Serikali iache kutoa taarifa kwa umma usiku wa manane

Serikali iache kutoa taarifa kwa umma usiku wa manane

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Siku hizi imegeuka tabia. Mimi nasema ni tabia isiyo na afya ya serikali kutoa taarifa kwa umma usiku wa manane. Hili ni jambo la kushangaza sana, najiuliza ni kitu gani kimeisibu serikali Kubehave kama genge la wachawi!.

Sisi tunajua kuwa mida hiyo wananchi wengi wanakuwa wamelala na hata bendera ya nchi inakuwa imeshushwa, Sasa hii ya kutangazia giza maana yake nini?.

Unapotoa taarifa kwa umma wakati watu wamelala unakuwa unataka kitu gani haswa?

Haya mambo ya kufanya kazi gizani ni dalili ya kutojiamini. Baba wa Taifa alikuwa hateui watu usiku na wala alikuwa hatangazi vifo vya viongozi wakubwa Usiku.

Sasa hii ya kufanya kazi gizani kulikoni?
 
Huwa tunam refer baba wa taifa as if alifanya mambo makubwa sana kwenye taifa hili. Kila awamu Ina namna ya uongozi wake ili mradi nchi imesonga mbele. Taarifa itolewe mchana au usiku itasomeka vile vile tu
 
Haya mambo ya kufanya kazi gizani ni dalili ya kutojiamini. Baba wa Taifa alikuwa hateui watu usiku na wala alikuwa hatangazi vifo vya viongozi wakubwa
Siku Ina masaa 24, kati ya hayo ni chini ya 8 tu ndiyo ya kulala. Mtu analala saa ngapi siyo suala la kitaifa ama kidunia. Kila mtu analala muda anao ona unafaa ama amemaloza kazi

Usiku ktk zama hizi maana yake ni "muda wa kupumzika". Siyo jua kuzama. Kuna nchi jua halizami (mchana tupu) na kuna nchi jua halipo kabisa (giza tupu).

Muache mhe rais afanye kazi muda anao ona unafaa na apumzzike atakapomaliza kazi (yaweza kuwa asubuhi, mchana, usiku ama jioni).
 
Muda huo unakuwa una wanga nini mkuu hivyo taarifa zinakupita.
 
Back
Top Bottom