Bill Lugano
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 1,189
- 6,450
habari zenu watanzania? nimerud nilikuwa busy sana na mikutano ya kimataifa USA,UK,Canada, Sweden, Egypt, South AFrica, Nigeria, Russia na France. nashukuru angalau nimerudi kwa week moja hivi nije angalia mnaendeleaje hapa nchini. naambiwa tu kuna joto n.k. sijui maana sijapata nafasi ya kuwa sehemu ambayo haina AC. so sijui, kama kuna joto kweli poleni.
nimeamua kuandika uzi huu kuzungumzia hivivyombo vya vya usafiri kama Vitz, IST, Altezza,Subaru n. k kwa kweli vinasumbua sana barabarani hasa sisi wenye magari tunapokuwa tunaendesha kwenda kazini au kwenye mikutano Hotel kubwa kubwa mjini. unakuta hawa waendeshaji kama wote akili zao zinafanana. wanakimbia kimbia muda wote na kusababisha ajali au usumbufu. hawa jamaa huwa wanapenda sana kuchomekea wenzao. hawavumilii kabisa foleni. muda wote akili zao ni kama zipo juu juu hawajielewi kabisa sijajua labda ni sababu ya pia hutu tudude tulivyo twepesi na hatueleweki eleweki nato.
juzi nilikuwa na Range yangu akaja mtu akanichomekea ghafla mbele yangu. kakanigusa kidogo na kuchubua rangi yake ikabaki kwenye gari langu. nilishuka tu taratibu na kumuuliza sasa inakuaje na alikuwa ana wahi nini?akawa hana majibu. akaja traffic kuja kupima maana alikuwa karibu. akaonekana jamaa ana makosa. so analipaje.... jamaa choka mbaya yaani mtu anatembea na fujo zote kwenye wallet ana 280,000? nlishangaa sana. hata fedha hana ana pesa tu hizo kidogo za kuwekea mafuta ila bado anakuwa na fujo barabarani utadhani naye anaendesha gari.
hutu tu dude kwa kweli tupigwe marufuku maana tunaweza leta maafa makubwa siku zijazo. tumekuwa twingi sana barabarani. yaani ukigeuka huku unakuta kuna IST, SUbaru ukiangalie kule nako ni hizi hizi tu. Magari unaweza kuta ni machache sana kwa kweli. nashauri serikali ipige marufuku matumizi ya vyombo hivi vya usafiri hasa mjini .... tubaki tu na magari ambayo ndo yataruhusiwa kwenda mjini. hivi vitu vingine viishie huko huko uswahilini kama kinondoni,masaki,sinza,kijitonyama,tabata,msasani n.k
ikishindikana basi zijengwe barabara maalum ambazo sisi tutakuwa tunalipia kwa mwezi tsh 5,000,000 kupita hizo barabara kuepukana na usumbufu wa ist,vitz,subaru,altezza n.k maana ni sumbufu sana kwa wengine.