wastani kwa idadi
JF-Expert Member
- Jun 28, 2024
- 503
- 1,432
Muhimu: Ni nje ya vyuo kama open university chenye matawi kila mkoa, Pia kwa vyuo vya kati vya ufundi, nursing, ualimu, utalii, hotel management, n.k.
Tanzania Bara kuna mikoa 26 inayoshiriki kuchangia pato la taifa lakini cha kusikitisha vyuo vya serikali vipo concetrated sehemu chache
Dar es Salaam na Dodoma ni exception kwasababu ni miji mikuu ya nchi na kuna mchanganyiko wa watu kutoka mikoa 26 ya Tanzania.
Shida inakuja kuna baadhi ya mikoa imekuwa na vyuo vingi wakati huo kuna mikoa ina chuo kimoja, viwili ama hakuna kabisa.
Mfano ni Mbeya kuna vyuo kama NANE vya serikali, vimejengwa na vinaendeshwa kwa kodi za wananchi wa mikoa 26 ya Tanzania
MADHARA YAKE
Uwiano usio wa haki wa wahitimu wa vyuo vikuu - Mikoa yenye vyuo vikuu vingi, kama Mbeya na Mwanza, inatoa nafasi nyingi zaidi kwa wakazi wa maeneo hayo kutoa wahitimu wengi
Gharama kubwa za elimu kwa wanafunzi wa mikoa mingine - Wanafunzi kutoka mikoa isiyo na vyuo wanalazimika kutumia gharama zaidi kwenye usafiri, kulipia hostel, n.k, wakati wenzao wanaweza kuishi na kula nyumbani.
Kuwepo kwa ushindani usio wa haki katika soko la ajira - Mikoa yenye vyuo vikuu vingi ina nafasi kubwa ya kuzalisha wahitimu wengi, ambao wanakuwa na sifa za kuajiriwa
Kudhoofisha maendeleo ya kitaifa - Kutokuwa na uwiano mzuri wa upatikanaji wa elimu ya juu kunasababisha kutokuwa na usawa katika maendeleo ya kitaifa.
Kubana maendeleo ya kielimu kwa watu wenye mahitaji maalum - watu wenye mahitaji maalum wanaweza kushindwa kuhamia mikoa ya mbali kwa sababu ya changamoto za afya, usalama, na kifamilia
USHAURI WANGU.
Mipango ya kujenga vyuo mikoa iliyojaza vyuo ipigwe stop, mikoa imejaza sana vyuo mpaka vya private, Ni zamu ya mikoa mingine kujengewa vyuo kama Njombe, Bukoba, Ruvuma, Mara, Rukwa, Katavi, n.k. lengo kupata uwiano wa idadi ya vyuo vya serikali kwa mikoa yote nje ya Dar na Dodoma, maendeleo ya elimu ya juu yawe na balance

- UDSM college of Health
- MZUMBE
- MUST
- TIA
- CBE
- ADEM
- UCC
- IFM
- TIA
- UCC
- IAA
- DIT
- MIPANGO