Serikali: Huu ndio ushauri wa mwisho kwa Bima ya Afya ya Taifa (NHIF)

Serikali: Huu ndio ushauri wa mwisho kwa Bima ya Afya ya Taifa (NHIF)

Ilikuwa ni jukumu la serikali kumtibu mtumishi wa uma, ila ufisadi wa Mkapa akafuta akaanzisha haya mavi yanaitwa NHIF!
Mkapa alaumiwe sana kutuletea huu upumbavu unaolitesa taifa hadi Yesu atakaporudi. Nchi ya kikwuma sana hii.
 
Wakuu kama taifa kila mmoja anaweza kuona makosa,

Wachache wanaishauri serikali iliyoshindwa. Iliyoishiwa pumzi.

Wachache zaidi wameamua kutafuta mfumo MBADALA

As a thinker nina suluhisho ktk endelevu ktk mazingira ya tz.

Thread 'Bima ya Afya Vikoba' SoC04 - Bima ya Afya Vikoba

Kama unaunga na una ushauri ktk kuboresha ili to make it happen. Plz shauri. Kama umependa naomba vote yote yako sawa na link hapo juu
Adante sana mkuu . Lakini hii bima ya afya ya NHIF hata ushauri namna gani hakuna namna itakuja kufufuka.
 
Naomba kutangaza masilahi (declare interest) kwamba mimi ni mnufaika wa mfuko huu kupitia wazazi wangu ambao ni watumishi wa umma.
Moja ya tatizo la mfuko ni hili mkuu 'tpaul'; wewe mwenye umri wa zaidi ya miaka 18 ni mtu mzima; na bado unawategemea wazazi katika swala hilo? Hii ni sehemu moja tu ya maeneo mengi yanayoikwamisha NHIF.
 
Mkuu, hapana , NHIF hawajawahi kulazimisha kutoa dawa aina moja , isipokuwa ni utashi wa priscibers, mfano dawa katika tiba ya mafua, sio tu lazima kuprescribe cetrizen, Kuna dawa kama chlorpheniramine, promethazine loratadine etc hizi zote zinatibu flue na common cold zinazotokana na allergic reactions , sasa hapa ni chaguo la daktar wako na qualification yake kuprescribe dawa hizo.
Duh.
Hata hizi ni dawa za 'prescription'? Mbona kwingineko ni OTC! (Over-the-counter).
 
Katika siku za karibuni Bima ya Afya ya Taifa imekuwa gumzo kila kona, hasa inapodaiwa kwamba mfuko huu wa bima unaotoa matibabu kwa watumishi wa umma na familia zao, unakaribia kukata roho. Naomba kutangaza masilahi (declare interest) kwamba mimi ni mnufaika wa mfuko huu kupitia wazazi wangu ambao ni watumishi wa umma.

Mbali na NHIF kuna mifuko mingine mingi inayotoa huduma nzuri zaidi hapa nchini ukilinganisha na mfuko huu ambao kila kukicha umekuwa ukiwafanyia vitimbi wananchama wake na kuwakosesha huduma za matibabu kwa sababu ambazo hazina kichwa wala miguu. Nasema haya kwa ushahidi mubashara. Uongozi wa NHIF umekuwa ukiwabania wanachama wake dawa nzuri na zinazotibu barabara kwa kuhofia wananchama wao kuwa na afya mujarabu. Lengo la kufanya hila zote hizi wanazijua viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia mfuko. Vitimbi vya karibuni kabisa kufanywa na NHIF ni kufuta fao la Toto Afya Card na kuwapangia wanachama kiasi cha kuumwa – kwamba kila mwanachama aumwe mara 4 tu kwa mwezi!

Kuna bima lukuki hapa nchini zinazotoa huduma nzuri bila unyanyapaa wala vitimbi kwa wananchama. Nimewahi kuwa mwanachama wa bima za afya Medex na AAR. Mifuko hii haina ujinga kama huu tunaoshuhudia NHIF. Wanajali zaidi uhai wa mwanachama tofauti na NHIF wanaojali matumbo yao na kuwaacha wanachama wajifie kifo cha mende. Ukiwa ndani ya AAR au Medex ni raha tupu. Hata ukiumwa ugonjwa mkubwa ulioshindikana kutibika hapa nchini, unasafirishwa nje ya nchi kwenda kutibiwa. Kupitia mifuko hii, wagonjwa wengi tu wametibiwa Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, Afrika Kusini India na mataifa mengine ya nje yenye huduma nzuri za afya. Lakini kwa NHIF, ugonjwa wako ukishindikana kutibiwa hapa nchini, unaachwa ujifie kama mbwa. Inauma sana.

