Serikali hii ya Magufuli itakuwa na ubavu wa kugomea masharti magumu ya Wachina ilhali wanataka kukamilisha miradi hii ndani ya miaka mitano?

Hii sgr hadi ifike mwanza na kigoma sijui hali itakuwaje, hapo bado katavi. kuna wataalamu wanadai tungekarabati hii iliyopo, maana na yenyewe ni sgr.
 
Magufuli hana rafiki; kwa hiyo hashindwi kabisa kuwakatalia Wachina papo kwa papo wakileta masharti asiyokubaliana nayo.
HIVI, vile visenti vya corona kutoka EU viliisharudishwa?
 
AMEN
 
Mkuu mbali ya kutanguliza muono wako, tujitahidi kila mara tuwe objective na tujitahidi kuwa na comparative analysis ya suala la mikopo kwa kufananisha na nchi mbali mbali zenye mazingira kama yetu..

Nchi yetu bado tunaweza kukopa bila kutikisika 64 billion USD.

Projects za Nyerere dam na SGR probable financial deficits ni 3 billion almost. Na hii pesa tunaweza ku raise kwa Multilateral, bilateral au Developement financing Agencies.

China ananunua US bonds za 260 billion USD kwa mwaka, kwa interest ya 2%.

Sisi tukitaka 30 billion atatupatia tuu, ila akiwa na wasi wasi wa sisi uwezo kulipa ama atatupandishia loan interest labda 4% , ama atatukopesha kibiashara kupitia shares contributions/ Financial loan influence alizo nazo, Africa Developement Bank, Asian Developement Bank, OECD Bank, au Bretton Wood Institutions kwa interest policy za mashirika hayo.
(Mfano tuu: China inasema lipa mambi ya mkopo kwa Tanzania 10 billion na akishindwa kulipa ni mimi nitamsimamia kwa michango yangu kwa Benki yako. Hii ni financial influence ya Nchi )

Au akapitishia IDA (International development Agency) chombo chesterfield kutoa misaada kwa nchi Maskini sana, ila huchukua muda kupata mkopo na nchi nyingi sana zinapenda zikopeshwe kupitia mfuko huu.

Wafanya biashara binafsi ndio uwekezaji wao kwetu unakuwa wa Kibiashara. Na hivyo wanatumia matakwa ya biashara kukopesha.
Ila nchi inaweza kulazimisha tukopeshwe ila collateral kwa mkopo huo Nchi ikatuwekea dhamana..

Nchi haikopeshi pesa yake ya Kodi kibiashara . Ila pesa hizi hutolewa na masharti ya kisiasa, tofauti na pesa za kibiashara ambapo siasa hua si lazima kwamba tana na mkopo.

International development funding policies ni suala pana kidogo na linahitaji muda kulieleza kwa ufasaha.
 
Kuna nini tena kimeinesha ishara ya mkwamo wa hiyo miradi.kila siku nipo u tube naona video za mwendelezo wa miradi.
 


Ni kama unapiga lamli, kwani hiyo miradi imesimama au inaendelea? Hebu tumia akili japo kidogo basi.
 
Inalekea ulikuwa hulipi kodi wewe, unaandika mpaka unaharibu keyboard kwa hasira?
 
Mmmmh...unaijua mikopo ya wachina kweli mkuu.mikopo ya wachina Ni collateral.Hela ya Mchina Ni hatari kuliko ya wazungu.Mchina hacheki na ndio maana hana habari na cjui utawala bora yy ni manufaa ya kiuchumiy kutoka kwako.Madhsifu yako hayamhusu.MCHINA SI RAFIKI JINSI UNAWAZA.NI HATARI.
 
Amini usiamini, unayoyasema ni kweli kwa client aliye fisadi. Ndo maana viongozi mafisadi kama JK wanawapenda maana wanawaeleza waongeze 20 percent nao wanakuwa na masharti ya kuua.

Ukiwa na kiongozi mzalendo, hiyo hakuna na mnapata dili safi. Tatizo mmekariri tu. Na hata hao wazungu wana masharti ya kunyonga pia.
 
Unahisi Ni kukariri,kuna siku yaja Afrika itakuwa ya mchina.Wewe unajua yaliyosainiwa na hao wanasiasa unaodhani ni wazalendo.Huwajui wanasiasa vizuri we.Mkopo wa mchina cyo km ule wa wazungu.Mradi unaoanzisha ndio dhamana ya mkopo.
Hawa unaodhani ni wazalendo,subiri watoke madarakani ndio utajua walikuwa wazalendo au la.
Kilichopo Danganyika kwa sasa ni kwamba wamepunguza wigo wa watu kufaidika na ufisadi.Ni wachache wanafaidi.kakikundi fulani.
Leo CAG hakagui sekta ya madini,hakagui ATCL unadhani ni bahati mbaya.
 
