OLS
JF-Expert Member
- Oct 12, 2019
- 426
- 685
Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara imekanusha suala linaloendelea mtandaoni kuwa serikali imepitisha Economic Partnership Agreement(EPA) ambayo imetajwa na wasomi wengi kuwa itasababisha Tanzania kupoteza mapato yanayotokana na Importations kwa takribani 71% in the long run
Wizara imesema mijadala inayoendelea mitandaoni kuhusu suala hilo halina ukweli bali bado Tanzania inaendelea kuwa na msimamo wa kukataa makubaliano hayo ambayo yalipingwa vikali na Rais Mkapa mwaka 2015 katika moja ya andiko lake, ambapo pia rais Magufuli aliyakataa suala hilo.
Serikali imesema inaendelea kufanya mambo yenye manufaa kwa nchi na Jumuiya ya Afrika mashariki na kuwataka wananchi kupuuza taarifa zinazoenea mtandaoni.
MIJADALA KUHUSU EPA
EPA ni makubaliano yanayotaka kuweka biashara huria kati ya nchi za Afrika na Ulaya, kwa kuondoa vikwazo vya kuingiza na kutoa bidhaa. Yaani Ulaya watakakuwa wanaingiza bidhaa zao nchini bila kodi na tozo, hali ambayo imeonekana itashusha mapato ya nchi yanayotokana na importations. Aidha kutokana na uchanga wa viwanda vilivyopo, makubaliano haya yametajwa kuua viwanda vya ndani. Ambapo rais Mkapa alisema kuwa yataifanya makubaliano yataifanya Afrika kuwa Dampo.
Katika nchi za Afrika mashariki, Kenya wameshakubaliana na EPA na wameanza kutekeleza huku Tanzania, Uganda na Burundi zikiwa bado hazijakubaliana na habari hiyo.
Tanzania kama nchi inayoendelea inafaidi kupeleka bidhaa katika nchi za Jumuiya ya Ulaya bila kutozwa kodi kutokana na makubaliano ya Everything But Arms(EBA) ambao uliingiwa mwaka 2001 ikiwa na nia ya kukuza viwanda vya nchi zinazoendelea.
Kuingia katika makubaliano ya EPA kutaifanya Tanzania isiweze kufanya protectionism. Na makubaliano haya yanakuwa kama EU nao wanataka kufaidi kile ambacho nchi zinazoendelea zinafaidi kupitia EBA.
HALI ILIVYOKUWA
Hivi karibuni kumekuwa na tetesi kuwa serikali ilikuwabaliana na suala hilo na kukawa na mijadala mtandaoni ikiwa nchi imefanya study ya kujua madhara ya suala hilo. Swali kubwa lilikuwa, kama nchi inafaidika kwa EBA kuna haja gani ya kujiunga na EPA?
Lakini kwa kanusho hili la Serikali limeleta unafuu na ahueni kwa kuona kumbe tuko makini
Signed
OEDIPUS
Pia, soma;
Thread 'Rais Samia kusaini EPA huko Brussels?' Rais Samia kusaini EPA huko Brussels?