Serikali iache kutujazia tozo kufidia matanuzi yao

Serikali iache kutujazia tozo kufidia matanuzi yao

Extrovert

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2016
Posts
70,785
Reaction score
186,690
Hii nchi ilipofikia nafikiri kilichobaki ni watu waamue kujitoa akili tu utaratibu uvurugike mazima hata nusu mwaka hivi then kitakachofuata baada ya hapo tutakaa kamati ya maridhiano maana dunia nzima itakuwa inaelewa hasa kinachoendelea ni nini!

Hii biashara ya kubembelezana watu wazima kwa mambo ambayo yako dhahiri kabisa ni uzwazwa unaotakiwa ufike tamati. Viongozi wametugeuza misukule wanatufanyia wanavuojiskia hadi lini hii hali. Hata paka ukimfungia ndani ukamtesa na kumuumiza kwa muda mrefu kitakachofuata hutakaa usahau katika maisha yako. Nachokiona yapaswa tuvae ujasiri wa paka.

Tunatambua makusanyo ya kodi ni lazima kwa kila mwananchi ili kuleta maendeleo ya taifa ila kinachoonekana ni kuwa watawala wanafanya ufahari na kuishi maisha ya isirafu bila kujali, wanatembelea magari ya bei ghali, kulipana mishahara mikubwa na posho za kuzidi kiwango, kupeana incentives kiasi kwamba hawajali kabisa na kutambua kuwa upande wa pili wa shilingi Watanzania wanaoogelea kwenye tope la umaskini.

Mikopo ni karibia kila week sasa kuna mkopo mpya unatangazwa wa mabilioni kama si matrillion ya fedha ila bado wananchi tunakamuliwa vilivyo. Maendeleo yanayomgusa mwananchi yako wapi? Maboresho ya huduma za kumpa unafuu mwananchi mbona hatuyaoni? Kama mtu anaweza akafia hospitali sababu tu Network ya NHIF iko down mna sababu gani ya kuendelea kukamua kodi kwa wananchi?

Miradi haimaliziwi, kazi ya kutengeneza mikataba mipya ya kudokoa 10% ndio inaonekana kushika hatamu awamu hii. Tulishayasahau haya kwanini tunarudishana nyuma? Hilo ndilo ambalo wananchi waliwatuma huko serikalini? Bila aibu wala soni mnasifia ubadhirifu wa fedha za kodi zetu kwa kuhonga wapinzani na kupalilia udokozi kwa kuita "Kulamba Asali". Hii ni zaidi ya dharau jamani.

Mmeanzisha tozo za miamala juu ya 18% VAT ambayo ilikuwa inachajiwa awali ila bado hamjaridhika..Sahizi mnataka mlete tozo kwenye ving'amuzi. Tupeni basi mchanganuo wa hizo tozo mnazokusanya. Mlidai zinajenga mashule hizo shule hazijaisha tu kwa mabilion mliokwisha kusanya kwa mwaka mzima? Mmeleta tozo kwenye luku hizo pesa zote zinaenda wapi na mtaani hela hakuna? Huduma za kijamii mbovu kabisa. Toeni malengo na utekelezaji wa kila senti ambayo imekusanywa kwenye tozo za awali kwanini mnaficha ripoti za makusanyo na matumizi?

Msituchukulie poa jamani hii hali inachosha kiukweli tunapoenda watu wanaweza wakawa mbogo tukavuruga ule urithi aliotuachia hayati baba wetu wa Taifa.
 
.. Wazungu wajanja Sana kujikata, unaongozwa na mtu ambaye ndugu zake wapo 4000 km away ,mpak uarabuni huko , hawezi tambua taabu unayopitia wewe uliyepo namtumbo , ndongobeshi , huko unyamboni au huko newala
 
Watanzania hawataki kulipa kodi.

Sio hawataki kulipa kodi! Kodi zimekuwa nyingi kodi ya majengo ambayo ni kwenye luku, tozo miamala, pia kama una biashara utanielewa kodi zake, bado walete kwenye king’amuzi mara sijui kodi ya kichwa hii si balaa hii mkuu?? Kiukweli tunakoelekea tutachapana hazarani niamini......

Na huku street pesa hamna mkuu! Hawa viongozi wameshidwa kuwa na ubunifu ni namna gani serikali inaweza kukusanya pesa..... zaidi yakutukomoa natamani tuchapane makofi aise
 
Rais wa Malawi aghairi safari za nje ili kubana matumizi



Serikali ya Malawi itaokoa TZS milioni 608.13 kutokana na kufutwa kwa safari mbili za Rais Lazarus Chakwera kama sehemu ya hatua za serikali za kubana matumizi.

Rais Lazarus hatahudhuria mkutano wa Wakuu wa Serikali wa Jumuiya ya Madola mjini Kigali, Rwanda, na Kongamano la Maendeleo ya Mfuko wa Opec huko Vienna, Austria, badala yake atawakilishwa na mawaziri.
Waziri wa Fedha, Sosten Gwengwe amewaambia waandishi wa habari kuwa serikali haijapiga marufuku safari za nje isipokuwa zile zisizokuwa na ulazima.

“Safari nyingine haziwezi kuepukika, kwa mfano Rais anakabidhi uenyekiti wa SADC kwa DRC mnamo Agosti, hiyo ni safari ambayo haiwezi kuwakilishwa,” amesema.

Malawi mwezi uliopita ilitangaza kushuka kwa thamani ya 25% ya fedha yake, Kwacha, kama sehemu ya marekebisho ya kupata ufadhili kutoka kwa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).
 
Back
Top Bottom