Serikali hutumia Tsh. Billion 558 kununua magari kwa mwaka

Cash Generating Unit

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
13,286
Reaction score
39,418
Unaweza usiamini ila ndo pesa za sisi walipa kodi zinapotea huku hapo bado kufanyiwa service, mafuta na takataka zingine.

Piga hesabu ndani ya miaka 10 pesa ngapi inapotea? Kwa dizaini hii tutaacha kukopa?? Juzi hapa Waziri wenu wa Fedha kanunua gari ya 800 milioni.

Inasikitisha sana kuona kodi zetu zinatumika vibaya afu maisha yanazidi kuwa magumu na matozo yanazidi kuongezeka mpaka benki.

IMG_5315.jpg

--

Pesa hizo (TSh. Bilioni 558.4) hutumiwa kila mwaka kununua magari, mafuta, vipuri na matengenezo ya magari

Akizungumza Bungeni wakati akiwasilisha Bajeti ya Taifa kwa mwaka wa fedha 2022/23, Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba alisema Serikali ina magari zaidi ya 15,742, pikipiki 14,047 na mashine 373.

Kwa hiyo, amependekeza Serikali ibadilike kutoka mfumo uliopo kwa kuwakopesha magari watendaji wa Serikali wenye sifa.

"Katika hali hiyo, gharama za matengenezo zitakuwa juu yao wenyewe, na mafuta yatatolewa kwa njia inayofaa," alisema

Hata hivyo alisema utaratibu huo utavitenga vyombo vya Ulinzi na Usalama, Mahakama, viongozi wakuu wa Wizara, Mashirika, Wakala, Mikoa, Wilaya na Wasimamizi wa Miradi ambapo hawatazidi watano (5) kwa kila taasisi.

“Viongozi wengine wenye haki ya huduma ya magari watakopeshwa kwa ajili ya magari, kwa kufanya hivyo, Serikali itapunguza gharama za matengenezo, mafuta na vipuri vya magari.”

Aliongeza: Kulingana na mbinu hiyo, gharama ya matengenezo, mafuta na vipuri vya Serikali kwa magari itafikia takriban Sh50.5bilioni

Kwa mujibu wa Mwigulu, akiba ya zaidi ya shilingi bilioni 500 itatengwa kwa ajili ya ununuzi wa dawa muhimu, kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya ufundi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo

Chanzo: The Citizen
 
Lipa Kodi mkuu wakubwa wazitumie watakavyo kwani mtafanya nini zaidi ya kulalamika tu .Nyumbu ni Nyumbu tu
 
Bunge lijao lazima tozo zitaongezeka ili zifanyie service magari haya.
 
Wangeongeza ifike hata trillions tatu ili watanzania akili zikae sawa.
 
800M ni pesa ndogo sana angenunua ya 5Billion kidogo hata mm ningeshtuka.. changa kodi kijana acha kulalamika
 
Tunakilema mahara fulani vichwani.
Hakuna mahali tutafika
 
Unaweza usiamini ila ndo pesa za sisi walipa kodi zinapotea huku hapo bado kufanyiwa service, mafuta na takataka zingine.

Piga hesabu ndani ya miaka 10 pesa ngapi inapotea? Kwa dizaini hii tutaacha kukopa?? Juzi hapa Waziri wenu wa Fedha kanunua gari ya 800 milioni.

Inasikitisha sana kuona kodi zetu zinatumika vibaya afu maisha yanazidi kuwa magumu na matozo yanazidi kuongezeka mpaka benki.

View attachment 2327833
NCHI YENYE WANANCHI MIL.60 MASIKINI wa KUTUPWA angalia KIONGOZI MWENYE UCHUNGU na RAIA WAKE
1660769087494.jpg
 
Pesa hizo (TSh. Bilioni 558.4) hutumiwa kila mwaka kununua magari, mafuta, vipuri na matengenezo ya magari

Akizungumza Bungeni wakati akiwasilisha Bajeti ya Taifa kwa mwaka wa fedha 2022/23, Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba alisema Serikali ina magari zaidi ya 15,742, pikipiki 14,047 na mashine 373.

Kwa hiyo, amependekeza Serikali ibadilike kutoka mfumo uliopo kwa kuwakopesha magari watendaji wa Serikali wenye sifa.

"Katika hali hiyo, gharama za matengenezo zitakuwa juu yao wenyewe, na mafuta yatatolewa kwa njia inayofaa," alisema

Hata hivyo alisema utaratibu huo utavitenga vyombo vya Ulinzi na Usalama, Mahakama, viongozi wakuu wa Wizara, Mashirika, Wakala, Mikoa, Wilaya na Wasimamizi wa Miradi ambapo hawatazidi watano (5) kwa kila taasisi.

“Viongozi wengine wenye haki ya huduma ya magari watakopeshwa kwa ajili ya magari, kwa kufanya hivyo, Serikali itapunguza gharama za matengenezo, mafuta na vipuri vya magari.”

Aliongeza: Kulingana na mbinu hiyo, gharama ya matengenezo, mafuta na vipuri vya Serikali kwa magari itafikia takriban Sh50.5bilioni.

Kwa mujibu wa Mwigulu, akiba ya zaidi ya shilingi bilioni 500 itatengwa kwa ajili ya ununuzi wa dawa muhimu, kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya ufundi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Toka nimjue meigulu leo ndio naona kaongea jambo la maana
 
Watanzania wenzangu, tuendelee tu kukwepa kodi. Hata sisi pia tungetamani kuendesha hayo Ma Vii Eitee.
 
Taarifa hii ya kusikitisha imeandikwa na gazeti la THE CITIZEN .

Ikumbukwe kwamba nchi ya Tanzania hununua magari ya kifahari hata kwa viongozi duni wenye vyeo vya chini kama MA RC , MA DC na MA DED , hela hizo ni kwa kila mwaka , na yaweza kuongezeka kutokana na hali ya uchumi wa kidunia

Taarifa iliyotolewa haikuweka wazi kiasi cha hela zinazotumika kwenye manunuzi ya mafuta ya mashangingi ya viongozi hao
 
Kama ni kweli haijakaa vizuri japo uandishi wako umetumia lugha isiyokuwa nzuri kwa viongozi wetu.

Inaama kila mwaka yale magari yanayo nunuliwa Zero KMS yanakuwa yamechakaa?

Huwa yanauziwa kina nani baada ya mwaka mmoja kwa kuwa sijawahi kusikia mnada?

Nafikiri hilo mtu akiliotea atakuwa amenunua gari jipia kabisa
 
Back
Top Bottom