kusikia wapi kuna kesi mahakamani ya mwenye mgahawa au mama ntilie anaefanya haya mambo ?
Swali ni umewahi kushuhudia uwepo wao?
 
Swali ni umewahi kushuhudia uwepo wao?
wewe labda unakaa sana ndani hupendi hata kuchangamana na watu, haya mambo kipya kipi ? hebu uwe unatoka nje kidogo mkuu, utafia humo ndani watu wasijue 😂😂
 
Reactions: Tsh
Mkuu ukisema ufuatilie hivi vitu huenda hata mkeo hapo Nyumbani Kuna uchakachuzi anaufanya pasi wewe kujua.
 
wewe labda unakaa sana ndani hupendi hata kuchangamana na watu, haya mambo kipya kipi ? hebu uwe unatoka nje kidogo mkuu, utafia humo ndani watu wasijue 😂😂
Hahaha. Okey mkuu.
Basi isaidie serikali kuwafichua hata kisiri siri. Usilee uovu.
 
Mafuta ya nguruwe mbona ni lishe nzuri? Labda mafuta ya transfoma ndio mabaya. Kuna msemo huko migahawani kama mchuzi le, wali ja, mchuzi ja wali le, yana unachanganyiwa chakula cha jana na chakula cha leo, ama mchuzi au wali. Wengi wanaokula migahawani ni watu ambao hawana ndoa, walioko kazini na wasafiri
 
Serikali tangu lini ilifanya biashara ya Mama ntilie?

Uliza hivyo wateja hautapata na automatic biashara itakushinda na kuchafua jina lako,
Hata uje Kupika vyakula halali na vizuri hautauza
Serikali tangu lini ilifanya biashara ya Mama ntilie?

Uliza hivyo wateja hautapata na automatic biashara itakushinda na kuchafua jina lako,
Hata uje Kupika vyakula halali na vizuri hautauza
Kuna mabwana afya na mabibi afya wa halmashauri ambao hufuatilia usafi na afya mitaani. Wamekuwa wakiingia migahawani kukagua usafi kwa wahudumu wa migahawa hiyo kama wako safi na mazingira ya kula ni masafi ikiwemo mavazi rasmi ya upishi. Kuhusu ubora wa chakula migahawani haijulikani kama wanachunguza vyakula vilivyoandaliwa kuliwa migahawani
 
Umekosea sana kumweka nguruwe kwenye hiyo tilte yako. Mkuu wa meza hachanganywi na mauchafu uliyotaja
 
Huwa Siwa elewi wanao kula vile vyakula vya dirishani wakiwa kwenye bus.
 
Kosa kubwa nikuiongezea majukumu TBS kuwa wakaguzi kazi iliyokuwa inafanywa na TFDA. TFDA wanaafadhali kuliko TBS
 
Hakuna wa kuwazuia, na ndo fursa za biashara hizo.

Cha kuwazuia ni mwili wako. Mwili wako ukipata shida kutokana na chakula cha kununua, basi utajua sehemu ya kutokula.

Ila katika ulivyotaja sio vyote vina madhara. Chakula cha jana hakina madhara, kitimoto hana madhara ni ujinga tu umewatawala watu,
 
A wake-up call for the responsible regulatory body (TBS) !!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…