Serikali haitabadili miaka ya Wanajeshi kuoa na kuolewa

Serikali haitabadili miaka ya Wanajeshi kuoa na kuolewa

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa (JKT) Dkt. Stragomena Tax, ameliambia Bunge kuwa kwa sasa utaratibu wa miaka 6 utabakia kama ulivyo kutokana na misingi iliyowekwa kwa ajili ya kuwaandaa Askari hao kulinda nchi.

Dkt. Stragomena amesema Askari wapya wanaojiunga na Jeshi wanabakia kuwa wapiganaji ambao hupaswa kupewa ujuzi zaidi na kutumika kwenye Vita, hivyo miaka 6 ya kutokuoa au kuolewa inatoa nafasi kwa Askari hao kutumika ipasavyo kwenye shughuli za kijeshi.
 
eb4f3784-56ce-4d64-8f1e-0c67cfbbc4b3.jpg
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb), leo Septemba 16, 2022 ametoa ufafanuzi Bungeni kuhusu utaratibu uliowekwa kwa askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wa kukaa miaka 6 bila kuoa ama kuolewa mara baada ya kujiunga na jeshi hilo.

Dkt. Stergomena Tax ameliambia Bunge kuwa kwa sasa utaratibu huo utabakia kama ulivyo kutokana na misingi iliyowekwa kwa ajili ya kuwaandaa askari hao kulinda nchi.

Dkt. Stergomena amesema askari wapya wanaojiunga na Jeshi wanahesabiwa kama wapiganaji ambao wanapaswa kupewa ujuzi zaidi mara baada ya kutoka Chuo cha Mafunzo ya awali (Recruit Training School) hivyo miaka 6 iliyowekwa ya kutokuoa ama kuolewa inatoa nafasi kwa askari hao kutumika katika shughuli za medani pamoja na Oparesheni za Kijeshi kulingana na mahitajio.

Amesema “Maafisa wenye elimu ya Darasa la 7 hadi Kidato cha 6 na wenye stashahada ndio wanakaa miaka 6. Wenye shahada ya kwanza wao miaka minne, shahada ya uzamili miaka mitatu, shahada ya uzamivu wao hawana muda.

“Hii ni kutokana na aina ya majukumu ambao askari hao huwa wanafanywa, katika kundi la kwanza wengi huwa ni vijana wadogo ambao wanahitaji muda wa kukomaa.”
 
Kwa hali hii wataendelea kubanduana mpaka basi! Yaani mnakuja kuoana mkiwa used mpaka basi.
 
Nawahurumia sana watoto wa kike, Hasa bachelor degrees walioingia jeshini wakiwa na 30s, kuitafuta ndoa na 36+ Ni hatari Sana kwa afya zao
Kwani jeshi linachukua mtu akiwa na 30? Mwisho si ni 28 au
 
Nawahurumia sana watoto wa kike, Hasa bachelor degrees walioingia jeshini wakiwa na 30s, kuitafuta ndoa na 36+ Ni hatari Sana kwa afya zao
na wanatoa mimba sana maana ukikutwa na mimba ni hatari
 
ila sheria ilikuwa nzuri changamoto ni wazee wanaojiunga na jeshi sasa hivi,
na vile wamerelax wanaishi kwa tabu
 
Back
Top Bottom