Baada ya kutoa dokezo hiili, naomba sasa nitoe ushauri wangu wa mwisho jinsi ya kuboresha huduma za NHIF. Kwanza ni kuondoa ukiritimba na figisu kwa wanachama. Nashauri wanachama wapewe uhuru wa kuchagua mfuko wa matibabu tofauti na sasa ambapo watumishi wote wa umma hulazimishwa kukatwa pesa na kutibiwa na NHIF watake wasitake. Wanachama wengi, ambao ni watumishi wa umma, wamechoshwa na vituko vya NHIF. Wanatamani wafunguliwe minyonyororo ya utumwa waliyofungwa kwa muda mrefu ndani ya NHIF wakatafute huduma nzuri kwenye mifuko mingine inayotoa bima za matibabu kama vile AAR, Momentum, Strategies, NMB, NSSF na mingine mingi tu iliyotapakaa hapa nchini.

Kwanini watu wanyimwe uhuru wa kujiunga na mifuko mingine ilhai kila siku NHIF inalalamika kuwa na hali mbaya ya kiuchumi? Ukiona hivyo ujue kuna manufaa ambayo serikali na watumishi wa NHIF wanayapata ambayo wakiruhusu watu waondoke, wanaweza kuyakosa. Kwa maana hiyo kumbe NHIF haipo kwa ajili ya maslahi ya wanachama bali ni kwa ajili ya maslahi ya serikali na wachumiatumbo wachache wasiopenda kuona watanzania wanakuwa na siha njema. Huu ni zaidi ya uhaini na uhujumu uchumi. Naomba TAKUKURU wafanye uchunguzi wa kina.

Ili NHIF iondokane na malalamiko ya gharama kubwa za matibabu kwa wanacham wake na kuhofia kufilisika, basi iwaachie wanachama waondoke mmoja mmoja waende wakatafute matibabu kupitia bima nyingine za afya. Wakibaki wanachama wachache inaweza kuwahudumia vizuri zaidi. Na hata hao wachache wakiamua kuhama, waachiwe waondoke. Wanachama wote wakishaondoka NHIF ifunge ofisi zake zote nchini na serikali iwapangie kazi nyingine waliokuwa waajiriwa wa NHIF. Kufikia hapo tatizo litakuwa limepata ufumbuzi wa kudumu. Huwezi kung’ang’ania jambo linakuuumiza kichwa wakati kuna ufumbuzi wa kudumu usiohitaji gharama yoyote.

Ikiwa serikali itafuata ushauri huu, itajiondoa jumla kwenye lawama za watanzania wanaokufa kila siku kwa sababu ya ubovu wa huduama za NHIF inayolalamika kutokuwa na fedha za kutosha kugharamia matibabu ya wanachama wake hadi kufikia hatua ya kufuta fao la Toto Afya Card na kuanzisha masharti ya kipuuzi kwa wananchma ambayo hayatekelezeki.

Nawasilisha.
Mkuu, uko misguided
1. AAR ilishakufa
2. NHIF wako too generous, vitita vya moba nyingine ni ghali zaidi na endapo nhif angekua anakusanya kwa wateja pesa sawa na private insurance… angekua the best in sub Saharan africa

Tatizo hamfanyi fair analysis
 
Mkuu, uko misguided
1. AAR ilishakufa
2. NHIF wako too generous, vitita vya moba nyingine ni ghali zaidi na endapo nhif angekua anakusanya kwa wateja pesa sawa na private insurance… angekua the best in sub Saharan africa

Tatizo hamfanyi fair analysis
Tatizo lilianzia wapi mluu? Wewe unaona NHIF wako fair kwa hivi vitita vyao vya kibaguzi? You cannot be serious mkuu
 
Tatizo lilianzia wapi mluu? Wewe unaona NHIF wako fair kwa hivi vitita vyao vya kibaguzi? You cannot be serious mkuu
Ni bima Gabi ina Toto afya card?

Kwa pesa za kitita cha nhif unaweza kupata similar services kwa hizo bima binafsi?

Be serious
 
Back
Top Bottom