Serikali iangalie namna ya kuwasaidia vijana moja kwa moja. Athari za baadaye ni kubwa zaidi

Serikali iangalie namna ya kuwasaidia vijana moja kwa moja. Athari za baadaye ni kubwa zaidi

Sas watu mnashinda Kubet unataka nani awatafutie fursa? Saiz tuu pm amezindua mfuko wa kukopesha Vijana ila mko busy TikTok, whatsup na upuuzi mwingine badala ya kutafuta fursa..

Kwenye Kaz zote za ujenzi za TanRoads na Tarura wanatengwa Asilimia 30% Kwa Ajili ya makundi maalumu ya vijana,wamama na walemavu..

Utaratibu ni ule ule lazima usajili kikundi chako au kampuni Yako na kusajili Wala hakuna gharama zozote..

Kuna Kaz za kusafisha mitaro,kufagia,kuchimba mifereji,ujenzi mdogo mdogo nk nk

Halmashauri pia zinatoka hizo pesa tena huko naona ni rahisi mnaweza buni mradi wa tofali wakawanunulia mashine na wao ndio wakawa wateja maana wanajenga Kila siku
Acha kuongea pumba
 
Hao kula kulala sahau kuhusu mabadiliko, kwani ujui methali ya mwenye shibe
 
Hali ya maisha imewachanganya vijana wengi, mazingira na hali sio rafiki kwa biashara, Ajira na zenyewe hakuna.

Vijana wamesoma na sasa wameishia mitaani, nguvu ya wazazi nayo imeishia hapo, serikali nayo imeishia hapo, kwanini kijana asichanganyikiwe.

Ongezeko la watoto wa mtaani nao ni zao la vijana ambao wapo kwenye kundi hili hapo juu kutokana na Kukosekana kwa maadili pamoja na familia bora yenye uchumi Dhabi tickets.

Ulevi wa kupindukia, wizi, utapeli, kubeti, kamari. Na michezo mingine michafu limekuwa kimbilio la vijana wengi wasomi kama njia mojawapo ya kujipa furaha na kuondoa msongo wa mawazo.

Pamoja na mambo mengine mengi Kukosekana kwa mfumo rasmi wa maisha juu ya vijana wetu ndio chanzo kikuu cha uovu unaendelea hivi sasa, kama vile ulawiti, ubakaji, mauaji pamoja na kuongezeka kwa wagonjwa wa akili.
Ccm inataka watu maskini, ni rahisi kuwatawala,ndio maana wanaona Bora wengi waishie kuwa bodaboda.
Kuna njia mbili za kutawala watu,ya kwanza,kuwatisha(frighten them)kwa njia za vyombo vya ulinzi na usalama.
Nyingine ni kuwakatisha tamaa(demoralize).
Mtu mwenye aliyeelomika(educated)mwenye afya(healthy),na anayejiamini(confident)sio rahisi kumtawala.
Ccm inataka watu machawa!!!wakati watoto wao ni masimba,wanaendesha mandege,wapo kwenye ajira UN,nje ya nchi,mburukenge wanahimizwa wawe bodaboda na maskini ya Mungu,wanaona ni Sawa,ndio haki yao,waliumbwa kuja kuwa wretched of the earth.
 
Mda mwingine ayo yote ni matokeo ya mtu kukata tamaa baada ya kusahaurika
Kukataa tamaa na kasahaulika ni stage moja mbaya sana, ndo huelekea vijana kufanya hayo maovu yote
 
Viongozi wengi wa Africa hawajali kuhusu wananchi wao bali wanajiangalia wao na familia zao, hakuna sera nzuri za kuangalia uwiano kati ya Mwananchi na kiongozi, ndo maana nchi nyingi za kiafrica ni maskini kutokana na sera mbovu za nchi
 
Hali ya maisha imewachanganya vijana wengi, mazingira na hali sio rafiki kwa biashara, Ajira na zenyewe hakuna.

Vijana wamesoma na sasa wameishia mitaani, nguvu ya wazazi nayo imeishia hapo, serikali nayo imeishia hapo, kwanini kijana asichanganyikiwe.

Ongezeko la watoto wa mtaani nao ni zao la vijana ambao wapo kwenye kundi hili hapo juu kutokana na Kukosekana kwa maadili pamoja na familia bora yenye uchumi Dhabi tickets.

Ulevi wa kupindukia, wizi, utapeli, kubeti, kamari. Na michezo mingine michafu limekuwa kimbilio la vijana wengi wasomi kama njia mojawapo ya kujipa furaha na kuondoa msongo wa mawazo.

Pamoja na mambo mengine mengi Kukosekana kwa mfumo rasmi wa maisha juu ya vijana wetu ndio chanzo kikuu cha uovu unaendelea hivi sasa, kama vile ulawiti, ubakaji, mauaji pamoja na kuongezeka kwa wagonjwa wa akili.
Unajua kijana asiye na ajira yuko tayari kufanya lolote katika maisha yake apate chochote kitu ili ku survive, kijana wa namna hii hana tofauti na wale wanajitoa muhanda kwa ukosefu wa imani dhabiti ndani yao..
 
Wabadili mfumo wa elimu kijana akimaliza form four aende Veta kujifunza stadi za maisha kama uselemala, welding, Ujenzi, na mafani mengine miaka mitatu then aende chuo kwenye ma theory inayotuzalishia wasomi ma bishoo mtaani
 
Unajua kijana asiye na ajira yuko tayari kufanya lolote katika maisha yake apate chochote kitu ili ku survive, kijana wa namna hii hana tofauti na wale wanajitoa muhanda kwa ukosefu wa imani dhabiti ndani yao..
Naunga mkono hoja
 
Back
Top Bottom