Serikali iache kutoa taarifa kwa umma usiku wa manane

halafu Wakuu naomba kuuliza, hivi kwa nini Bendera ya Taifa lazima ishushwe ifikapo jioni? Na Kwa wale viongozi ambao magari yao Yana Bendera, je, nao huzifunika Bendera hizo ifikapo jioni hata kama wako safarini?
 
Na Kwa wale viongozi ambao magari yao Yana Bendera, je, nao huzifunika Bendera hizo ifikapo jioni hata kama wako safarini?
Gari ya serikali haipaswi kusafiri zaidi ya saa 12 mkuu. Saa 22 gari ya serikali inapaswa kupaki somewhere
 
Sasa hivi Ni 2:00AM huu ndo Muda mzuri wa kutoa Taarifa kwa wananchi tulio makini.
 
Wadau mbona hamsemi ipo taarifa Gani🤔
 
Serikali yetu hailali Kama wewe unavyolala , muda wote serikali yetu IPO kazini kuwatumikia watanzania, unapokuwa umelala na kuota ndoto zako kuwa kuwa serikali IPO kazini ndio maana unaona ukilala kwa amani na utulivu, Kama serikali ingelala Basi kuwa kuwa wewe hapo ulipo ungekesha macho kuangalia mlangoni pako
 
Hii tabia ilianza tangu enzi za Magu kama sikosei.

Uko sahihi kabisa, hii tabia muasisi wake ni Magufuli na mama Samia naye kaiiga. Hata hii tabia ya kila siku rais kuonekana kwenye TV, muasisi wake ni Magufuli. Nadhani washauri wa rais wanadanganyana kuwa mbinu ya raisi kukubalika ni kuwa mubashara kila siku kwenye TV. Wanaamini Magufuli alikubalika kwa kujitangaza kwenye tv kila siku, cha ajabu ilipofika wakati wa kampeni wakaona mwitikio tofauti, na hiyo ndiyo iliyopelekea uchaguzi kunajisiwa.
 

Asilimia 90+ ya watanzania baada ya jua kuzama, yaani usiku kuingia wote huenda kulala. Isitoshe shughuli nyingi za kiserikali hufanyika wakati wa siku na sio usiku. Huu ndio uhalisia na sio kinyume chake.
 

Serikali ni mfumo, hapa tunaongelea binadamu ambao usiku hulala. Asilimia 80+ ya ofisi na shughuli za serikali usiku husimama.
 
Serikali ni mfumo, hapa tunaongelea binadamu ambao usiku hulala. Asilimia 80+ ya ofisi na shughuli za serikali usiku husimama.
Unazani ukilala wewe na serikali imelala? Iheshimu Sana serikali na upunguze matusi kwa serikali, ujuwe unapata muda wa kuandika utakavyo kwa kuwa tu Kuna amani ambayo inalindwa usiku na mchana na Serikali yetu Hii shupavu chini ya mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani
 
Basi nenda wewe ukaonekane kwenye TV uone Kama utakubalika, mh Rais wetu mpendwa anakubalika kutokana na utendaji kazi wake uliotukuka na kugusa maisha ya watanzania wanyonge, kwa hiyo wewe unaumia Nini mh Rais wetu akionekana na watanzania wakiona kazi anazozifanya na kutekeleza? Unataka afanyie gizani? Watanzania Tunafurahi kumuona mh Rais wetu akiwa anatatua kero zinazokuwa zinatukwamisha kusonga mbelee
 
Hahah
Umechoka kulishwa viporo siyo?
 

Serikali ni mfumo nazungumzia watu ambao ndio watendaji wa serikali. Ni wapi naitukana serekali? Maana siku ukitoa maoni yasiyoifurahisha serekali, nyie wapambe tafsiri yenu ni matusi.

Kwa taarifa yako kuandika sio sifa ya amani, bali ni nafasi ya kufanya hivyo. Mimi sijawahi kujivunia uoga ambao kwako unaita amani, mimi ni muumini wa haki fullstop.
 
Hoja dhaifu sana, eti mnataka kuaminisha watu kuwa serikali inafanya kazi sana. Basi ofisi za serikali zifunguliwe masaa 24.
 

Amesimama hapo kutokana na cheo chake na sio kupendwa kwake. Sema matamanio yako ni yeye apendwe, kwani akiendelea kubaki madarakani ww ndio maisha yako yananyooka.
 
Amesimama hapo kutokana na cheo chake na sio kupendwa kwake. Sema matamanio yako ni yeye apendwe, kwani akiendelea kubaki madarakani ww ndio maisha yako yananyooka.
Mimi Kama mkulima naona mchango wa mh Rais wangu mpendwa kuinua maisha yetu wakulima baada ya uamuzi wake wa kuamua kutoa Ruzuku ya billion Mia moja hamsini iliyopelekea kushuka kwa mbolea, vilevile kwa Sasa soko Ni la uhakika Sana chini ya uongozi wa mh Rais wetu mpendwa na kauli mbiu yake ya kilimo Ni biashara, Nani Kama mama? Kiukweli Hakuna, upinzani mtapata Taabu sanaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…