Serikali: Huu ndio ushauri wa mwisho kwa Bima ya Afya ya Taifa (NHIF)

Hivi swali la gharama za bima nyengine limejibiwa? Na kuhusu ukomo wa umri kumekaaje huko. Na uwezo wa kuwabeba wazazi na wakwe?
Gharama zao ni sawa na za NHIF na baadhi yao gharama zipo chini ukilingansha na NHIF. Kwa bima nyingine, mwanachama ana haki ya kumuandikisha yeyote yule bila kupangiwa.

NHIF wanawapangia wanachama aina ya wanufaika.....wanataka mke/mume na watoto tu. Bima nyingine unamuingiza shangazi, mjomba, housegirl, jirani au mtu yeyote bila kubaguliwa ilmradi idadi ya wanachama izingatiwe.
 
Joined Feb 3 2008. Bado ananufaika na bima ya wazazi.
Ndio mkuu. Kwani shida iko wapi? Ni wazazi wangu wana haki ya kunilea mimi mtoto wao. Mtoto kwa mama hakuwi.
 
Reactions: Atn
Je wajua hyo mifuko mingine ulioitaji hata kufikika ni kazi na ofs zao hazijulikani na ada zao huenda zikawa ghali sana hata kufikika
Mfano ofs za STRATEGIES OR MOMENTUM MIE SIJAWAHI KUZIONA NA SIJUI WAKO WAPO HUENDA WAPO DAR TU HATA SIMU ZAO NAMBA ZAO HAZIJULIKANI naaomba kujua wako wap msaaada
 

Mkuu kwa ambao tunataka kuandikisha watoto tu, inawezekana?
 
Mkuu, vitabu vyote navifahamu vizur sana, kuna NHIF pricing, na NHIF ICD codes, nachokwambia sibahatishi, NHIF wanataka mtoa huduma afuate taratibu matibabu kwa mujibu wa standard treatment guidelines ( STG) wakati wateja wao wanataka wanabagua dawa, mfano mzuri ni kwenye UTI , unakuta mteja anataka azithromycin ( Azuma) lakini STG imeelekeza toa amoxycillin au nitrofurantoin au ciprofloxacin katika level ya zahanat, lakini health centre na hospital imeelekeza toa Amoxy clav, AMA kwa msaada wa culture and sensitivity toa powercef.

Kifupi huoni mahala pameandikwa toa azuma, hapa ndipo ulipo mkanganyiko kati ya wanachama na NHIF kuona wanaonewa sana, ila taratibu za matibabu zinatakaje?

Hili linafanyika kuondoa risk ya usugu wa dawa
 
Strategies wako mikoa mingi sana, ila ada ya kuchangia malipo ya uanachama yako juu sana kuliko watu wanavyofikiria, NHIF wana gharama ndogo sana kulinganisha na hao wengine
 

Mkuu utakuwa wewe ni Mfanyakazi wa NHIF nina mtu anafanyia kazi NHIF tena anacheo aliyosema jamaa ni kweli kabisa labda wewe unatetea ugali wako.
 
Mkuu utakuwa wewe ni Mfanyakazi wa NHIF nina mtu anafanyia kazi NHIF tena anacheo aliyosema jamaa ni kweli kabisa labda wewe unatetea ugali wako.
ingekuwa poa sana ningekuwa nafanya kazi NHIF, ila hata fikra hizo hazipo, nimegombana nao sana kwa nyakati tofauti tofauti, nawafahamu sana, changamoto zao ni financial management kama Dulu zisemavyo wanajipigia hela za wanachama, ila upande wa huduma tusiwaonee hivyo, watu wanafanyiwa dialysis, operative procedures na major surgeries mbalimbali, Jamani Mnyonge Mnyongeni haki yake mpeni
 
Chanzo cha kwanza cha huo mfuko kuyumba ni ubadhirifu wa pesa za michango ya wanachama.Fedha ambazo haziwezi kurudi kwasababu zimeenda kwa wenye kula nchi.Sasa huo mzigo umeletwa kwa wanachama kwa sababu mbali mbali zisizo na kichwa wala miguu ila wasababu hii nchi hatujielewi tunaona ni sawa tu.
 
Hapana mkuu, kuilaumu serikali moja kwa moja is unfair, Serikali inapowapa taasisi watu waisimamie maanake imewapa dhamana kubwa, wakifail haimaanishi serikali imefail ila watu hao, cha msingi ni reformation tu
Serikali ndiyo iliyoshindwa.kwasababu serikali ndiyo iliyoshindwa kuwasimamia hao waliowapa hiyo dhamana yajufanya hiyo kazi.Wananchi tumeiajiri serikali kwahiyo lawama lazima ziende kwa tuliyemuajiri.Serikali ingekua inachujua hatua hayo maujinga yasingekuwepo.Ila haiwezi kwasababu yenyewe ni sehemu ya tatizo.
 
Ushauri wangu.
1. Serekari iache kudokoa pesa za wagonjwa na psssf.

2. Nilimpoteza mamaangu. Inaniuma Sana. Bima ya afya iachwe isiguswe. Ummy mwaimu utachomea moto wewe
 
Mkuu kwani ugonjwa unapokuja unaagalia kama mgonjwa hana access ya kituo cha kutolea huduma chenye level ya kutoa dawa nzuri. Mimi nakuambia dawa fulani hainitibu afu wewe unanilazimisha uniandikie dawa hiyo nikafanyie nini? Huoni kwamba huo ni ukiritimba usioikuwa na sababu zozote za msingi?

Niliwahi kwenda hospitali fulani wakaniandikia dawa ambazo hazinitibu nikaamua kwenda kuziuza pharmacy nikapata pesa nikaongezea nikaenda kununua dawa halisi. Je, huoni huu ni usumbufu kwa wateja?

Halafu hili katazo la kumzuia mgonjwa kwenda kupata dawa kwenye pharmacy ikiwa ipo out of stock kwenye hospitali ni la kipuuzi sana aisee! Sasa wagonjwa sisi tufanyeje tupone magonjwa ikiwa tunazuiliwa kwenda pharmacy? Nchi ya kipumbavu sana hii.
 
Mkuu utakuwa wewe ni Mfanyakazi wa NHIF nina mtu anafanyia kazi NHIF tena anacheo aliyosema jamaa ni kweli kabisa labda wewe unatetea ugali wako.
Huyo atakuwa anatetea mpunga bila kujali kwamba hata ndugu zake nao wanahitaji matibabu. Jamaa mbinafsi sana aisee!
 
Wakuu kama taifa kila mmoja anaweza kuona makosa,

Wachache wanaishauri serikali iliyoshindwa. Iliyoishiwa pumzi.

Wachache zaidi wameamua kutafuta mfumo MBADALA

As a thinker nina suluhisho ktk endelevu ktk mazingira ya tz.

Thread 'Bima ya Afya Vikoba' SoC04 - Bima ya Afya Vikoba

Kama unaunga na una ushauri ktk kuboresha ili to make it happen. Plz shauri. Kama umependa naomba vote yote yako sawa na link hapo juu
 
Kuna tetesi kuwa serikali ilichota fedha NHIF na kupelekea mfuko kuwa taaban. Sasa hivi Nhif ni usumbufu mkubwa kila ukienda kutibiwa unakuta kuna foleni nyingine ya kuhakikiwa.
Ilikuwa ni jukumu la serikali kumtibu mtumishi wa uma, ila ufisadi wa Mkapa akafuta akaanzisha haya mavi yanaitwa NHIF!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…