Serikali: Hatujasaini EPA, Msimamo wetu uko palepale

Brother umeelewa lakin maana ya EPA?au umekurupuka kuandika.
 
Hujaelewa vizuri mkuu, kasome tena.
Kwa kifupi tukisaini mkataba wa EPA bidhaa kutoka Ulaya hazitalipiwa kodi hivyo nchi kupoteza 70% ya fedha itokanayo na kodi kwa bidhaa hizo.
 
Hujaelewa vizuri mkuu, kasome tena.
Kwa kifupi tukisaini mkataba wa EPA bidhaa kutoka Ulaya hazitalipiwa kodi hivyo nchi kupoteza 70% ya fedha itokanayo na kodi kwa bidhaa hizo.
Lakini wananchi watapata bidhaa kwa bei rahisiiiii, kuliko zile zinazozalishwa ndani,
Na hii kwa ajili ya ulaya tu, China ambao ndio tunaagiza sana wao wataendelea kulipa,
So hiyo 70% mimi sikubakiani nayo
 
Mimi nafkiri tunaagiza sana bidhaa kutoka nchi za asia, kwa hiyo tutaendelea kupata kodi nyingi tu, hawa ulaya kwani tunaagiza nini zaidi ya china?
Kwa hiyo epa ije tu
 
Hujaelewa vizuri mkuu, kasome tena.
Kwa kifupi tukisaini mkataba wa EPA bidhaa kutoka Ulaya hazitalipiwa kodi hivyo nchi kupoteza 70% ya fedha itokanayo na kodi kwa bidhaa hizo.
Mimi kwa baadhi ya mambo niliyoyasoma, nimeshapata ufahamu kuwa, bila Ulaya na Marekani hakuna nchi inayoweza kuendelea.

Malaysia iliendelea kwa teknolojia kutoka Ulaya. China iliendelea kwa teknolojia ya Ulaya. Nchi zote tunazozijua zipo hapo zilipo baada ya kuruhusu mwingiliano wa bidaa kutoka kule kulikoendelea.

Sisi mbumbumbu wa Tanzania hata tufungiwe mipaka, kusiingie chochote, hatutaweza kufanya lolote. Tuache ujinga wa kudanganywa na wajinga wa CCM kuwa tuna cha maana sana tunachoweza kufanya kwa kuzuia ushirikiano wa soko na Ulaya.

Tuwe wabunifu katika kutafuta vyanzo vipya, na pia watanzania wawe wabunifu wanunue teknolojia badala ya juice, cheni, hereni, saa na simu.
 
Hiyo advantage unayoitaja unaipata kwenye EBA ambapo vitu vyote hivyo huingia EU bila kodi mkataba ulisainiwa 2001, nia ikiwa ni kukuza uchumi wetu. Hili suala la EPA ni suala la EU kuingiza bidhaa nchini bila kodi. Elewa kipengele hicho kwanza
 
Msimamo wa serikali ni upi??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…