Nadhani kunashida kwetu sisi wananchi na sijui hii shida inaanzia wap nadhan hatupendi kusoma au tunapenda sana umbea na hatutaki kabisa kujishugulisha nijuavyo mimi miradi hii haijawahi kuomba pesa ikakwama na mfano ule mradi wa sgr pesa ya kufika dodoma tulisha pewa na ipo lakini pia nijuavyo mimi serikali ya magufuli au yetu sisi watanzania ya sasa sio serikali ya hivo mkataba wowote utaingiwa kama una maslahi mapana ya taifa period.
 
Kama awamu hii ya uongozi ilikinzana na China juu ya mkataba wa ujenzi wa Bandari Bagamoyo, iweje leo masharti ya wachina tuyaweze?

Msaada, tuta angani!
 
Teyari Wachina wameshaanza kuzengezengea ukiona ndege aina ya tai akizunguka angani sehemu fulani ujue chini kuna mnyama anakaribia kuwa mzoga.
Kuzengea zengea nini mkuu, nani kakwambia Wachina wanaganga njaa!!

Kwa taarifa yako hivi sasa Taifa la China limekwisha ipiku Amerika kiuchumi, hawana shida yoyote na mali asili zetu wala nini sijui, wanaweza kuzipata popote Duniani muda wote wakizihitaji.

Mnashangaa nini Wachina wanaposema wakijenga reli au Bandari basi wao ndio wawe wahusika wakuu kukusanya mapato ili iwe rahisi kwao kurudisha mikopo yao on time mpaka Deni litakapo isha, hawajawahi kusema katika ukusanyaji mapato Serikali itakosa gawiwo - sisi tunalalamika nini wakati hatuta invest chochote zaidi ya aridhi na rasimali watu.

Niliwahi kuwambieni Wachina wanafanya hivyo kutokana na bad experience katika ujenzi wa reli ya TAZARA, Wachina walitumia matrillion na matrilion ya pesa za walipa kodi wao, hivi sasa ni karibu miaka hamsini tangu wajenge na kutukabidhi reli kwa mkopo husio na riba, mwisho wa siku wamevuna nini tumewazika hela zao hatajawarudishia hata senti tano ya mkopo wao na wala hawajatupeleka kwenye Mahakama ya Kimataifa kudai deni lao, hivi kwa akili za kawaida unategemea Wachina wana waamini tena Washwahili - sisi tunakazania Wachina wezi wezi, kumbe sisi ndiyo matapeli namba moja!

Hata wakisema ndio wawe wakusanyaji wakuu wa mapato ya reli za Kenya na Uganda wanazo jenga, mimi naona bora iwe hivyo ngozi nyeusi si watu wa kuaminika hata kidogo - sisi tunakazania kuwalaamu Wachina 24X7, cha ajabu hakuna anaye kumbuka tulivyo watapeli/wazika fedha zao lukuki walizo jengea reli ya TAZARA kwa mkopo - Wachina wali-learn a very hard lesson katika project ya ujenzi wa reli TAZARA hawawezi kuruhusu ujinga huu ujirudie tena,walisha baini ufujaji na wizi wa fedha za umma katika mashirika ya umma na Serikalini kwenye Nchi nyingi za Kiafrika ndio maana walisha kata shauri kwamba wakitaka mkopo yao urudi kwa uhakika ni lazima wakusanye mapato mpaka deni lao lote liishe mradi wanatoa %ge fulani ya mapato kama gawiwo kwa Serikali husika - mbona mimi sioni kama hilo ni tatizo. Hapo sijazungumzia kuhusu ujenzi wa Bandari ya Bwagamoyo - mantiki zinabaki zile zile - hatuaminiki katika ulipaji madeni ndio maana tunawekewa kwa kile mnacho kiita masharti magumu, period.
 

Mkuu umekuwa so Negative mpaka inanipa wasi Aina ya mtu. Watanzania hatuko Hivi. Tunakuwa na positiv na wakati negative. Maandiko yako yako so empty kiasi naogopa unaweza jiua wewe miradi ya kuwasaidia wananchi ikikamilika. JPM aliomba misada yenye masharti nafuu. But wewe unakuja na RAMLI ili tu Tz ijadiliwe vibaya. You are a sadomasochistic.

Uchaguzi umepita Sasa wa kuangaliwa ni MTanzania. Embu fanya kitu cha matokeo Chanya. Toa mchongo. Mpigie simu hata Lissu akupe sehemu ya mipango yake kwa nchi ya Tz kupata hela za marekani na ulaya bila masharti. Au mpaka Uwe kiongozi ndo utasaidia Mwananchi. Basi Acha kuandika maoni hasi. You seem to be a loser.
 
Bado kidogo Zambia watakabidhi Ikulu kwa wachina ili kufidia madeni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…